Natamani kufa

Hakuna kutoroka hali n ngumu kwa Wote
Kikubwa n kukomaa na kumuomba mungu


yaan ukijaribu kutoroka halafu tukakudaka na jela miaka 45
 
Sasa mkuu, kila unachogusa kina fail ndio sababu ya kuwa depressed hivi?. Umegusa mara ngapi?. Mbona kuna waliogusa mpaka mara elfu kumi na bado hawakuwa na mawazo kama haya?..Don't give up, gusa vitu strategically huku ukimtanguliza Mungu mbele mambo yatakaa sawa.
 
Mkuu ondoa hizo fikra akilini mwako, hapa nilipo ninapitia Hali ngumu sana Karibu Kila angle kiafya na kiuchumi pia. Tangu January hadi sasa mwaka unaisha Bado nateseka & at the same time I don't see the light at the end of the tunnel lakini Bado nasonga mbele. Mawazo hayo sometimes hunijia na natamani sana kuyafanyia kazi lakini naweza kusema MUNGU kama kaendelea kuweka hai jua ana kusudi lake, may be He's preparing the best version of yourself Ili mambo yatakapokuja kupinduka uwe mtu Bora zaidi. Hakuna mtu ambae a hundred percent mambo yake yanaenda tu, may be kuna watu wana nyakati ngumu kuliko hata wewe lakini Bado Wana tumaini ndani Yao.

Pambana mkuu!! PULL UP YOUR SOCKS, nyakati ngumu Zina muda wake. Jaribu kumshirikisha MUNGU, usipambane kujikwamua kwa akili yako pekee


Believe 🙏🙏
 
Wewe nae bana.

Achana na hizo changamoto Anza upya kabisa.

FUTA hayo mawazo ya kijima.... Panga upya.
 
Kujikataa ni sehemu ya stress nyingi, kuwaza jambo moja muda mrefu na halibadiliki, Ondoka hapo kimtizamo, Achia unayowaza yasahau kabisa, achia kila kitu fanya lile linalowezekana kwa wakati huu ijapokuwa kila mara utahisi shinikizo kutoka nje usigeuke nyuma, unao wakati mzuri sasa wa kufanya mageuzi binafsi tena.
 
Kausha muombe mungu, kila kitu ni temporary…..jua kila mtu ana magumu kwa kipimo chake
 
Kama mtu inapitia Sana hali ngumu ya kiuchumi au kimaisha share apa ndoto unazoota mara Kwa mara tatizo wengi watu hatuzielewi huwa zinaonyesha tatizo na nin cha kufanya
 
Pole sana Mkuu, jaribu kuhama eneo ulilopo, kama umejenga hama kwa muda. Pia jaribu kubadili mfumo wa maisha.

Ila pole sana mkuu
 
You may not start a conversation with the following recipients: Mshana Jr. ujumbe ninao pata
Usikate tamaaa,vuta subira kidogo,amini Kuna kesho njema.
Nenda nyumba ya ibada,fanya ibada.
Biblia inasema tumtwike Yesu fadhaa zetu.
Hata km humjui na Wala humwamini Yesu,wewe fumba macho,omba hivi(Bwana Yesu naomba unisaidie )
Utasaidika
 
Maisha ni vita hayahitaji lelemama. Pigana kwa kila silaha mpaka ushinde usikate tamaa. Wengine tumepitia moto sana miaka ila tulivuka baada ya kutokutaka kuonewa huruma Bali kwa kupambana. Pambana
 
Usife mwamba,maana huko kwenyewe tunakoenda hatujui kukoje,ukute nafuu na hapa....pambana mwanangu
 
Soma historia za akina Thomas Edison. Mtu anafanya jaribio mara 10,000 na hakati tamaa hadi anachokitaka kipatikane. Ikibidi fanya mabadiliko. Anza na kubadili kufikiri kwako,ikiwezekana hama eneo,n.k. Fanya mabadiliko chanya kwenye Kila eneo la maisha yako.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
siyumwe say something, tunataka tukusikie kama upo sawa,

Kumbuka ni bora kuishi maisha ya dhiki kuliko kufa.

Unaweza kutueleza kinachokusibu tukaona namna ya kukusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…