Habarin wana JF.
Mimi ni kijana mwenye Umri 28. Moja kwa moja niende kwenye kichwa husika. Nimekua mvutaji wa bangi kwa miaka kama mi3 mpaka sasa, Nataman sana niache kwasabab nimeambiwa ni dhambi na dini hairuhusu kila nkijitaid kukaa bila kuvuta najikuta narud tena.
Naomben ushaur nifanyaje?
Yesu anasema katika Mathayo 11:28
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."
Hiyo bangi ni mzigo unaokulemea. Kwa nguvu zako huwezi kuacha. Lakini ukiamua sasa hivi kutubu dhambi hiyo na dhambi zote nyingine, na kumpokea Yesu moyoni mwako kwa imani atawale maisha yako, hiyo kiu ya bangi ataiondoa kabisa. Kama uko tayari kufanya hivyo fuatisha sala hii kwa moyo wako wa dhati kisha utaona badiliko. Omba sasa maneno yafuatayo:
"Ee Mungu, nakiri mimi ni mtenda dhambi. Nimekukosea kwa kuvuta bangi. Natubu uovu huu. Naomba Mungu unisamehe dhambi hii na dhambi zangu zote nyingine. Niko tayari kuziacha kuanzia sasa. Ee Yesu, nakupokea ndani ya moyo wangu, uwe Bwana na Mwokozi wangu. Utawale maisha yangu kuanzia leo. Nakushukuru Mungu, naamini umenisamehe na kuniokoa, katika Jina la Yesu Kristo. Amen."
Kama umeomba hivyo kwa dhati/kwa moyo wako wote, tayari umeokoka. Mungu amekusamehe na hiyo hamu ya kuvuta bangi hutaisikia tena.
Kinachokupasa sasa kutenda, anza kusoma Neno la Mungu(Biblia) kila siku na kumwomba Mungu akuwezeshe kuishi maisha ya ushindi siku zote. Tafuta pia kanisa lolote linalofundisha kweli yote ya Neno la Mungu ili ujifunze zaidi jinsi ya kuishi maisha hayo mapya ya wokovu. Ubarikiwe sana ndugu.