Nataka nihame Tanzania, Naombeni mnipe ushauri kati ya Macau na Singapore ni wapi kuzuri zaidi?

Nataka nihame Tanzania, Naombeni mnipe ushauri kati ya Macau na Singapore ni wapi kuzuri zaidi?

Kwa kukusaidia tu, huko hakuna msosi wa buku jero

Hakuna chumba cha elfu 30

Maisha ni magumu mara 10 ya hapa hasa kwa mgeni.

Kazi hakuna, kuishi lazima serikali ikujue.

Nakushauri (japo hutaki) kaa chini uwaze upya, mi mara mia ukajichimbie vijijini ndani ndani ulime nyanya, tikitiki na mazao mengine kuliko kwenda kutesekea huko.

Kikumbuke kisa cha yule baharia aliekimbia kwao na kwenda mbali, baadae maisha yakamchapa na akawa anakula na nguruwe

Mkuu mimi mwenyewe najipanga kwenda DUBAI, connection ninazo lakini najipanga hasa.

USIFANYE MAAMUZI UKIWA NA HASIRA

NA

USIFANYE MAAMUZI UKIWA NA FURAHA SANA

Tunza ushauri wangu utakuja kukusaidia.
Lakini mwana mpotevu hakwenda kusaka life bali alikwenda kuponda starehe. Hela zilipoisha ndio joto akaipata. Sasa mie siendi kuponda starehe bali naenda kusaka maisha.
 
Mi nakushauri upambane uende Belize, hii ni nchi pekee kule kwa walatino ambayo inazungumza kingereza na hakuhitaji Visa, japo iko mbali ila kuna fursa nyingi za kazi, kila la heri mkuu
 
Why usiende Bahamas?
Nako hakuna viza halafu karibu sana na Miami..

Macau nasikia kuna kazi nyingi since kuna casino nyingi hutashindwa
 
Unataka kwenda kufanya nini huko na Hamna kazi kwa wageni wasio na vinakua vya kuishi maana wewe visa tu ya miezi mi3 ikiisha bs tena either utoke au ushakua overstay person ukidakwa imekula kwako hizo sehemu ulizotaja sahau kupata kazi hata za Hanja Hanja Kama Europe au Amerika
 
Screenshot_20210125-200527.png
 
Nina elimu kubwa tu na umri unasogea. Hela ya kujiajiri sina. Naombeni mnipe ushauri kati ya Macau na Singapore ni wapi kuzuri zaidi? Nimechagua hizi nchi kwa sababu ukiwa na passport ya Tanzania huhitaji viza kuingia.

Natanguliza shukrani zangu.
Pamoja na kujiita msomi ni kichwa maji unakimbilia kwa waliokomaa na kutotoka kuijenga nchi yao unataka akujengee nani huku
 
Inanda
Nenda Google search huko mkuu Utapata taarifa nyingi kuhusu unachokihitaji.
Nb:cost of living kwenye hizo nchi Ni kubwa.
 
.
 

Attachments

  • EC8A442E-2EF9-42CC-87E5-55D684299C2E.jpeg
    EC8A442E-2EF9-42CC-87E5-55D684299C2E.jpeg
    72 KB · Views: 13
  • 1D5D87D0-645E-4685-826F-716EEACDC311.jpeg
    1D5D87D0-645E-4685-826F-716EEACDC311.jpeg
    76 KB · Views: 13
Kumbe Elimu pekee haitoshi kumfanya mtu atoboe kimaisha na kushia kuwaza kuikimbia nchi.

Naishauri Serekali kama haiwezi kuajiri wahitimu wengi, itoe mikopo kwa wahitimu wa vyuo pale wanapomaliza chuo ili wapate mitaji ya kujiajiri na sio mikopo ya kuwasomesha.
Kwani kila mtu anaweza kuzalisha huo mkopo aliopewa ili apate faida?
 
Mi nakushauri upambane uende Belize, hii ni nchi pekee kule kwa walatino ambayo inazungumza kingereza, japo iko mbali ila kuna fursa nyingi za kazi, kila la heri mkuu
Asante sana kwa ushauri. Vipi, na yenyewe ukiwa na passport ya Tanzania huhitaji viza?
 
Back
Top Bottom