Natamani Ma-Celebrity wa Bongo wangekuwa kama Ma-Celebrity wa Nigeria

Natamani Ma-Celebrity wa Bongo wangekuwa kama Ma-Celebrity wa Nigeria

Halafu kingine nachoshangaa kutokana wingi wawo wa watu wanaotumia mitandao unakuta Celebrity mkubwa ana followers 100 K ila ukija Bongo Celebrity kajamba nani ana Followers Milioni 1.

Kuna mahali niliona wakisema Princess Tiffah wa mondi ana followers wengi instagram kuliko mtoto mwingine yeyote wa celebrity wa umri wake akiwemo Blue Ivy wa Beyonce+Jay Z.

Ishu sasa ni kwa namna gani umaarufu wa social media unawaingizia hela bongo celebrity kuacha endorsement uchwara na malipo ya you tube...
 
You nailed it honey Money Penny
Tatizo la ma celebrate wetu ni kufake, yaani hata hiyo Prado unayosema anaendesha unakuta amehongwa na mbaya zaidi kadi ya gari yenyewe anayo mwanaume😀😀😀
Wameshindwa kuomba mitaji ili wafanye biashara na uwekezaji kwa manufaa yao ya baadaye, wao wanaomba wapangishiwe apartments Mbezi beach.
Ila Money Penny njoo uwape semina elekezi hao mastaa wetu angalau wajitambue sisi wanaume wa JF tutagharamia posho ya kujikimu na malazi😀😀😀
 
Elimu elimu elimu! Celebrity wa ki Nigeria mwenye elimu ndogo ana degree. Ndiyo maana tunasema ukisoma unajikomboa hata ukitaka kuwa mwizi au Malaya utaifanya vizuri inavyotakiwa, lakini hawa wa kwetu asilimia kubwa ni form four failures na darasa la saba, halafu pia wengi wa celebrity wa ki Nigeria wametoa kwenye familia nzuri. Sisi wa kwetu wengi ni watoto wa uswazi halafu hawataki kubadilika,
U nailed it.....bongo celebs wenye elimu kubwa eti O LEVEL tena kazungusha! Utatoboaje hapo kwa mfano?
 
Kama yule Ini Edo ana maapartments mia kidogo....yaan ye kila wiki anabadilisha ndinga mpya na za maana only!

Hadi Tonto Dikey mvuta bangi, kicheche nae tajiri mbaya yaan...chinekeeeee
 
Mpaka leo Wema, Wolper, Uwoya, Ant Eze wanaringishiana Nyumba za kupanga!
Hongera sana kwa dada Jide na SHISHI BABY mambo yenu si haba.
Sooon Shilole atawafunika hao hapo juu maaana anaonekana ana uchu wa maendeleo hataki kuuza sura.
 
Nimewacheki Mademu, Celebrities, Singo Maza, Madanga na Malaya waliokubuhu huko Nigeria, wala sijaenda pengine

Jinsi walivyoendelea, kila mwanamke ana maisha yake... wanamiliki Majumba, Wamewekeza kwenye Real Estates, Movie Industries, wamejenga Ma-Appartments... akaunt zao zinasoma Billion Nairas... Magari yao wanacheza kwenye BMW, AUDI, PORCHE Cars ... Wanalipa kodi...

Mwanamke ukimkuta Instagram anajidai lakini anajidai kwasababu ana maisha yake na hela zake ... na yupo Proud ...anasema kabisa mimi zamani nimeanza vibaya lakini sasa hivi nina wafanyakazi 50 mpaka 100 wananitegemea... haijalishi ulipoanza Mwisho ndio kila kitu, finali ndio kila kitu!

TUKIRUDI HUKU KWETU BONGO:

Wanawake kama hao hao wa Nigeria, wapo Buzy Instagram wanagombana nani kaenda kwa Mganga... sijui nani kampeleka mwanae kwa Mganga akiwa mtoto kwanza... sijui Mara Kuchambana... kiki za kijinga jinga... huko kwa Youtube ndio kabisa ni vituko... Kuzungukana na kuibiana Mabwana... sasa si bora muibiane Mabwana lakini muwe mnaenda Mbele kuliko kurudi nyuma!

Wengine Buzy wanapost mapicha wamepiga mamekapu ya elfu 70 kwenye akaunt hawana hata mia wanategemea wakadangwe

Tunaomba jamani Nduguzetu Mnaojiita Ma-Celebrity, Madanga Maarufu, Malaya mliokubuhu angalau basi mjifunze kwa nduguzetu wa Nigeria!

Nyie mkiendesha TOYOTA mnajiona mmefiiiiika! oh Nina Prado!


Tunaomba Wadada wa Kitanzania muamke basi Mtalala mpaka lini?

Mimi ndio maana nikiwa nje ya Africa wakiniuliza where are you from nasemaga Am from Ethiopia au Mouritious!

Kiru!

Ngoja niendelee kuandika hadithi mie!


Porsche not porche
 
Umeandika upuuzi wa hali ya juu...
hujawaonea huruma kwa dhambi ya uzinzi waitendayo....hv mnajisahaulisha kama kuna kiama???pls tell .... people the good thing....usiwa encourage uzinzi
 
Back
Top Bottom