Hapo inategemeana scenario ya kupishana kwenu, na hilo litaamua kama hicho unachokifanya ni sahihi au ni upumbavu.
1. Kama yeye ndiye chanzo cha mgogoro kisha anataka wewe ndio uwajibike kuweka mambo sawa na anakushinikiza kwa ukimya wake, usithubutu kabisa kuwa wa kwanza kumtafuta na hata akikutafuta usiingie kingi moja kwa moja mpaka pale atakapokubali kulizungumzia kosa lake na akiri kuwa amejirekebisha. Ukijifanya kuendeshwa na hisia ukamtafuta wewe, basi tambua umekubali kuwa chini ya miguu yake kwa kipindi kirefu sana na lazima huko mbele yatakufa hayo mapenzi.
2. Kama wewe ndio uliyemkosea na mpaka sasa wewe ndio unasubiri kutafutwa ili ufukie makosa yako, tambua kuwa unafanya upumbavu kwasababu yeye pia ana haki ya kuumizwa na kile unachomkosea na kusubiri yeye aliyeumizwa ajishushe ni utoto usiokuwa na faida.
Kama wewe ndio ulikosea, mtafute kiume kisha umuombe msamaha kama mwanaume (Sio kwa kujilizaliza na kuomba huruma yake), muelezee nini kilitokea na kwamba kama mwanaume wake utajitahidi kuziondoa hizo dosari. Baada ya hapo kama atakusamehe endeleeni, kama ataendelea kununa na kutaka ujishushe zaidi, ujinyenyekeze na kulialia kwake kwa kuomba huruma, maana yake anatafuta kuku manipulate kupitia kosa lako. Kaa kimya, nawa mikono kisha ondoka kwenye hayo mahusiano.