NATO itaiponza Ukraine. Leo wametangaza kupeleka ndege vita huko Ukraine

Kaka unategemea urusi atabaki sawa na hiyo Vita?non sence hivi mnajua maana ya uchumi au mnakariri?
Nawe unategemea wasiokua Russia watabakia sawa
Acha kusema watu wanakariri bila kuleta fact
Hii mbungi kama India na Uchina wataendelea kuwa upande wa Russia hayo mnayoyawazia kuikumba Rusdia kwakweli muyasahau
 
Hizi zako ngonjera na kutapata tapa kusiko maana
PUT IN day one anatangaza kuingia UKRAINE aliyatangaza majimbo manne kujiunga na RUSSIA vipi ulilisikia jimbo la KIEV😀
Mnadhani simu janja mnazopekeenu enyi pro manato acheni kupiga fix watu
 
Wakati wa vita za Ghuba au Yugoslavia Kuna ndege za akina NATO zilikua zinatokea kwenye viwanja vya ndege vya nchi zao na baadhi zikitokea kwenye nchi marafiki,mfano Kuna baadhi ya ndege za USA zilikua zikitokea UK kwenda kupiga Iraq ama Serbia.
Sasa kama NATO kweli ni wababe wanaogopa Nini kuziweka katika nchi Wanachama wa NATO badala yake wanataka kuziweka Ukraine wakati wanajua fika hawawezi kuzificha dhidi ya macho makali ya Urusi?
Ilhali wanajua fika Putin taziona na atazichoma zote?
Nawashauri waziwekeke kwenye nchi za NATO, ziwe zinatokea Poland Au Romania,🤣🤣🤣🤣
 
Heheheee uzuri Russia alishatangaza hili mapema
Atapiga popote ambapo ndege zitakua zinaruka kwenda kushambulia majeshi yake
Kama kuna NATO anawashwa washwa aweke ndege aone
 
Sio sisi ukisema sisi unatukosea sisi wengine sema viongozi
Unakuta viongozi wana save za chakula hata za miaka 100 wakati raia wao wasipotoka tu wanakufa njaa kwa kukosa chakula
Kuna ukweli katika hili.
 
Hizo F-16 si mpya ni za zamani zilotumika hadi na vita ya Libya. Walikuwa wakizifanyia matengenezo. NATO na Marekani hawawezi kupeleka ndege mpya zikaunguzwe zote Ukraine.

Ni katika hatua za kumaliza stock walokuwa nazo kwenye mabohari kupisha stock ya ndege mpya.
 
Watanzania hatuna utaratibu wa kuweka data usiamini sana hizo taarifa mali inayouzws nje ya nchi hii ni nyingi sana.
Kama data haziaminiki ni ngumu kuwa na hakika kuwa wanatutegemea kwa kiwango gani huenda ukawa sawa na huenda usiwe sawa maana nijuavyo sisi hadi ngano tunaimport.
 
Hizi zako ngonjera na kutapata tapa kusiko maana
PUT IN day one anatangaza kuingia UKRAINE aliyatangaza majimbo manne kujiunga na RUSSIA vipi ulilisikia jimbo la KIEV😀
Mnadhani simu janja mnazopekeenu enyi pro manato acheni kupiga fix watu
Sasa hayo majimbo manne aliyotangaza kujiunga na RUSSIA mbona juzi ameiomba ukraine hadi wayaachie asimamishe vita?

wewe hujui lolote, hayo majimbo aliyotangaza tu kwa mdomo lakini yapo ndani ya himaya ya ukraine base kubwa sana, russia katika hayo maeneo wana hold maeneo machache sana ambapo vita inaendelea kuhakikisha mvamizi anatema kila kitu. Fuatilia habari usiwe mvivu sasa ukraine wanapambana kurejesha hadi Cremea, F-16 zipo njiani, putin sasa imebidi akajiunge na north korea taaban nafsi yake mwaka wa 3 sasa hajatoboa.

Kama lengo lake halikuwa Kiev mbona alipovamia magari ya kivita ya russia yakiranda maeneo kote Kyiv uliza sasa kwani walitoka na kuitema Kyiv
 
Ukraine ina Mig-29, Su-25, Mig-27 na Su-24 kwenye inventory inazitumia sembuse ikatae F-16.
Ukraine imepewa Mig-29 kutoka Poland imezipokea na inazitumia. Ndio ije ikatae F-16 kwamba hazitofanya kazi. F-16 zina rekodi nzuri kuliko ndege zote zilizopo Ukraine. Kusema F-16 haitafanya kitu ni sawa na kusema ndege zote za Ukraine hazifanyi kitu na hazitumiki.

Si rahisi kubeba hizo EW systems na AD kuzipeleka frontline. Kuna cases za S-400, S-300 kupigwa na HIMARS na HARM missiles pale Crimea na maeneo mengine.
Urusi hana control ya airspace ya Ukraine hivyo hawezi weka silaha nzito na ngumu kuhamishika deep within Ukrainian territory. Hizo mifumo ya EW najua Russia yuko vizuri ila hazifungi karibukaribu anafunga mbali.

Ukizisogeza karibu EW systems zinapigwa sababu ili zifanye kazi inabidi zirushe mionzi ambayo inaonekana kwa electronic reconn drones au ndege za NATO. Na radiation ya EW inabidi iwe kubwa kuzidi uwezo countermeasure hivyo inaonekana kwa nguvu. Zimeletwa Krasukha, Leer-2, Zhitel, Bylina na all the best of the best Russian EW assets ila zikienda frontline zinapigwa. Sanasana frontline kuna mifumo midogo ya kufungwa kwenye gari moja ambayo ni kusumbua drones ndogo.

F-16 zitafanya kazi na zitatoa matokeo, na nyingine zitadunguliwa. Na hizo F-35 unazotaka nazo zingekuja kuna ambazo zingedunguliwa. Kama Russia imepoteza A-50 yenye electronic warfare, radar, wataalamu wabobevu zaidi ya 10 ndani na kila kitu ikadondoshwa na Ukraine zaidi ya 200km kutoka frontline sembuse jet yenye rubani mmoja/wawili na vifaa basic vya EW.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…