Kutokea kwa vita ni ngumu ila Mrusi anachofanya ni kutengeneza mazingira ya kuwaleta mezani kwa ajili ya mazungumzo na Muafaka, ila wakishupaza shingo kuna baadhi ya majimbo nchini Ukraine yanakwenda na maji kama vile Cremia. Ngoja nijaribu kuchambua kwa namna hii kidogo.
Ngoja nirudi kwenye Mgogoro wa makombora wa Cuba, 1962. Viongozi wawili huru kabisa, Nikita Khrushchev na Fidel Castro waliamua kwamba lingekuwa wazo zuri kwa Urusi kupeleka Makombora kwenye aridhi ya Cuba.
Je, walikuwa na haki ya kufanya uamuzi huo?
Kwa kuwa ni nchi mbili huru walikua na uhuru wa kufanya maamuzi hayo.
Hivyo wakafanya makubaliano hayo ya kupeleka makombora au kufnaay utaratibu wa kuyaunganisha pale Cuba na USA wakagundua hili, na Kennedy akawaambia Warusi, wageuza meli zao au watazizamisha, na ikiwa itasababisha Vita ya tatu ya dunia na iwe ivyo tu. Warusi wanageuza meli zao lakini kulikuwa na maelewano. Haikuwekwa hadharani nchini USA wakati huo, Kennedy alikubali kutoa makombora ya Maekani nchini Uturuki kwa kubadilishana, kwa sababu Warusi walisema, tazama, una makombora nchini Uturuki karibu kabisa na mpaka wetu. We unasema makombora yetu ni tishio kwako kuwepo nchini Cuba, lakini pia makombora yako ni tishio kwetu kuwepo nchini Uturuki. Toa makombora yako nchini Uturuki na sisi hatutapeleka makombor ayetu nchini Cuba.
Hayo yalikuwa maelewano kati ya hawa watu wawili.
Kennedy akaomba kwamba hili lisitangazwe hadharani kwa sababu lingeonekana kama upotevu wa imani na blah, blah, blah na halikuwekwa wazi na mpaka baadaye sana.
Hayo yalikuwa maelewano kati ya hawa watu wawili.
Na hii ikasaidia kuzuia Vita ya tatu ya dunia.
Kwa hivyo sasa hivi viongozi wa Urusi wanaona NATO kama tishio kwao.
Hivi ndivyo inavyoonekana machoni kwa viongozi wote wa Urusi, na hii sio siasa. Wanajiuliza, kwa nini unaendelea kuileta NATO karibu na mpaka yetu? wanajiuliza.
Uko Latvia, umepakana na sisi, uko Estonia umepakana na sisi. Sasa Ukraine inaelekea magharibi, ni swala gumu, Maekani ilicheza mchezo fulani wakati wa uchaguzi wa Ukraine mwaka, hili sio la maana sana. Kikubwa wanachowaza Urusi ni kwamba Ukraine inaelekea magharibi. Wanaendelea kuwaza ikiwa hatimaye itaingia katika eneo la magharibi, basi kwamba Ukraine itajiunga na Umoja wa Ulaya na itakuwa mwanachama wa NATO. Sasa, Ukraine ina mpaka na Urusi. Si hivyo tu, lakini Cremia ambayo ilikuwa na asili ya Kirusi na wanaongea Kirusi, si hivyo tu kuwa na asilia ya Kirusi na kuongea Kirusi kuna kubwa zaidi katika Cremia. Kuna kambi ya Sebastopol ambayo hutumiwa na jeshi la wanamaji wa Urusi katika Black Sea. Kwa hivyo ikiwa Cremia itabaki Ukraine, na ikiwa Ukraine itakuwa sehemu ya NATO, basi kambi hii haitakuwepo, zaidi kutakuwepo na kambi ya wanamaji ya NATO ikiongozwa na Marekani katika eneo hili, na NATO itakuwa kwenye mpaka wa kusini-magharibi mwa Urusi, na Warusi wanaona hii kama hatari kwao, na wanasema hawataruhusu ilo kwamwe.
Je, hili linaingiliana na sheria za kimataifa?
Hapana, haliingiliani. unapozungumza kuhusu sheria za kimataifa kama ilivyo katika Mgogoro wa makombora wa Cuba. Unasema, Hapana hatujalijinsi unavyojsikia. Hatutaruhusu hili kwamwe hatakama unaumia, utajua mwenyewe ila sisi hatuajali kwa ajili ya masilahi yetu. Ni maoni yangu kwamba tangu awali kulikuwa na aina fulani ya makubaliano ya mazungumzo ya kimataifa kwamba Ukraine haitakuwa mwanachama wa NATO na hakutakuwa na tatizo la aina yeyote nchini Ukraine. Lakini makubaliano hayo yanaonekana kuvunjwa, Ukitaka kujua hili tafuta hotuba ya Putin Inayoitwa Munich Speech.
Marekani ina mpaka mkubwa sana na Mexico.
Sasa fikiria kuwa kutokee mapinduzi huko Mexico. Hii si ngumu kufikiria, na fikiria kuwa serikali inayoingia madarakani sio shabiki ama rafiki mkubwa wa Marekani, lakini kwa kuwa inaogopa kutokana na ukubwa wa Marekani, inawaomba Warusi kupeleka jeshi kuwekwa na kuwekwa mpakani mwa Marekani na Mexico.
Unadhani Marekani italikubali hili?
Je kwanini Warusi walikubali hili la Ukraine kuwa wanachama wa NATO?
Je, lazima kuwe na maelewano?
Kwa maoni yangu, Ndiyo lazima kuwe na maelewano na maelewano ni dhamani kwa Ukraine kutokuwa mwanachama wa NATO, na maelewano ni kwamba Warusi kutoka nje ya Ukraine na kuiacha Ukraine ijiendeshe. Tunatoka lakini kuna dhamana.
There must be a compromise, and Russian’s have created it so it is up to western to negotiate right now.
View attachment 2094821
View attachment 2094822