Nategemea kwenda Shinyanga kwa pikipiki aina ya Boxer, CC 125

Angalia mkuu usije ukaibeba begani pale itakapogoma, huo umbali si mchezo!
 
Utatumia pesa Nyingi sana kwenda na kurudi na usalama wa maisha yako ni 40%…mafuta,oili Nk…

Kata tiketi mbezi panda Basi nenda then hio boxa Muachie mtu deiwaka elfu 10 kwa siku…
 
Jamaa anachoongea kina ukwer lakn ugumu wa safari na gharama zisizo za ulazima ndicho tunachokwepa😄
 
Umeanza vizuri sema umeharibu hapo kwenye wosia,ni umakini tu njiani.
 
Sasa mkuu atapataje uzoefu bila kuendesha safari ndefu?Au awe anaanza kwa safari za km 300 kwanza halafu ndipo atafute road trip ya km 1000?
 
Mchawi koti tu
 
...pikipiki hiyo sio ya masafa mkuu utaionea... Inaweza kuhimili lakini hyo ni ya root za town boss... Afu chuma inameremeta mkuu hyo angalia barabara za shinyanga nyekundu kama ugoro wa subiana
 
Mkuu bado hujaanza safari tu?? Usitishwe tembea br,zingatia tu walivyo shauri wadau,usisahau ibada na uodaye s hapa,ukifika manyoni nijuze nikupekuku na mguu wa mbuzi
 
Wakakata moto kivipi, kwan hizo za masafa wanafikaje?
 
Wakakata moto kivipi, kwan hizo za masafa wanafikaje?
 
Kufika unafika ila usikamie safari,nenda kwa vituo ukijihisi umechoka pumzika yani usiwe na haraka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…