Nataka nitumie mbinu hii kupata ajira

Nataka nitumie mbinu hii kupata ajira

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,275
Reaction score
3,316
Nataka nijitoe ufahamu kwa kuandaa CV yangu vizuri, halafu nitaandika barua moja kwa moja kwa Rais ikulu, nitaambatanisha vyeti vyangu vyote kisha nitavizia siku rais yuko Dar.

Ntapeleka barua yangu pale geti la ikulu, ntawakabidhi walinzi kisha nitawaomba wamfikishie mheshimiwa hiyo barua yangu.

Kwa wataalamu wa protocol, je hapa nitakua nimevunja sheria yoyote ya nchi?
 
Hutatoboa hapo getini😅
barua wanapokea fresh tu pale getini yaani hata ukiwa na mtu unamfahamu anafanya kazi pale ukaenda kumuona wanaasiliana naye na anaweza kuja pale getin (reception) ukaonana naye na mkaongea kabisa kuna hadi sehemu private ya kuongea hapohapo reception, kuna reception kubwa pale ina hadi masofa ya kukaa wageni. Walinzi wa pale getini kazi yao ni kuwa screen watu na magari tu na kuwaelekeza reception. ambapo ndipo wanapokea barua zote na kusikiliza shida ya mtu na kumshauri jinsi wanavyoona inafaa, Walinzi wa pale hawawezi kukuzuia labda wakubaini you are security threat
Ila pitia geti la huku juu wizara ya fedha sio kule baharini.
hiyo barua yako na uhakika rais itamfikia na ataisoma , ila kujibiwa inategemea na bahati yako manake anapokea barua nyingi sana za watu wenye ishu mbalimbali za kiofisi na kibinafsi .
Barua nyingi anazipeleka kwa wahusika wazishughulikie mf ma RC or KM. kama ni kuhusu malalamiko fulani
 
Back
Top Bottom