Hivi sasa kuna missiles za kisasa na radar za kisasa, halafu nilishaeleza hapa capability ya Russia kwenye EW.
Hio F-16 italinda nini wakati huu? ndio maana nimesema labda kwa kushambulia Syria, Iraq na Gaza zitafaa lakini sio kwa taifa kama Russia.
Hio F-16 ina maajabu gani itakayopelekea kudhibiti mifumo ya kiulinzi ya Russia ?
Zilikuwepo missiles zinazofuata joto zenye IR sensors, ndege vita zikaja na flares kuzichanganya missiles hizo na zilifanikiwa.
Wajanja wakaja na missiles zinazotumia radar, zina trace ndege inapoelekea kwa kutumia radar, hapo flares hazitofanya chochote, kuna Semi Active radar missiles ambazo zilitegemea kupiga target kwa kupata taarifa kutoka kwenye launcher. Hivyo missile inakutafuta hadi upatikane.
Zikaja AR missiles ambazo ni Active Radar missiles ambazo zinapata taarifa kutoka kwenye launcher na pia zina radar yake zenyewe, missile ina radar yake inajitegemea kuitafuta target.
Ndege vita zikaja na na vitu inaitwa chaffs ili kupambana na hizo missiles ambazo ni AR.
Lakini haikusaidia, radar zimeboreshwa zaidi na zaidi , zamani utaona hata kwenye movie ndege inaruka chini kukwepa radar, hio haipo tena kwa radar za kisasa ambazo ni hatari tupu, uruke chini , uruke juu bado utaonekana.
Ndio maana nakuambia vita na Russia sio vita na Afghanistan au Syria unapeleka ndege ukitegemea uta escape missiles kwa kuachia flares na chaffs.
Ndipo wataalamu wa mambo wanasema hadi sasa njia pekee ya kuzuia radar za adui kukuona ni kupitia electronic warfare, ndio maana unaona US anahangaika na hizo anasema ni multi role fighter kama F 35 ambazo wanasema zina stealth features, kuna F 22, E/A-18G Growler , B-2 n.k...
Ndio maana nilisema humu kwenye comment kule juu, hao Ukraine wasaidiwe hizo F-35 ambazo ni capable of EW...
Naweza kukuwekea hapa pdf ikielezea uwezo wa Russia kwenye electronic warfare unavyotisha, jamaa wapo mbali sana, ndio maana nasema hizo F-16 subiri tutapata habari hapa hapa.