I can feel your pain…man! Uzi wako unawakilisha majuto ya watu wengi sana hasa graduates…mtu anakaa nyumbani miaka 5+ bila kazi ya maana na hapati kazi ambayo alitarajia pamoja na elimu yake…! Inafika wakati anajuta kabisa kusoma anajuta kabisa kusomea alichosomea!
Ukweli ni kwamba wahitimu wa miaka hii hasa 2010 kwenda mbele wanapitia kipindi kigumu sana sana na wengi wana majuto na depression kubwa sana…mwingine unakutana nae unaweza fikiri hapati chakula kabisa lakini sio kweli bali ana majuto na sononana hatari …….
Kwakweli ni vigumu kuvaa viatu vya mtu aliyesoma vizuri na akasota zaidi ya miaka kumi mtaani kwakweli huyu mtu anahitaji matumaini makubwa na faraja ya aina yake kusonga mbele na kusimama!
……
Mkuu pole sana lakini ninachoweza kusema zidi kupambambana pengine hukupangiwa kupata kazi unayoitafuta pengine ni wakati wa kuangalia upande mwingine!
Lakini lamsingi unatakiwa kujua kuwa kujuta ni kujikatia tamaa na kumkatia Mungu tamaa…Mimi naamini kwa Mungu hakuna kuchelewa wala kuwai…Kwa kuwa Mungu amekupa uhai wapaswa kumshukuru kwa hilo….. usijute usijute …usijute ….Ungali hai….
Ofcourse , wengi wao wamebaki kupambana kupata vimia mbili wale na kuvaa vizuri alafu wanajirusha facebook kila uchwao ukijiuliza labda wana maisha jibu ni hapana wanafanya vile sababu ya mawazo waliyonayo na pia wanatamani labda jamii ijue kuwa wana maisha mazuri .
Guys , siwakatishi tamaa ila ninalo neno kwenu , acheni kuwaza kuwa ulipoteza muda kuwepo shule ila tambua uliongeza chochote kitakachokufaa maishani .
Zaidi napenda kuwakumbusha kuwa mnayo nafasi na mawazo ya kuamua leo kuondoa dhana potofu ya kuamini kuwa elimu uliyoipata ni lazima uajiriwe .
Anza leo kuamini na kuishi kwa kujua haukupata elimu ili uje kuajiriwa bali kuzitatua changamoto unazokutana nazo .
Dear rafiki zangu , mnaowajibu wa kuamini kuwa dunia imebadilika inahitaji akili nyingi na nguvu kidogo ila karatasi ya darasani haitoshi kama hauna uthubutu na kujituma hivyo nipende kusema kitendo cha kuilaani Elimu mnakosea sana .
Zaidi waza unavukaje mabonde yaliyo mbele yenu .
Leo nakutumeni tena kwenye jamii mnazoishi , kawatizame walimu , madaktari , manesi , maaskari na kada zinginezo maisha wanayoishi alafu njoo kwangu nikunong'oneze .
Hao wenye hizo kada walitamani kuajiriwa kama ninyi na kweli wakapata hizo nafasi ila nipe walau watu kumi walio katika hizo kada walio na maisha mazuri yakukutisha ?
Come on friends of mine , watakuwepo wawili kati ya sita , lakini unajua mafanikio yao ni nini ? Ni nyumba ya kuishi , gari la kutembelea nalo utembea siku za mama Samia zikiwa on fire lakini vipi wao ni kuwa walijiwekeza hapana ni big no wengi wao ni mikopo ndiyo maana hawang'ai sura japo mnawaona wametoboa .
Sikatai kuwa hawana mafanikio wote ila ni mmoja katika kumi aliye na maisha bora tena ya kujiwekeza pembeni ambaye leo ukimuambia acha kazi haoni shida .
Sasa rafiki zangu wasaka ajira still unahitaji kuingia kwenye mtego ule ule ?
Utanijibu nataka niingie kutafuta mtaji [emoji3][emoji3] Rafiki mtaji ni wewe na ideas ila sio mikopo katu huendi mbali nature itakukamata .
Aisee itoshe kukuambia jitafute kwa jasho lako na nguvu zako utafika uendeko .
Mungu awasaidie na awatie nguvu katika upambanaji wenu .
Mwenzenu nipo Mbeya Pazuri kwa sasa hapa Mbeya naendelea kumalizia hela ya Mkopo niliochukua ABSA .
Karibuni na poleni sana .