Natangaza rasmi kuachana na masuala ya Siasa, nina ya kujutia mengi

Natangaza rasmi kuachana na masuala ya Siasa, nina ya kujutia mengi

Ndiyo kwasababu pamoja na Umafia wa CCM bado upinzani nao hawajawa serious kwenye ishu za kuongoza, kila siku hao hao kina Mbowe
Nazungumzia CCM, ok, kwahio tunaweza kuhitimisha kuwa CCM wako leo hapo walipo kutokana na "figisu" za kuwatesa na pengine "kuwapoteza" Wapinzani wake? Au pengine kwa maneno mepesi, CCM wananuka damu?? Una maoni gani hapa??
 
Now that umekiri kuwa mulikuwa munapora ushindi halali wa upinzani kwa hila,ili uwe msafi inabdi uanike mbinu hizo,na pia naamini umeona huruma kwa maovu dhidi ya watu safi,itasaidia ukianika ili watu waenende tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mkuu kwa kutambua, kukiri kisha kuazimia kuiacha njia ovu uliyokuwa umeiendea kwa muda mrefu. Ni kweli inawezekana kwa namna moja ama nyingine, kazi yako iliacha maumivu makubwa kwa watanzania wasio na hatia, hata hivyo Mungu wetu ni Mungu wa Rehema, anasamehe kila mtu anayekiri makosa yake. Ni kwa sababu hiyo, naamini utasamehewa.
Nakutakia maandalizi mema ya Noeli bro.
 
Kwahiyo umechoka kutumiwa na mhutu Dunderhead au malipo mhutu atoi siku hizi.
 
Nimekuwa naandika Sana kuhusu mambo ya siasa,
Nimekua napewa baadhi ya tetesi nazirusha hapa,

Nimekuwa na Mlengo wa Chama Cha Mapinduzi kwa Muda mrefu

Kuna muda nimeshabikia mambo ya Kinyama yaliyofanywa na Chama changu cha Mapinduzi

Nayakumbuka Matukio

1.Nimeshiriki sana Kuiba kura za wapinzani

Nimeshiriki Mafinga,Bukoba vijijini, Nimeshiriki Hata kura za kitaifa, mbinu nyingi CCM wanazitumia kuiba kura,

2.Nimeshirika Cyber war kwa kipindi cha Kampeni za Magufuli, na kushiriki kuwachafua viongozi wa upinzani

3.Nitaandika Nitaandika mengi ila naishia hapa kwa sasa


Suala linaloniuma na Kujuta ni la Mheshimiwa Lissu Kupigwa Risasi nikafurahia, lakin kadri muda ulivyopita nika kaa na kuwaza kwamba tuweke chuki pembeni tutangulize ubinadamu
Sitashiriki Kampeni yeyote ile
Sitashiriki Siasa kivyovyote vile


Nitabakia kuwa Mtazamaji tu

Britannica,
Vladivostok, Russia
umeshalaaniwa na Mungu ameshakupatiliza wewe kizazi chako.hadi cha nne.
 
mtatajana wote taratibu tu.
Siku zinakuja mbaya sana ktk.maisha yao Walipemda sana kuzifurahisha nafisi zao kwa maovu dhidi ya wenzao. Vipesa wanavyolopwa kwa kudanyia anasa vinawazuzua sana. Na waapia kila aliyekula sh hata moja iliyotokana na pesa zao za udhalim wamelaaniwa.
 
Kuachana na shetani ni jambo jema. CCM hakiwezi kuwa chama chenye baraka mbele za Mungu. Na wote waliojishikamanisha na ibilisi huyu, laana ijuu yao na wana wao. Chama hiki kinaua, kinateka, kinatesa na kudhulumu watu. Lakini pia chama hiki ni cha kishirikina.

Kuna mjumbe mmoja wa CCM alielezea jinsi pale Mwanza, usiku wa manane walivyokusanywa kwenye ukumbi wa jiji usiku wa manane, tarehe 14 Octoba 2015, na kisha viongozi wao wa mkoa kuwaacha na mganga wa kienyeji (mchawi) aliyewapa dawa na maelekezo ya namna ya kwenda na dawa hizo usiku ule kwenye vituo vya kupigia kura. Yule mama mjumbe wa CCM alisikitika sana lakini akasema nilitekeleza kwa sababu ya hofu. Anasema waliambiwa atakayeshindwa kutekeleza kwa kadiri ya maelekezo, atakuja kujutia.

Hata siku moja, Mungu haelekezi kuua, kubagua, kutesa, kuonea au wewe kujiona bora kuliko binadamu wengine. Yeyote anayeyafanya hayo, hakika ni lazima, ametoka kwa shetani, anatekeleza matakwa ya shetani. Shetani baada ya kukutumia, lazima akuangamize.

Pale Mwanza, tazameni yaliyompata Mabina, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa. Alikuwa mbabe hasa, aliyeogopwa na hata na mawaziri. Pamoja na ubabe wake, aliuawa kwa unyonge zaidi ya kuku. Jiwe moja dogo la mwanakijiji lilimwondolea uhai. Tupu zake zikakatwa na wanakijiji kudhihirisha chuki dhidi yake. Hatufurahii kifo lakini kuna vifo vya laana, na Mungu anatukumbusha tuliosalia na kujisahau.

Roho ya mwanaCHADEMA, mwanaCCM, mwanaCUF, mwanaACT au hata asiye na chama, ina thamani kubwa mbele za Mungu. Unaweza ukaua leo, ukatesa, ukaonea, ukabagua, ukapendelea, ukateka, ukapoteza watu, na kwa ujinga ukajiona mwamba kweli maana unatenda lolote utakalo, kwa kauli tu usiowapenda wanatetemeka na kuangamia lakini usichokijua, ni UNYONGE ulio nao. Unyonge wako unaweza kuzidiwa hata ule wa simbilisi.

Wababe wengi mwisho wao huwa ni wa kinyonge sana, na wala huwa hawaondolewi na wabaya wao waliowategemea. Huondolewa na wasiowatarajia kabisa.

Britinica, hongera kwa kuondoka kwenye unyonge, shetani ni mnyonge. Huwakamata walio wanyonge zaidi. Ambatana na Mungu mwenye nguvu na mamlaka makubwa, nawe utaufurahia ukuu wake. Mungu akujaze neema zake zitakazokufanya uuchukie uovu milele. Mwovu anayetubu na kubadilika, ni furaha kubwa kwa Mungu na ushirika wa watakatifu wake waliopo mbinguni na duniani.
Acha kumhusisha Mungu na mambo yenu ya siasa za ovyo ovyo. Umeweka bandiko refu kama unalazimisha tuamini kuwa Mungu wa Abraham Isaka na Yakobo ana upande wa siasa na upande huo ni ule ulio wewe. Siasa za kibongo zina watu wa ovyo kila upande including hao wachawi uliowasema.
 
Acha kumhusisha Mungu na mambo yenu ya siasa za ovyo ovyo. Umeweka bandiko refu kama unalazimisha tuamini kuwa Mungu wa Abraham Isaka na Yakobo ana upande wa siasa na upande huo ni ule ulio wewe. Siasa za kibongo zina watu wa ovyo kila upande including hao wachawi uliowasema.
Mungu gani unamzimungumzia ambaye ameliacha taifa lake?
 
Wewe akili Zako ndogo na zitakugharimu

Wewe unapewa tetesi unazirusha bila kuzifanyia tafiti.(wewe mwehu)

Unyama ulifanywa na CCM ni upi,
Weka evidence.

Wewe uliajiriwa na mtu binafsi uibe kura hukuwa unalipwa na CCM kwa wizi mliokuwa mnafanya.

Kuchafuana kwenye siasa ni Jambo la kawaida na ndio maana zikaitwa siasa.

In short naona umekurupuka tu kutoka usingizini Wala hujielewi

Nakushauri kwasababu unazijua mbinu Za kuiba kura nenda upinzani wape mbinu hizo ili 2020 upinzani ushike Dola.

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Humjui vizuri unaemkosoa hivi, funga bakuli lako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa uamzi mzuri na mgumu kama ni kweli unachokisema!, ila ningekuomba usiache siasa ila fanya siasa safi, nyeusi wambie watu kuwa ni nyeusi na kama ni nyeupe waambie watu ni nyeupe!.

Naamini unayo yafahamu ni mengi katika siasa za nchi yetu, ukifanya hilo nililo kushauri watu wataelimika, watapona na kujua siasa za nchi yetu!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya Magufuli kutomteua huku alifanya maovu mengi kwa sababu ya ccm sasa ameamua kuzila.
 
Back
Top Bottom