Halafu ongezea katoka bara! Kwa muda niliokaa huku, kuna ugumu wa kuoa mwanamke wa huku hata kama ni muislamu mwenzao kutoka bara. (Utakuwa shahidi)
Mwanaume wa huku ataoa mwanamke kutoka bara, lakini ukweli kutoka moyoni huyo mwanamke atapata sana mateso ya kisaikolojia hasa kama wanakaa huku Zanzibar! (Utakuwa shahidi)
Wanawake kutoka bara iwe muislamu au mkristo huchukuliwa kwa jicho la tofauti na ni baya.Wanaume ndiyo kabisa.(Utakuwa shahidi).
Sifa za wanawake wa huku hazitofautiani sana na wanawake wa pwani. Viburi , ujeuri na kupandisha sauti ni kawaida tu.Mwanamke wa huku hapigwi na ni nadra sana kukuta mwanamke kapigwa (Utakuwa shahidi)
Baba mkwe anakuozesha mwanae kwenye usia anamwambia "akikushinda njoo nyumbani chumba chako bado kipo".
Dini imesema ahudumiwe kwa kila kitu yeye kazi yake kukaa ndani na kuangalia nyumba, watoto na kumstarehesha mume.Wenyewe wamezoea, wewe je? Je, dunia tuliyopo inaruhusu hivyo ukilinganisha na vipato vyetu tulio wengi?