Nategemea kwenda Shinyanga kwa pikipiki aina ya Boxer, CC 125

Nategemea kwenda Shinyanga kwa pikipiki aina ya Boxer, CC 125

Ndugu wanajamvi nategemea kwenda Shinyanga nikitokea Dar es salaam kwa Piki piki boxer cc125 mwenye uzoefu itakuwa vyema ukanisaidia.

Nataka kujua mafuta naweza kutumia kiasi gani. Je, nijiandae kwa changamoto gani barabarani pikipiki hii ninayotaka kuitumia ni mpya. na nina tegea kwenda na kurudi....

View attachment 2760635.mrejesho,
Nilibadili safari nikaenda Tanga, muda huu saa 11:30 nipo Mkata. Nilitoka dar es salaam saa 7:30 asubuhi nilikuwa naendesha speed 70 Hadi 80 kwakweli tunaogopa TU.

Ila Kwa boxa IPO vizuri sana barabarani imetulia japo ukizidi speed 90 inayumba nadhani ni kutokana na kuwa sikuwa nimebeba mzigo.

Usafiri wa piki piki ni hatari sana kwani Kuna baadhi ya madereva awazingatii sana Sheria za barabarani.

Nilinusurika kugongwa nikasukumiwa Kando ya barabara baada ya dereva kuovatake bila kujali kuwa nilikuwa mwendo Kasi nakuja Kwa mbele yake...nisingetoka nje ya barabara ninge gongana uso Kwa uso na gari iliyokuwa inaovertake.😭😭😭

Ila Kwa ufupi ukiacha uchovu kidogo barabara haipo busy. Hivyo haikuwa hatarishi sana. Mliokuwa mnaogopa kusafiria pikipiki ndugu zangu msiogope PIKI piki ni usafiri mzuri TU na WA haraka sana.
View attachment 2761644
Angalia mkuu usije ukaibeba begani pale itakapogoma, huo umbali si mchezo!
 
Utatumia pesa Nyingi sana kwenda na kurudi na usalama wa maisha yako ni 40%…mafuta,oili Nk…

Kata tiketi mbezi panda Basi nenda then hio boxa Muachie mtu deiwaka elfu 10 kwa siku…
 
Mkuu fungua moyo. Waweza tembea na pikipiki hio umbali wowote.
Dar- shy ni pafupi.
Mimi nikuwa natembea mbeya to Bukoba via Iringa/Tabora huku nikitumia siku 2 na nilikuwa naenjoy balaa.
Cha msingi ni kukipenda chombo.
Nilikuwa natumia Sinoray 150-18

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Jamaa anachoongea kina ukwer lakn ugumu wa safari na gharama zisizo za ulazima ndicho tunachokwepa😄
 
Mkuu mi Nina boxer cc150 Huwa napiga sana hizo safari mpaka Kuna nyakati nishawahi sinzia nikiwa road kutokana na uchovu, nakumbuka Kuna siku nilisinzia mpaka pkpk ikasimama yenyewe ndipo nikashtuka nlikuwa natumia Honda Manji(cc125).

Kwa safari yako Dar to Shy
Hakikisha pkpk ipo fresh Kwa maana umeifanyia service ya kutosha na hakikisha nat zimekazwa vzr(zinakawaida ya kulegea, ni hatari sana), tairi weka oko(ziwe tubeless), honi iwe poa,sight mirror, breaks zote ziwe vzr, indicators zote ziwe poa, Oil tumia zenye kumudu umbali mrefu km vile Oryx, Mogas, Advanced etc. Pia beba baadhi ya spana muhimu kama vile size 10, 19,20 etc Kwa ajili ya kutatulia matatizo madogo madogo. Funga walau tofali moja la block ili kupata utulivu na kupunguza kuyumbayumba ukipigwa na upepo mkalli.

Kwa upande wako, Vaa jacket nzito sana, kofia ngumu,viatu vya kupanda mpaka kwenye ugoko, miwani, gloves ngumu za mikono ili kujikinga na baridi nyakati za usiku, begi ambalo utaweka vinywaji hasa energy na maji.

Kuhusu wese, Lita moja inatoboa km 35 mpaka 45, hivyo ni kupiga tu hesabu zako(tumia minimum km 35 Kwa Lita).

Ukiwa safarini, Vaa earfone zako weka nyimbo au simulizi ufurahie safari na pia ikate usingizi. Pia, ukihisi uchovu simama pumzika, nawa maji usoni au km Kuna huduma ya kuoga is best option, sight mirror iwe unajiupdate muda wote, jitahd kubana upite kushoto Kwa mstari wa road kuepuka kujisahau alafu ukashtuliwa na honi ya GSM au HOOD. Kuwa makini muda wote Kwa kuchukua taadhari zote za kiusalama, kumbuka gari kubwa zikiwa main road huwa hawajali waendesha pikipiki wanawachukulia watu wabishi hivyo hawajali kama nawe unategemewa na familia.

Kumbuka:
Kuomba Dua muda wote, beba vitambulisho Incase ili iwe rahisi, pia toa updates Kwa mtu wako wa karibu ili kama utarest iwe rahisi kufuatilia, kama una familia andika wosia.

Nikutakie safari njema, enjoy the View mkuu.
Umeanza vizuri sema umeharibu hapo kwenye wosia,ni umakini tu njiani.
 
Mkuu sikukatishi taa ila walau ungekuwa na pikipiki yenye mwendo walau kama BMW 1200 series and the likes.

Hizi pikipiki ndogo ukishaanza kuitafuta 100 vibrations ni nyingi.

Kitu cha pili sijui una uzoefu gani wa kuendesha safari ndefu, ila kama hauna basi tafadhali pakia tu pikipiki kwenye basi au lorry.
Sasa mkuu atapataje uzoefu bila kuendesha safari ndefu?Au awe anaanza kwa safari za km 300 kwanza halafu ndipo atafute road trip ya km 1000?
 
Ndugu wanajamvi nategemea kwenda Shinyanga nikitokea Dar es salaam kwa Piki piki boxer cc125 mwenye uzoefu itakuwa vyema ukanisaidia.

Nataka kujua mafuta naweza kutumia kiasi gani. Je, nijiandae kwa changamoto gani barabarani pikipiki hii ninayotaka kuitumia ni mpya. na nina tegea kwenda na kurudi....

View attachment 2760635.mrejesho,
Nilibadili safari nikaenda Tanga, muda huu saa 11:30 nipo Mkata. Nilitoka dar es salaam saa 7:30 asubuhi nilikuwa naendesha speed 70 Hadi 80 kwakweli tunaogopa TU.

Ila Kwa boxa IPO vizuri sana barabarani imetulia japo ukizidi speed 90 inayumba nadhani ni kutokana na kuwa sikuwa nimebeba mzigo.

Usafiri wa piki piki ni hatari sana kwani Kuna baadhi ya madereva awazingatii sana Sheria za barabarani.

Nilinusurika kugongwa nikasukumiwa Kando ya barabara baada ya dereva kuovatake bila kujali kuwa nilikuwa mwendo Kasi nakuja Kwa mbele yake...nisingetoka nje ya barabara ninge gongana uso Kwa uso na gari iliyokuwa inaovertake.[emoji24][emoji24][emoji24]

Ila Kwa ufupi ukiacha uchovu kidogo barabara haipo busy. Hivyo haikuwa hatarishi sana. Mliokuwa mnaogopa kusafiria pikipiki ndugu zangu msiogope PIKI piki ni usafiri mzuri TU na WA haraka sana.
View attachment 2761644
Mchawi koti tu
 
...pikipiki hiyo sio ya masafa mkuu utaionea... Inaweza kuhimili lakini hyo ni ya root za town boss... Afu chuma inameremeta mkuu hyo angalia barabara za shinyanga nyekundu kama ugoro wa subiana
 
Mkuu bado hujaanza safari tu?? Usitishwe tembea br,zingatia tu walivyo shauri wadau,usisahau ibada na uodaye s hapa,ukifika manyoni nijuze nikupekuku na mguu wa mbuzi
 
Wakakata moto kivipi, kwan hizo za masafa wanafikaje?
Kuna wale madogo waliamua kwenda Karatu kwa pikipiki aina ya SanLG kutokea Morogoro, hata Dumila hawakuiona wakakata moto! Kuna mwalimu aliamua kusafiri kwa pikipiki kwenda kumzika mamake huko Simiyu akitokea Dodoma Msalato sec. Hata Manyoni hakuiona akakata moto! Tutofautishe pikipiki za masafa marefu wanazotumia Wazungu na hizi bodaboda! Kwa bahati unaweza kufika salama lakini iwe "at your own risk!"
 
Kufika unafika ila usikamie safari,nenda kwa vituo ukijihisi umechoka pumzika yani usiwe na haraka sana.
 
Back
Top Bottom