Natamani kuifanya familia yangu kuwa kama ya Bakhresa na ya akina Mo Dewji, nipeni muongozo

Swali binafsi unalotakiwa kujiuliza na ndugu zako Wana maono hayo?
Iko hivi ukiwa na pesa na ukiwa unasupply Kwa kila mmoja utadhani ulichelewa kuwasilisha hayo maono kwani kila mmoja atakusapoti kila unalosema.
Ila supply ya pesa ikikata utajua kuwa uliona nuru gizani Kwa mwanga WA mshumaa.
 
Baadhi wana maono kama yangu pia kuhusu level ya uchumi naweza sema tupo sawa tu tofauti ni kuwa mimi ndio msomi pekee
 
Lengo langu sio kufanana nao kimuonekano ila kiuchumi na kimaendeleo ya familia kama vile ushikamano na ushirikiano

Pia sio kwa mimi pekeangu kwa familia nzima

Wewe umekula chumvi nyingi nipe muongozo mjukuu wako
Anza kwa kusali sala tano lwa siku kama Bakhresa na Mo.

Ukipenda boga penda na ua lake.
 
Waislam sala tano kwa siku ni lazima siyo chaguo. Hazina udhuru.
Twende kwa mtu personal, kuwa muislam sio kuswali swala tano

Kwa upande wa Mo na Bakhresa unao uhakika kuwa wanaswali swala tano?

Nahitaji mbinu za kuifanikisha familia yangu kiuchumi nipe mbinu za kijasiliamali tofauti na hizo za swala tano
 
Wakuu kwenye familia yetu tuna asset muhimu kama ardhi, mashamba na nyumba kadhaa ila usimamizi ndio hakuna.

Kama mtoto niliesomeshwa na kuhitimu elimu ya juu natamani siku moja familia yangu iwe familia kubwa na yenye miradi endelevu kwa manufaa ya familia na jamii kwa ujumla.

Wakuu, kwa heshima na taadhima naomba mnipe muongozo na mawazo kipi nifanye ili kufikia malengo yangu ya kufaifanya familia iwe kama ya Bakhresa.

Natanguliza shukrani.
Ukitaka kufanikiwa hama unapoishi, kajifiche sehemu na mtaji wako na uanze biashara. Familia zetu za kiswahili mara nyingi hazitaki kuona mafanikio kwa baadhi ya wanafamilia, khususan pakiwa na tofauti au kupishana maneno kwa wanafamilia.
 
Hapa nazungumzia uchumi wa familia nzima sio mimi pekeangu

Kuhusu mimi nipo na mishe zangu tofauti na eneo la nyumbani na kila mtu kwenye familia kwa sasa anapambana kivyake ni kama kila mtoto kasusa mirathi ya mzee
 
Hapo ndio makosa tunafanya, unataka kuanza upya baada ya kuanzia alipoishia Mzee wako na kuendelea kwenda mbele.

Kama Mzee wako alijenga, huhitaji kujenga zaidi ya kuboresha hapo alipojenga na wote mkae hapohapo.
Mzazi ana nyumba kiwanja cha kutosha buguruni kwa mfuga mbwa kinatosha vyumba viwili na hata gari haiingii unaboresha nini ?

Unaenda nunua eneo eka tano unashusha ghorofa la kueleweka hapo lenye Park xa magari ya kutosha na garden juu
 
Twende kwa mtu personal, kuwa muislam sio kuswali swala tano

Kwa upande wa Mo na Bakhresa unao uhakika kuwa wanaswali swala tano?

Nahitaji mbinu za kuifanikisha familia yangu kiuchumi nipe mbinu za kijasiliamali tofauti na hizo za swala tano
naona trunazunguka hapohapo. Nimeshakueleza, ukipenda fata hukupenda usifate.

Mmeshindwa kumuelewa Yeshua mtaweza kunielewa mimi? Mawee.
 
Andiko langu halihusiani na dini japo mimi mwenyewe ni mwanadini kwa hapa tupeane ushauri kuhusu suala lililopo mezani
usiogope kusali sala tano kama unataka kuwa kama Bakhresa au Mo. Ni jema kwako hilo kama lilivyo kwao.

Maisha yana msingi wake, na msingi wa kwanza ni sala tano.
 
Sawa naona wewe umejikita kwenye imani ila imani na vitendo imani pekee haitoshi
 
Wakuu kwenye familia yetu tuna asset muhimu kama ardhi, mashamba na nyumba kadhaa ila usimamizi ndio hakuna.

Kama mtoto niliesomeshwa na kuhitimu elimu ya juu natamani siku moja familia yangu iwe familia kubwa na yenye miradi endelevu kwa manufaa ya familia na jamii kwa ujumla.

Wakuu, kwa heshima na taadhima naomba mnipe muongozo na mawazo kipi nifanye ili kufikia malengo yangu ya kufaifanya familia iwe kama ya Bakhresa.

Natanguliza shukrani.
Mwongozo kachukue kwa hao unaotaka kufanana nao!
 
Back
Top Bottom