[emoji28][emoji28][emoji28] mwaka flani baada ya kumaliza chuo, nilipata tempo kufundisha kishule kimoja cha kata. I wasnt gettig paid that much, wazee wenzangu wa tempo mnajua.
So, ili kuongeza kipato nikaanzisha kimradi cha kupiga picha wanafunzi nikusanye zile buku buku zao. Nilitoka chuo na ki-digital camera changu kidogo kiroho safi. Na nilijua soko langu kubwa litakuwa kwa mabinti. Mabinti na picha aisee....
Ile shule ilikuwa na hostel. Pamoja na kwamba nilikuwa napiga picha huku nje fresh tuu, ila nilipata wazo. Kwamba kama nitaweza kuwafuata wale mabinti kule kwenye mabweni yao naweza kupiga picha nyingi huko kuliko huku. Sasa naingiaje?!
Ikabidi nimtumie huyo binti. Mwanafunzi wa kidato cha nne. Demu wa kwenda. Mshapu yani. Nilimuona yeye anaweza kunifaa kwa kazi ile.
Yaani awe anaenda na kamera mabwenini kwao, anawapiga hukoo, then wakitosheka, ananiletea weekend naenda kuzisafisha, au najiiba katikati ya week. Namletea anazigawa. Kisha ananiletea pesa.
Nilipiga noti, nae alianza kula vimandazi bwana, na viwali kwa mama muuza si haba.
Nikajichanganya sasa. Huyu shetani huyu!!. Si nikamtongoza yule binti bwana! Yaani ile mikutano ya wawili ya kupeana picha na hela ikanifanya nijione mimi ndio mwaaaamba, nikatupa vokali.
Hata kabla vokali zangu hazijapewa majibu ya kueleweka zile hela za picha zikawa sio zangu tena, zikawa zetu. Demu akaanza kuzila anavyotaka. Akiniletea hesabu imepwaya namuuliza kulikoni ananijibu zingine katumia. Aisee!
Project yangu ikayumba, mwisho niseme tuu ikafa. Maana sasa ilibidi nimnyang'anye kamera na sikupata mwingine kirahisi wa kufanya nae kazi. Si unajua tena vyanafunzi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwahyo mleta maada, take it from here. Kupanga ni kuchagua.