NATO itaiponza Ukraine. Leo wametangaza kupeleka ndege vita huko Ukraine

NATO itaiponza Ukraine. Leo wametangaza kupeleka ndege vita huko Ukraine

Ukitaka kuelewa kinachpendelea duniani usiwe mshabiki! Hanyosheki mtu!
Haya fuatilia kwenye link hii usikie Zelensiky anasemaje!
Mkuu Ukraine ameanza kupokea silaha toka vita ianze na kazi inaonekana ndio maana wazungu wanaendelea kumwaga masila, na tokea vita inaanza Zelensky ni kawaida kuendelea kuhitaji silaha zaidi na zaidi kulingana na ukubwa wa adui, hamaanishi kwamba hizo ndege chache alizopewa hazitaleta tija.

Putini break ya kwanza alipovamia ukraine target ilikuwa ni Kiev lakini alirudishwa nyuma mpaka sasa anapiga kelele kwa nje nje tu
 
Russia wanavamia eneo , wanaweka SAM(Surface to Air Missile) zenye uwezo wa kulinda eneo walilovamia na kulichukua. Hivyo NATO itabidi warushe missiles au ndege kwenda kupiga air defenses za Russia, kitu ambacho ni kigumu.

Kingine uwezo wa Russia kwenye EW (Electronic warfare ) unatisha, NATO wanakiri juu ya uwezo wa Russia kwenye EW na wameshangazwa kwa kuchelewa kufahamu uwezo wa Russia kwenye EW, uwezo wa EW wa Russia ni hatari kwa vifaa vya NATO kuanzia drones zinazoruka kwenye highly altitudes hadi mifumo ya ulinzi kama airborne early warning and control (AEW&C)
Grumman_E-2C_Hawkeye_in_flight_DN-SD-04-13416.jpg

Hizo AEW&C ndizo zile radar huweka kwenye ndege na kuruka juu kwa ajili ya kukusanya taarifa kwa ajili ya kujilinda na kushambulia, AEW&C system moja inaweza kugundua ndege ya adui iliyopo umbali wa 400 km, na kuweza kukusanya taarifa ndani ya eneo lenye ukubwa wa 312,000 km2, Tuseme ndege moja tu yenye mfumo wa AEW&C inaweza kupata taarifa ya anga zima la nchi ya Uganda lenye 241,038 km2.

Hata hili suala la F-16 soni kama ni threat kwa Russia.
NATO inabidi waweze kutawala electromagnetic spectrum katika anga la Ukraine, hivyo unapozungumzia air superiority inapaswa uelewe pia kama Russia hawawezi air superiority je NATO wataweza air denial ? jibu ni NO.

Kingine Russia wanatumia drones na missiles kupiga air defenses na missile defenses za NATO, NATO inabidi wawe na silaha za kutosha zenye uwezo mkubwa na nyingi ili kuweza ku target launch positions za Russia, washambulie na kulipa kisasi, mfano long range ATACAMS au watumie JASSM ambazo cost yake moja ni zaidi ya 1 million usd. Hapa sioni kama NATO wataweza kuilinda Ukraine kwa gharama hizo dhidi ya Russia, gharama za ATACAMS na JASSM ni kubwa mno.
US_clears_sale_of_50_AGM-158B_B-2_JASSM-ER_air-to-ground_missiles_for_Japanese_Air_Force_1.jpg

jassm missile

Hii vita NATO hawakujipanga vyema kupambana na Russia.
 
Hii Vita imenifanya nisiamini Viongozi,Tangu nakua nimekuwa nikiamini Viongozi ni watu wenye fikra za juu sana.Lakini kwa hiki kinachoendelea,hata mtoto mdogo atashangaa.
Hakuna namna yoyote Ile Urusi atashindwa hii Vita.
Ni sawa na Rwanda au Burundi wapigane na Nchi kama Tanzania.
Ni kichekesho Cha kuhuzunisha.
 
Russia anazalishq silaha mwenyewe na chuma anachimba mwenyewe. Ameingiza vifaru vipya elfu hamsini na bado viwanda vina endelea kuzalisha
Ule msururu wa vifaru aliovamia nao ukraine wenye urefu wa 64km uliishia wapi ata akazalisha vyengine? vifaru kwa technologia ya sasa kwenye vita havina impact yoyot.

Wewe unaenda na vifaru wenzako wanaingia F-16 kuna kifaru kitabaki hapo? get your head mkuu, putin kaisha
 
F-16 sio kitu kwenye modern warfare kama sasa, F-16 ni issues za US military industrial complex kwa ajili ya kutengeneza faida.

Unaweza kuniambia kuna haja gani ya kutumia F-16 hali ya kuwa hivi sasa kuna drones na missile zinasafiri hadi zaidi ya 5000 km? na zinalenga kwa shabaha ya hali ya juu na zina gharama nafuu kuliko hio F-16?

Nchi ambayo ni wajanja kama Iran wame deal zaidi na high precision missiles trchnology na drones ambapo gharama ni nafuu na wanazalisha nyingi zaidi.

F-16 zitabaki kuwa nzuri kwa CAS(Close Air Support) missions , na hapo uwe unapambana na nchi kama Afghanistan, lakini kwa taifa lenye uwezo kama Russia hizo F-16 zinashambuliwa. Hata A-10 Thunderbolt US walizitumia kwenye missions za CAS huko middle east lakini A-10 huwezi ipeleka Ukraine.
 
Hizi ndege zimekuja kwa kuchelewa.....

Ukraine ingepata msaada wa kutosha toka awali hali ingekuwa njema upande wake.

T14 Armata
Fighter jets zinahitaji maintenance kubwa na familiality ya systems zake. Ukraine haikuwa na F16 kwanza, kabla ya kuipa hizo ndege ni mpaka yawekwe mazingira wezeshi. Ambayo yalichelewa ila bado wasingeziwahisha sana. NATO tangu mwaka juzi walitoa Soviet made jets, kina Poland walitoa hizo Mig-29 sababu Ukrainians wako familiar nazo. Hata vifaru vya Kisovieti walivipata mapema ila hivi vya NATO walichelewa.

Ndio maana kila pact inapenda kutumia slaha zake ili kuwepo na integration. Ni maamuzi magumu kwa mfano Poland kununua weapon systems za South Korea. Mpaka kuwepo na faida nyingi sana kama tech transfer na local assembly, otherwise hutoona mfano Belarus ina silaha muhimu iliyotengenezwa Ufaransa.
 
Mkuu Ukraine ameanza kupokea silaha toka vita ianze na kazi inaonekana ndio maana wazungu wanaendelea kumwaga masila, na tokea vita inaanza Zelensky ni kawaida kuendelea kuhitaji silaha zaidi na zaidi kulingana na ukubwa wa adui, hamaanishi kwamba hizo ndege chache alizopewa hazitaleta tija.

Putini break ya kwanza alipovamia ukraine target ilikuwa ni Kiev lakini alirudishwa nyuma mpaka sasa anapiga kelele kwa nje nje tu
Tangu apokee hizo silaha ni lini?
Nasikia zimeisaidia kurudisha maeneo yaliyonyakuliwa na Russia!
 
F-16 sio kitu kwenye modern warfare kama sasa, F-16 ni issues za US military industrial complex kwa ajili ya kutengeneza faida.

Unaweza kuniambia kuna haja gani ya kutumia F-16 hali ya kuwa hivi sasa kuna drones na missile zinasafiri hadi zaidi ya 5000 km? na zinalenga kwa shabaha ya hali ya juu na zina gharama nafuu kuliko hio F-16?
Drone gani inalinda airspace. Drone gani inafanya interception iwapo ndege ya adui inaingia anga lako. Yani ukienda vitani mwenzako ana fighters wewe una drone utapigwa uchakae, eti unaacha anga uchi kisa vidrone vyako.

Suicide drone inayotumika mara moja unailinganisha na F-16 yenye kuweza kuruka mara elfu.

Urusi si inazo Shaheed na copy zake, mbona bado inatumia Su-34 kurusha mabomu kama FAB-500 inaweka glide kits.
Mbona inatumia Tu-22 kurusha makombora mazito kina Kh- series. Utumie drones kurusha Kh-101 yenye tani 2.5, au bomu la FAB-3000 lenye tani tatu?
Nchi ambayo ni wajanja kama Iran wame deal zaidi na high precision missiles trchnology na drones ambapo gharama ni nafuu na wanazalisha nyingi zaidi.
Unaisema Iran ipi isiyotaka fighter jets, hiihii Iran inayohangaika kuunda 3rd generation fighter kwa kukopi F-5 Phantom za Marekani ilizonazo kwenye inventory tangu early 1970s?

Unaisema Iran hii inayopambana sana ipate kusaini deal la Su-35 na Russia.

Kama Iran ingekuwa haitaki fighters ingeanza na kuziondoa zote ilizonazo tena made in America. Ina F-4, F-5, F-14 Tomcats zinachakaa inachokonoa inaingia gharama nyingi. Marekani aliyemuuzia zake zimestaafu muda sana ila Iran bado inatumia hivyohivyo outdated.
F-16 zitabaki kuwa nzuri kwa CAS(Close Air Support) missions , na hapo uwe unapambana na nchi kama Afghanistan, lakini kwa taifa lenye uwezo kama Russia hizo F-16 zinashambuliwa. Hata A-10 Thunderbolt US walizitumia kwenye missions za CAS huko middle east lakini A-10 huwezi ipeleka Ukraine.
Ni lini umesikia ndege ya Urusi mainland ya Ukraine, tofauti na mipakani. Urusi hana ndege yeyote ya kuweka anga la Ukraine lets say kwenye mji wa Pavlograd kule Mashariki. Hivyo ni sawa unaitaka Urusi iache kuunda Mig-30, Mig-35, Su-30, Su-35 kisa haziwezi ingia waziwazi anga la Ukraine hivyo ni failure kwenye vita ya kisasa.

F-16 itashindwa mazingira yaleyale inayoshindwa Su-30. Yaani ikae Patriot hapo, ije Su-30 ipigwe alafu useme fighter jets ni hasara. Inategemea umezitumiaje silaha kila moja ina limitation yake na zinategemeana.
 
Siyo anapigana kistaarabu Bali huo uwezo hana Kama tulivyodanganywa, hata kutawala anga la Ukraine hawezi, Vita vya ardhini vimekuwa vigumu kwake, huko baharini meli amepeleka mbali baada ya kuzamishwa na Ukraine.
Msituone wote hatuna akili ya kung'amua Mambo wakati ukweli uko bayana.
Hiyo akili yako ukiitumia vizuri utagundua kwamba Russia anagonga kwenye mitambo ndio maana watu wamekufa wachache

Lakini Israel anawalenga raia hana tofauti na Hamas
 
Kwani Gaza kuna mauaji ya kikatili?
Si mnasema wazayuni wanakiona kila siku toka kwa mashabibi wa hamas?

Msalimie chura kiziwi
Naona huelewi unachokiandika au unajitowa ufahamu tu.

Hamas kwanini wanapigana na mazayuni?

Hayo ya kuuliwa hoivyo Wapalestina ndiyo yamehamasisha kuzaliwa Hamas, unafahamu maana ya Hamas?
 
Unafurhia uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi ndogo jirania ya Ukraine, siyo? Ni kati ya wanaodhani ni kutuniana na West wakati huo ni uvamizi haramu.t isingeisaidia Ukraine, kwa plan ya Putini sassa hivi Ukraine ingekuwa imefutwa kwenye ramani, na wee ungefurahi sana.

Yaania na wewe unaamini View attachment 3038808
Mimi sifurahi vita! Hii ni vita ya Russia na NATO,Zelensiky ni kibaraka wao na ndiye anayeiangamiza Ukraine.
 
Drone gani inalinda airspace. Drone gani inafanya interception iwapo ndege ya adui inaingia anga lako. Yani ukienda vitani mwenzako ana fighters wewe una drone utapigwa uchakae, eti unaacha anga uchi kisa vidrone vyako.

Suicide drone inayotumika mara moja unailinganisha na F-16 yenye kuweza kuruka mara elfu.

Urusi si inazo Shaheed na copy zake, mbona bado inatumia Su-34 kurusha mabomu kama FAB-500 inaweka glide kits.
Mbona inatumia Tu-22 kurusha makombora mazito kina Kh- series. Utumie drones kurusha Kh-101 yenye tani 2.5, au bomu la FAB-3000 lenye tani tatu?
Hivi sasa kuna missiles za kisasa na radar za kisasa, halafu nilishaeleza hapa capability ya Russia kwenye EW.

Hio F-16 italinda nini wakati huu? ndio maana nimesema labda kwa kushambulia Syria, Iraq na Gaza zitafaa lakini sio kwa taifa kama Russia.

Hio F-16 ina maajabu gani itakayopelekea kudhibiti mifumo ya kiulinzi ya Russia ?
Zilikuwepo missiles zinazofuata joto zenye IR sensors, ndege vita zikaja na flares kuzichanganya missiles hizo na zilifanikiwa.

Wajanja wakaja na missiles zinazotumia radar, zina trace ndege inapoelekea kwa kutumia radar, hapo flares hazitofanya chochote, kuna Semi Active radar missiles ambazo zilitegemea kupiga target kwa kupata taarifa kutoka kwenye launcher. Hivyo missile inakutafuta hadi upatikane.

Zikaja AR missiles ambazo ni Active Radar missiles ambazo zinapata taarifa kutoka kwenye launcher na pia zina radar yake zenyewe, missile ina radar yake inajitegemea kuitafuta target.

Ndege vita zikaja na na vitu inaitwa chaffs ili kupambana na hizo missiles ambazo ni AR.
Lakini haikusaidia, radar zimeboreshwa zaidi na zaidi , zamani utaona hata kwenye movie ndege inaruka chini kukwepa radar, hio haipo tena kwa radar za kisasa ambazo ni hatari tupu, uruke chini , uruke juu bado utaonekana.

Ndio maana nakuambia vita na Russia sio vita na Afghanistan au Syria unapeleka ndege ukitegemea uta escape missiles kwa kuachia flares na chaffs.

Ndipo wataalamu wa mambo wanasema hadi sasa njia pekee ya kuzuia radar za adui kukuona ni kupitia electronic warfare, ndio maana unaona US anahangaika na hizo anasema ni multi role fighter kama F 35 ambazo wanasema zina stealth features, kuna F 22, E/A-18G Growler , B-2 n.k...

Ndio maana nilisema humu kwenye comment kule juu, hao Ukraine wasaidiwe hizo F-35 ambazo ni capable of EW...

Naweza kukuwekea hapa pdf ikielezea uwezo wa Russia kwenye electronic warfare unavyotisha, jamaa wapo mbali sana, ndio maana nasema hizo F-16 subiri tutapata habari hapa hapa.
 
Ule msururu wa vifaru aliovamia nao ukraine wenye urefu wa 64km uliishia wapi ata akazalisha vyengine? vifaru kwa technologia ya sasa kwenye vita havina impact yoyot.

Wewe unaenda na vifaru wenzako wanaingia F-16 kuna kifaru kitabaki hapo? get your head mkuu, putin kaisha
Sasa wewe unadhani Russia hana ndege za kisasa fighter jet? Unaijua SU - 57?
Screenshot_20240711_173950_Google.jpg
 
Ni kweli ila wenzetu wametuzidi jambo moja, ambalo ni kujiandaa na kujipanga katika nyakati za shida. Mfano, ukitazama reserve ya gold kwa bara la ulaya na marekani inaweza kuwapeleka pengine hata miaka 10 au 20 bila kuihitaji, sasa sisi reserve yetu ya mafuta unakuta ni 2month, hatuna source ya internet wakitaka wanazima hata kesho.
Dhahabu ni mfano tu nimekupa lakini bidhaa tunazotegemeana ni nyingi sana mkuu.
 
Ni kweli ila wenzetu wametuzidi jambo moja, ambalo ni kujiandaa na kujipanga katika nyakati za shida. Mfano, ukitazama reserve ya gold kwa bara la ulaya na marekani inaweza kuwapeleka pengine hata miaka 10 au 20 bila kuihitaji, sasa sisi reserve yetu ya mafuta unakuta ni 2month, hatuna source ya internet wakitaka wanazima hata kesho.
Sio sisi ukisema sisi unatukosea sisi wengine sema viongozi
Unakuta viongozi wana save za chakula hata za miaka 100 wakati raia wao wasipotoka tu wanakufa njaa kwa kukosa chakula
 
Back
Top Bottom