Jibu maswali yafuatayo kwanza;
PART A
1. Utajiri ni nini?
2.Utajiri kwako ni nini kwa maana ya kumiliki,mfano uwe na nini?
3.Unataka utajiri ili iweje?
4.Kwa mujibu wako sadaka ni nini?
5.Mpaka sasa umetoa sadaka kiasi gani ili uwe tajiri?
6.Kitu au jambo gani KWAKO thamani yake ni kubwa na haipimiki au kununulika (priceless)? Mfano UHAI,SEHEMU YA MWILI,UANAUME au UANAMKE n.k
7.Chanzo cha utajiri kitanufaika vipi kwa wewe kuwa sehemu ya wakazi/raia wake?
MASWALI HAYA HAYANA UPANDE WA GIZA WALA MWANGA JIBU KADRI UNAVYOJUA
PART B
Hapa kuna mzani wa alama 1 HADI 10, 1 ni alama inayomaanisha kidogo sana na 10 ni alama ya juu kabisa.
5 ni wastani. Weka alama kwa kila swali.
Je kwa kila kauli hapa chini unajipa alama ngapi?
1. "Najitoa sana kusaidia kwa mawazo na vitendo ninaposhindwa kutoa pesa kwa watu walio katika nyakati ngumu katika jumuiya na jamii yangu"
2."Najiskia vizuri na kuwatakia heri ninapoona hata watu niliowapuuza au kuwaona wa kawaida wanapata mafanikio kabla yangu"
3."Natumia takribani masaa mawili mpaka manne YA ZIADA kila siku kufanya jambo moja ambalo nataka hata nisipokuwepo linitambulishe"
4. "Mara nyingi nimejitoa mstari wa mbele kuongoza jambo chanya bila kujua wala kujali maslahi binafsi"
5. "Kila ninapodhani najua najikuta ninachojua ni kidogo sana,nachukua hatua kujifunza zaidi"
UKIMALIZA KUWEKA ALAMA, ZIJUMLISHE zikiwa chini ya 85, basi jua kuna changamoto katika kuwa tajiri.