Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 4,107
- 9,671
Waliouliwa kulikuwa na Dereva Taksi maarufu Ndugu Juma akiishi Sinza. Wale jamaa walikuwa ndugu wa yule mama alikuwa Waziri aliyesema Lowasa atakufa matokeo yake akaanza yeye Celina Kombani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukikaa nafasi ya aliyekuwa RPC Msaidizi Bw Abdalah Zombe unaziona zikipatikana mkuu?Hivi zile hela zilipatikana?
Nijuavyo mimi jamaa bado anadunda.Aliyewatuma ni Bwana Zombe. alishatangulia Jehanam
eti ni kweli alisha RIP?Nijuavyo mimi jamaa bado anadunda.
Hii kesi ya kitambo sana dah!Kumbe alikuwa bado hajanyongwa tu huyu jamaa?
Hii ni Habari njema Sana kwa Wapenda HAKI hapa Tanzania.Mwangwi wa sauti ya Wakabing'oko!
SSP Christopher Bageni, atanyongwa hadi kufa! Ndivyo Mahakama ya Rufaa ilivyoamua. Hakika uamuzi wa leo ni wa mwisho katika mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia wala pa kupinga, ni kweli Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Hivyo Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Its over! imeisha!!
Hawezi kukata rufani tena kwa sababu hukumu ya leo ni review, marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo 16 Septemba 2016 ambapo alihukumiwa kunyongwa "hadi kufa" na jopo lile la majaji watatu wakiongozwa naye Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya 'kujadili' tena shauri hilo labda iwe kupitia msamaha wa Rais
View attachment 3243016
Sasa kwao wasiokumbuka, Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi, wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye, akiwa na wenzie, wakiongozwa na aliokua Kaimu RPC Dar Abdallah Zombe, walituhumiwa "kupanga njama" za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro. Sasa A. Zombe anadaiwa kuongoza wenziye kwenye 'mpango' huo baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.
Hivyo 'wakaikamata' gari waliyokua wameikodi! Na kisha Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Kisha "wakapora" madini pamoja na fedha zote walizokuwa nazo. 'Wakawafunga' vitambaa vyeusi usoni, na hadi pingu mikononi. Wakapigwa risasi za 'kisogoni' na kuuawa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha. Aise!!
Na kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi, yaliyokua yanarushiana tu risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda 'tume' ya Jaji Kipenka kuchunguza jambo hilo. Ikabainika jamaa, hawakuwa Majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa "familia moja". Mama mmoja alipoteza wanae watatu pia watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao. Na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za watumishi wachache!
Zombe alifanikiwa 'Kuchomoka' kwenye kesi hii baada ya kusota "rumande" kwa miaka kadhaa!! Lakini Bageni 'alikutwa' na Hatia! Akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa na akafeli. Akaomba review ya kesi sasa rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA. Yani si kunyongwa tu!
Hakika waliomtuma hawapo nae Segerea. Wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Na Wanaohangaika nae sasa hivi angalau kumfariji ni familia yake, A. Zombe hayupo OCD wake hayupo na hata IGP wa wakati ule hayupo pia. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa pekee!!
Hakika hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo i.e kuteka kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Aliyekutuma hatakuwepo, basi utasimama mwenyewe kutoa hesabu, ya maovu yako. Kama sio hapa duniani basi hata kule mbinguni. Lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo, Wema ni Mbegu. Na Ubaya pia ni mbegu, humea hukomaa na ni lazima uvune! Usijitume wala Kutumwa kwa mabaya, Hukumu ya Mungu ni ya haki. Hakuna jasiri wa kudumu!!
Nchi yangu, Machozi yako, Nchi tamu ya uhuru!
Mbona anawaka ananawiri kama afisa wa kitengo fulani muhimuHakika waliomtuma hawapo nae Segerea. Wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Na Wanaohangaika nae sasa hivi angalau kumfariji ni familia yake,
Keshatangulia siku nyingi. Mbele yake, nyuma yetu.Selina kombani ameshafariki ama yupo hai ?
Selina kombani ameshafariki ama yupo hai ?
Aseeh kuna siku nilijiuliza mbona simsikii.....Ameshakufa
Aseeh ndo nimejua saa hivi.... Apumzke kwa amaniKeshatangulia siku nyingi, mbele yake nyuma yetu.
Abdala Zombe Yupo Morogoro Pale Mkambalani
Inauma Sana Wamewauwa Watu Ambao Ni Innocent Kwa Tamaa Zao
Ni huzuni kwa kweli! Haya maisha kuna wakati yanakosa ladha kabisa!Mwangwi wa sauti ya Wakabing'oko!
SSP Christopher Bageni, atanyongwa hadi kufa! Ndivyo Mahakama ya Rufaa ilivyoamua. Hakika uamuzi wa leo ni wa mwisho katika mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia wala pa kupinga, ni kweli Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Hivyo Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Its over! imeisha!!
Hawezi kukata rufani tena kwa sababu hukumu ya leo ni review, marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo 16 Septemba 2016 ambapo alihukumiwa kunyongwa "hadi kufa" na jopo lile la majaji watatu wakiongozwa naye Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya 'kujadili' tena shauri hilo labda iwe kupitia msamaha wa Rais
View attachment 3243016
Sasa kwao wasiokumbuka, Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi, wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye, akiwa na wenzie, wakiongozwa na aliokua Kaimu RPC Dar Abdallah Zombe, walituhumiwa "kupanga njama" za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro. Sasa A. Zombe anadaiwa kuongoza wenziye kwenye 'mpango' huo baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.
Hivyo 'wakaikamata' gari waliyokua wameikodi! Na kisha Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Kisha "wakapora" madini pamoja na fedha zote walizokuwa nazo. 'Wakawafunga' vitambaa vyeusi usoni, na hadi pingu mikononi. Wakapigwa risasi za 'kisogoni' na kuuawa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha. Aise!!
Na kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi, yaliyokua yanarushiana tu risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda 'tume' ya Jaji Kipenka kuchunguza jambo hilo. Ikabainika jamaa, hawakuwa Majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa "familia moja". Mama mmoja alipoteza wanae watatu pia watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao. Na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za watumishi wachache!
Zombe alifanikiwa 'Kuchomoka' kwenye kesi hii baada ya kusota "rumande" kwa miaka kadhaa!! Lakini Bageni 'alikutwa' na Hatia! Akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa na akafeli. Akaomba review ya kesi sasa rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA. Yani si kunyongwa tu!
Hakika waliomtuma hawapo nae Segerea. Wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Na Wanaohangaika nae sasa hivi angalau kumfariji ni familia yake, A. Zombe hayupo OCD wake hayupo na hata IGP wa wakati ule hayupo pia. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa pekee!!
Hakika hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo i.e kuteka kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Aliyekutuma hatakuwepo, basi utasimama mwenyewe kutoa hesabu, ya maovu yako. Kama sio hapa duniani basi hata kule mbinguni. Lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo, Wema ni Mbegu. Na Ubaya pia ni mbegu, humea hukomaa na ni lazima uvune! Usijitume wala Kutumwa kwa mabaya, Hukumu ya Mungu ni ya haki. Hakuna jasiri wa kudumu!!
Nchi yangu, Machozi yako, Nchi tamu ya uhuru!
Mbele yake nyuma yetu tena?Keshatangulia siku nyingi, mbele yake nyuma yetu.