Natarajia kufunga ndoa, nipe maneno ya hekima yatakayonisaidia

Natarajia kufunga ndoa, nipe maneno ya hekima yatakayonisaidia

Habari wakuu,
Mimi ni ME, wiki chache zijazo natarajia kuingia katika ndoa, naomba wenye uzoefu na wanaofahamu mambo wanipe maneno ya hekima yatakayonisaidia kwenye maisha ya ndoa.
Usiniambie kataa ndoa kwakua nimeshafanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Ndoa ni gereza hakikisha umemtafuta mfungwa mwezio wakuvumuliana katika hali zote hata mauti iwatenge
 
USITARAJIE UTOFAUTI MKUBWA SANA kwa mwanamke wako kiasi cha kuhisi wanayopitia wenzio huko nje kila siku, eti wewe hayawezi kukupata. Kila mmoja ana mapito yake, ikiwa haukuamua kuyafuatilia kabla ya ndoa basi achana nayo na usiwahi kuyafuatilia.

KILA LA KHERI.
 
Misingi ya ndoa yenu inaanza mapema kabisa,
0. Suala la uchumi lina nafasi kubwa sana katika kuleta stability ya ndoa yenu, tafuta hela kwa nguvu zote, ila kwa halali.
1. Kama kitu hukipendi basi mkeo ajue tangu mwanzoni kua hukipendi, sio mwanzo unamuachia kisha baadae unasema hukitaki, kama mmekubakiana mshirikiahane simu basi iwe hivyo.
2. Usijihusishe na zinaa ni mbaya na inaharibu familia
3. Kuoa isiwe kigezo cha kuwafungia vioo marafiki na ndugu lakini pia usiwape mda mwngi kuliko mkeo, ubalance
4. Mkeo ni mtoto wako wa kwanza wa kike, umchunge, wahuni wengi
5. Mpende mkeo, wazuri hawaishi huko mtaaani,
Nitaongeza baadae
 
1. Mpelekee moto.
2. Mpe hela.
3. EXpect less from her
4. Hakuna jipya sanaa kwenye ndoa.
5. jitahid usiwe mbinafsi , u need to sacrifice more
6. Dont forget urself completelly, u need comfort too..usiwaze sana familia ukajisahau mpaka wewe.
7. Chochote utakachofanya kwa mkeo, dont think u will be appreciated so fanya kwakua ni wajib wako kufanya usifanye ili wakushukuru kumbuka u will never be seen a hero until they lose you.
8. You are not perfect..your wife too...kila mmoja ana madhaifu yake.. appreciate yale machache mazuri aliyonayo..na wewe pia usijalaumu sanaaa pindi unashindwa kukidhi vigezo vyake.....u will not be completelly enough to her soo kila unachoweza fanya usichoweza endelea kujifunza.
9. Jitahid ku maintain your qualities.Mkiwa wawil maisha ya kila siku ni lazima mmoja atamu affect mwenzake positivelly au negativelly..na hili huwa ni ngumu ku notice untill it is too late unajikuta kuna tabia unazo ambazo hukua nazo kabla yake...so either yeye akuvute au wewe umvute uoande wake..ukindwa sanaa hayo mawil basi jitahid ubaki unaffected.

10. Spending sometimes in religious or spiritual moments ni muhim sana ukiwa kwenye ndoa.

11. Usipende kusuluhishwa sana na watuu ..maisha ni ya kwenu and you are in controll as a man..

12. Pesa ndio nguvu za kiume kwa mwanaume.
Mkeo atakuvumilia kwenye yoooote ila sio kwenye njaa..Hapa atakusomesha namba zote zilizoko duniani.

Niishie hapa.
NB.
Nimekushauri kutokana na experience yangu ndogo ya miaka 9 kwenye ndoa.
 
Habari wakuu,
Mimi ni ME, wiki chache zijazo natarajia kuingia katika ndoa, naomba wenye uzoefu na wanaofahamu mambo wanipe maneno ya hekima yatakayonisaidia kwenye maisha ya ndoa.
Usiniambie kataa ndoa kwakua nimeshafanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Compromise ndo siri ya mchezo.

Na pia usitumie akili zako za darasani au ofisini kuendesha ndoa.

Jitahidi kupuuzia vitu vidogo dogo mara kwa mara na usishindane sana KE, ingawa yeye atakutest mara nyingi.

Jitahidi matatizo yenu muyamalize wenyewe pasipo raia wengine
 
Habari wakuu,
Mimi ni ME, wiki chache zijazo natarajia kuingia katika ndoa, naomba wenye uzoefu na wanaofahamu mambo wanipe maneno ya hekima yatakayonisaidia kwenye maisha ya ndoa.
Usiniambie kataa ndoa kwakua nimeshafanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Kila la heri mkuu
 
Usijichekeshe ovyo mbele yake km kakuchekesha kachekee chooni ajue mda wko ukiwa unatoka asubuhi ila kurudi asikukariri, asijue unashabikia timu gn mda mwingi uso wa mbuzi na wakati wa misosi hakikisha unakula sana ili akiwazia namna unavyokula akili ya kipigo kikubwa itamjia. Usisahau kutimiza majukumu yako km mume
 
Usiwe mtu wa kukurupuka, mkanye asikuambie fulani kanitongoza maana hawacheli
Usijaribu kumpiga hata kwa kosa kubwa labda uwashirikishe wazazi ikibidi

Mpendane ila usiwe yule wa kila kitu Honey, sweetie, baby hapana be a man

Mpe matumizi yake kila wakati bila hiyana na epuka michepuko kama umeamua kuingia huko
Simama na mke wako tu
Mengine ntaongeza
 
Back
Top Bottom