NATO ndio dola ya mwisho, hakuna nyingine itakayoinuka

Yaani Putin kuwapiga mkwara NATO nao wakaufyta kumefanya USA na allies wake wote kudharaulika.

Hata Zelensky anamesema wazi NATO hamna kitu, we have to fight for ourselves...wanaishia kutoa silaha tu ila kuingia vitani wanaogopa Putin atafanya nini. Hili huenda likawa kichocheo cha kuwaamsha maadui wa western allies kuanza upya mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa madhila yaliyoletwa na sera na vita toka kwa nchi za magharibi. Hivi majuzi tumeona ni nini Iran imefanya huko Iraq....kwa mwendo huu ndio Russia anaenda kupata washirika ambao wana lengo moja dhidi ya Marekani na nchi za magharibi.

Ikiwa hii vita itaingiza NATO kupigana, basi huenda mgogoro huko mashariki ya kati ukaendelea kuibuka. Ingawa hili kiutabiri haliko sawa.
 
Unaweza kutumia Biblia ku support chochote....

Sina hakika na ulichosupport lakini.
Kwa wasoma wazur wa maandiko na historia. Hapo anaposema kuwa Israel itashambuliwa, na ktk ule unabii Yesu alisema watu wajifiche milimani n.k sasa ktk historia huu unabii ulishatimia miaka mingi tu.

Ni kweli Yerusalemu ikaja ikatekwa na ikazingirwa pande zote. Kwahiyo nabii nyingi tayar zilishatimia kitambo.

Nakubaliana na wewe kuwa waweza kutumia Biblia kusupport chochote kile.
 
Ndugu yangu una pointi kiupana ila umechanganya habari kidogo. Ndio marekani na ulaya watahusika na unachoongelea kibiblia lakini sio kama unavowazia na kuelewa.

Hapo chini ni picha ya makao makuu ya EU (kushoto) na mnara wa babeli (kulia). Wanatamba wazi wameiga mjengo... kwa nini? Wameiga mjengo tu ama itikadi za Babylonia? ... cha kujiuliza kwa wale wanaoona ndugu yangu anachoongelea hakieleweki.

 
Roma haikuanguka kama unavyo sema, Yenyewe ilijibadili kutoka kutawa kijeshi hadi kutawala kidini. Ambayo leo kupitia Vatican inatawala mataifa yote, USA ni Mkono wake wenye nguvu ulipo.

Mnachanganya vitu wazee ukisikia neno Rumi nahis wengi sana hapa wanazani ni Roma Italia ndio ilikuwa dola kuu
 
Kwa mujibu wa historia, kuna mtu akiyewahi kufikiri dola ya Rumi ingeanguka?
Hiyo dola haijaanguka , ndio mnyama wa NNE na anatawala mpaka sasa.Kasome vizuri biblia

Wanyama ni hawa:

1. Babylon
2. Wamed na waajemi
3. Wayunani
4. Warumi

Now tupo mnyama wa nne , anakaribia mwisho kisha watakatifu wa Mungu watakuja kuuchukua ufalme
 
Utabiri wa kujatibu kutafsiri hayo maandiko kila aliyejaribu uwa anaangukia pua.
Dunia badi ipo sana ndo kwanza tunatoka zama za Pisces kuelekea Aquarius.
Yesu mwenyewe alitabiri kuhusu Aquarius:
Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akiwa amebeba mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye.
 
Sababu ya NATO kukubali wanachama dhaifu kiuchumi ni kuongeza eneo la utawala wao. Michango ya nchi tajiri inatosha kuendesha jumuia.
 
All in all Palestina itakua free siku moja.
 
Kama NATO ndio dola ya mwisho ,atapigana na Nani !!?, dola ambayo itakuwa na nguvu sio NATO ,Kuna dola inakuja muda si mrefu na ss ndo mwanzo unaanza ,waasisi watakuwa ni Russia na China .hiyo dola mpya ndo itazipiga na na NATO(USA).
Na hii Vita itakuwa Niya nuclear na mabomu mazito mazito. USA itadondoka pamoja na NATO yako!!
 
Hakuna kitu kama icho bwashee
 
Nimekuelewa bwashee
 

Umeanza vizuri umemaliza kishabiki,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…