Natamani Watanzania tuanzishe Sanduku la kuchangia nguo tusizozitumia kwa wenye uhitaji

Natamani Watanzania tuanzishe Sanduku la kuchangia nguo tusizozitumia kwa wenye uhitaji

kanisa katoliki wana utaratibu wa aina hiyo,
mara nyingi wanaufanya kipindi cha kwaresma ingawa hawazuiwi kufanya hivyo wakati wowote unaofaa,

nadhani kwa kuanzia,
unaweza kuanza nao na hatimae malengo na nia yako njema ikatimia kwa ufanisi zaidi.

Mwenyezi Mungu akubariki sana kwa moyo wako wa ukarimu na huruma kwa wahitaji 🐒
Asante mkuu
 
Wakuu, nimefanikiwa kutembea baadhi ya mikoa vijijini kama Dodoma, Kagera, Kigoma, na Mara.
Hali ya watanzania wenzetu vijijini hairidhishi, nawaza hata tungeanzisha visanduku vya misaada ya nguo ambazo hatuna matumizi nazo ili ziwasaidie wengine huko.
Najua wengi tuna nguo ambazo zipo tuu kwenye kabati na hatuzitumii, natamani tufanye hiki kitu, sio lazima kusubir misaada kutoka nje ikiwa hata hiki kidogo tunaweza kusaidiana sisi kwa sisi
Huyu ndo kijana mwenye mchango mkubwa katika taifa letu
 
Nguo zipo kiboa karume labda wanunuliwe kuliko kusambaziana magonjwa ya ngozi na hayo matambara yaliyokwisha valiwa
Nani ananunua? Na atanunulianwangapi? Bro tunaongelea vijiji sio kaya..
Je hizo za karume hazikuvaliwa na watu?

Tunapoongelea kutoa nguo maana yake baada ya hilo zoezi kuna hatua zinafatwa kama kusafishwa kwa madawa na kuondoa uwezekano wa contact disease….
Ingekua kugawa nguo ni magonjwa bas masoko ya mitumba yangeshafungiwa
 
Ni magonjwa ndio , na hayawezi kufungwa ile ni biashara, hizi gharama za kutibu hizo nguo bora wanunuliwe mpya tu .
 
wazo zuri na linawezekana kabisa kufanyika…
 
Ni magonjwa ndio , na hayawezi kufungwa ile ni biashara, hizi gharama za kutibu hizo nguo bora wanunuliwe mpya tu .
Mkuu tembea hata nchi kubwa duniani uone…

Ukienda UK wana donation bins kila mtaa, Zimewekwa maalum kwa makubaliano ya nchi, nenda pia marekan wanazo donation bins za kuweka vitu bora usivyovitumia ni tofaut na dust bins… maana yake unachoona hakikufai kuna mwingine kwake ni ndoto..
 
Back
Top Bottom