soine
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,113
- 2,329
Yaani Putin kuwapiga mkwara NATO nao wakaufyta kumefanya USA na allies wake wote kudharaulika.Marekani na nato NATO mwisho wao umefika.....hamna cha nato kutawala tena.....kitu pekee kinachowabeba sasa ni propaganda walizotengeneza kwa muda mrefu, nguvu ya hizo propaganda zikiisha na wao ndo kwaheri ..........their matrix is falling rapidly.......
Hata Zelensky anamesema wazi NATO hamna kitu, we have to fight for ourselves...wanaishia kutoa silaha tu ila kuingia vitani wanaogopa Putin atafanya nini. Hili huenda likawa kichocheo cha kuwaamsha maadui wa western allies kuanza upya mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa madhila yaliyoletwa na sera na vita toka kwa nchi za magharibi. Hivi majuzi tumeona ni nini Iran imefanya huko Iraq....kwa mwendo huu ndio Russia anaenda kupata washirika ambao wana lengo moja dhidi ya Marekani na nchi za magharibi.
Ikiwa hii vita itaingiza NATO kupigana, basi huenda mgogoro huko mashariki ya kati ukaendelea kuibuka. Ingawa hili kiutabiri haliko sawa.