Natangaza rasmi kuachana na masuala ya Siasa, nina ya kujutia mengi

So sad, some JF members wanasikitisha sana. Matatizo yao binafsi hayawezi kuwa issue ya kitaifa.
 
Tunaomba msaada wa mbinu kukisimamisha ACT-WAZALENDO kuwa chama kikuu cha upinzani 2020. Najua kushinda urais ni ngumu pia kwanini umeamua kuachana na siasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatusaliti sio?...
 
Ungekuwa mstaarabu ungewaomba msamaha uliowakosea kwanza. Hata hivyo naamini uamuzi wako ni mzuri
 
Leo baada ya miaka yote hiyo wewe ni mtu mwoga sana

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi shiriki mauaji ila niliwahi kushiriki mtego wa kuwajua wanaomtukana Rais mtandaoni
 
Nashukuru kwa kuniruhusu, hope utakua very sincere! Swali, kwa mtazamo wako, je bila hizi "figisu" unafikiri CCM wanaweza kui-face Chadema?
Ndiyo kwasababu pamoja na Umafia wa CCM bado upinzani nao hawajawa serious kwenye ishu za kuongoza, kila siku hao hao kina Mbowe
 
Kuachana na shetani ni jambo jema. CCM hakiwezi kuwa chama chenye baraka mbele za Mungu. Na wote waliojishikamanisha na ibilisi huyu, laana ijuu yao na wana wao. Chama hiki kinaua, kinateka, kinatesa na kudhulumu watu. Lakini pia chama hiki ni cha kishirikina.

Kuna mjumbe mmoja wa CCM alielezea jinsi pale Mwanza, usiku wa manane walivyokusanywa kwenye ukumbi wa jiji usiku wa manane, tarehe 14 Octoba 2015, na kisha viongozi wao wa mkoa kuwaacha na mganga wa kienyeji (mchawi) aliyewapa dawa na maelekezo ya namna ya kwenda na dawa hizo usiku ule kwenye vituo vya kupigia kura. Yule mama mjumbe wa CCM alisikitika sana lakini akasema nilitekeleza kwa sababu ya hofu. Anasema waliambiwa atakayeshindwa kutekeleza kwa kadiri ya maelekezo, atakuja kujutia.

Hata siku moja, Mungu haelekezi kuua, kubagua, kutesa, kuonea au wewe kujiona bora kuliko binadamu wengine. Yeyote anayeyafanya hayo, hakika ni lazima, ametoka kwa shetani, anatekeleza matakwa ya shetani. Shetani baada ya kukutumia, lazima akuangamize.

Pale Mwanza, tazameni yaliyompata Mabina, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa. Alikuwa mbabe hasa, aliyeogopwa na hata na mawaziri. Pamoja na ubabe wake, aliuawa kwa unyonge zaidi ya kuku. Jiwe moja dogo la mwanakijiji lilimwondolea uhai. Tupu zake zikakatwa na wanakijiji kudhihirisha chuki dhidi yake. Hatufurahii kifo lakini kuna vifo vya laana, na Mungu anatukumbusha tuliosalia na kujisahau.

Roho ya mwanaCHADEMA, mwanaCCM, mwanaCUF, mwanaACT au hata asiye na chama, ina thamani kubwa mbele za Mungu. Unaweza ukaua leo, ukatesa, ukaonea, ukabagua, ukapendelea, ukateka, ukapoteza watu, na kwa ujinga ukajiona mwamba kweli maana unatenda lolote utakalo, kwa kauli tu usiowapenda wanatetemeka na kuangamia lakini usichokijua, ni UNYONGE ulio nao. Unyonge wako unaweza kuzidiwa hata ule wa simbilisi.

Wababe wengi mwisho wao huwa ni wa kinyonge sana, na wala huwa hawaondolewi na wabaya wao waliowategemea. Huondolewa na wasiowatarajia kabisa.

Britinica, hongera kwa kuondoka kwenye unyonge, shetani ni mnyonge. Huwakamata walio wanyonge zaidi. Ambatana na Mungu mwenye nguvu na mamlaka makubwa, nawe utaufurahia ukuu wake. Mungu akujaze neema zake zitakazokufanya uuchukie uovu milele. Mwovu anayetubu na kubadilika, ni furaha kubwa kwa Mungu na ushirika wa watakatifu wake waliopo mbinguni na duniani.
 
Pamoja mkuu wanguu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…