NATO wanatishia, Urusi hatishii atavamia kweli na inaweza kutokea Vita kweli

NATO wanatishia, Urusi hatishii atavamia kweli na inaweza kutokea Vita kweli

Unajua historia vizuri wewe,kati ya Marekani na Urusi nani alisalimu amri kwa Watalebani kabla lengo lilimpeleka Afghanistan halijatimia?
Najua wewe unazungumzia miaka ya nyuma kwenye kuanguka kwa usoviety. Lakini Urusi hii ya Leo sio ya kipindi kile,cheki Putin alivyomzuia Marekani kumpindua Assad huko Syria,akamzuia kumpindua rais wa venezuela na akatwaa Jimbo la Crimea huku Marekani akijitahidi kuzuia lakini wapi.
 
Mkuu kwani hujawahi sikia tuhuma za Russia kuingilia uchaguzi wa USA kumsupport TRUMP .......na ukiconect dot ni kwamba trump alianza kuivuruga USA sema tu CIA waliona mbali wakampiga chin second term MAMBO YANAYOONESHA TRUMP KUWA KIVURUGE

1. Kijitoa kwny mikataba ya kibiashara na nchi za pacific and Latin america

2 Kipind cha TRUMP ndipo China ilikua zaid kiuchumi zaid ya marais wengne

2: alitishia kuivunja NATO kitu ambacho hakijawah hata kuwa ndoto ya rais hata mmoja wa USA.....Pia kumbuka NATO ndo adui mkubwa wa RUSSIA

3: Alijitoa kuwa sponsor wa WHO kitu ambacho USA hatak coz anataka dunia imtegemee yeye

4:alitaka kuleta vita na IRAN kitu ambacho ingekua hatar pale middle east baada ya kumuua kasim soleman PIA kwa Korea kaskazin

5:Kwenye reign yake hakukuwa na uhusiano MBOVU na RUSSIA kama ilivyosasa kwa BIDEN

That's y up to now CIA wanaamin TRUMP alikua ni mtu aliye supportiwa na Putin ........nadhan utakua umepata concept kidogo mkuu
Bado unakosea kumtaja Putin bora ungesema Rusia; sijui kwanini unapenda mtu tofauti na taasiai.
 
Likija swala la vita isee ..... Russia ni hatari ........lile ni jesh la mtu mmoja
Sawa lakini kumbuka NATO ni umoja wa nchi zaidi ya tano Tena zenye nguvu kijeshi na kiuchumi sidhan Kama Russia anauwezo peke ake kupambana na NATO yte watamtia vidole
 
Sawa lakini kumbuka NATO ni umoja wa nchi zaidi ya tano Tena zenye nguvu kijeshi na kiuchumi sidhan Kama Russia anauwezo peke ake kupambana na NATO yte watamtia vidole
Russia hata mkimchangia ni kazi bure aisee, awa jamaa kiukweli wanajiweza sana kwenye mambo ya kivita na pia ni watu majasiri na wenye mapenzi ya dhati na taifa lao.

Kwenye ww2 kulikuwa na mapigano ya kugombea jimbo la stalingrad.Mrusi akiwa peke yake huku upande wa pili yupo Mjerumani,Mtaliano, hungary na Romania.ilipigwa vita ya kufa mtu na mwisho wa siku Mrusi akaondoka na ushindi.
 
Sawa lakini kumbuka NATO ni umoja wa nchi zaidi ya tano Tena zenye nguvu kijeshi na kiuchumi sidhan Kama Russia anauwezo peke ake kupambana na NATO yte watamtia vidole
Of course hawez kuziweza nchi zote ila dunia itaaribiwa ..,..KUMBUKA RUSSIA ndo anaongoza kwa kuwa na SILAHA ZA NUCLEAR dunian
 
Mgogoro Kati ya Ukraine upo kweli na Vita kubwa sana yaweza Kutokea baina ya Urusi na Ukraine wakisaidiwa na NATO.

Chokochoko hapo ni Marekani tu ndio ambae anampa kiburi na kumdanganya Ukraine.

Nia ovu ya Marekani Ni kuwa na wanachama wengi wa NATO walio karibu na Urusi na hasa wale walikua wasoviet walionitenga. Lengo kuu Ni kumzunguka Urusi.

NATO wanatishia kumuonya Urusi asijaribu kuingia/kuvamia Ukraine. Wanaonya kuwa Urusi akiingiza majeshi Ukraine atakiona.
Hapa wanatishia tu.hakuna watakachokifanya Kama Urusi akiamua kuingiza,na hajaamua. Zaidi watakachokifanya Ni kujaribu kumpa silaha Ukraine,na ambazo zinaweza kuishia mikononi mwa Urusi.

Kwa Nini nasema NATO wanatishia tuu,Ni kwa sababu Ukraine sio mwanachama wa NATO,na NATO akiingiza jeshi lake hata kwa kurusha risasi moja tu kuelekea Urusi basi hiyo itakua Vita kamili,amabapo Urusi itatoa jibu kamili kabisa kwa NATO,au kwa lugha nyingine Risasi hiyo itajibiwa kikamilifu na Urusi.

Sasa hapo kitakachochotokea Ni Vita kamaili. Na Vita Kati ya Urusi na NATO itakua sio viita ya Risasi na Bunduki,Wala ndege,Bali Vita vya Makombora. Wote tunajua Hawa mahasimu wawili yaani Urusi na NATO uwezo wao kwenye Makombora.

Je Ni Nani Yuko tayari kwa upande wa NATO kukubali Makombora mapya na ya zamani ya Urusi yatue kwenye nchi zao kwa ajili ya Ukraine ambae hata sio mwanachama wa NATO?

Tena kwa mgogoro amabo hata yeye Ukraine Ana ukorofi wake?

Urusi hatishii,
atavamia kweli na hakuna wa kumfanya kitu.

Katika mgogoro wa Ukraine na Urusi Ni Ukraine na Urusi kweli ndio Zina maslahi sio NATO,NATO lengo la Ni kujitanua tu.

Ukraine yeye anataka kujiunga na Magharibi kweli lakini ndani yake Kuna majimbo yanataka kuwa upande wa Msahariki( Urusi).
Haya majimbo yakijitenga Ukraine inabaki Nusu,hivyo haiko tayari kwa Hilo.

Urusi in Maslahi makubwa kuliko NATO na hata Ukraine,Urusi bado inaipenda Ukraine,lakini Ukraine haiipendi Urusi. Urusi inaogopa Ukraine ikijiunga na NATO kwa sababu NATO itakua kubwa Sana na itakua mlangoni pa Urusi.

Ukraine inawapiga waasi amabao Ni Warusi wa asili. Ukraine ikijiunga na NATO Crimea inaweza kuchukuliwa Tena na Ukraine kwa msaada wa NATO. Hizo Ni sababu chache tu za kwangu kuonesha jinsi Urusi ilivyo na maslahi makubwa na Ukraine.

Kwa maslahi hayo ndio maana nasema Urusi hatishii atavamia kweli na hajali matokeo yoyote Yale tofauti na nchi Kama Ufaransa Ujerumani Italy na wanachama wengine wa NATO labda kidogo Marekani atajitutumua kuonesha Yuko pamoja na Ukraine,lakini ki ukweli wale NATO hawana maslahi makubwa kwao zaidi ya kutanua huo umoja ambao Marekani ndio anafaidika zaidi.

Kwa Ni I Naamini Kuwa Urusi hatishii na atavamia kweli.

Urusi aliwahi kuivamia Georgia kwa ujinga Kama huu wa Georgia kuwapiga waasi wanaotaka kujitenga wa Southern Ossetia na Abkhazia. Urusi alikuja juu na kushusha kipigo kwa Georgia na NATO wakibaki kupiga kelele bila kufanya chochote ingawa walikua wakimpa kiburi Georgia.

Urusi ilikwenda mbali zaidi kwa kumpinga Georgia Hadi ndani na Urusi kuyapa Uhuru majimbo hayo mawili ya Southern Ossetia na Abkhazia kibabe tu. NATO walipiga kelele na UN walipiga kelele Urusi walitia pamba masikioni.

Baada ya mgogoro wa Ukraine kuanza kipindi kile kupelekea Rais aliekuwepo Ukraine wakati ule kupinduliwa na kukimbilia Urusi,baada ya Majimbo ya Luhansk na Donesk kutaka kujitenga Urusi iliingia Ukraine kiana na kujitwalia Jimbo la Crimea iliyokua sehemu ya Ukraine NATO na UN waliishia kupiga kelele huku wakiwa Kama watazamaji wa nyumba inayoungua bila msaada.Urusi hapa hakutishia alifanya kweli.

Mgogoro wa Waasi wa Syria waliokua wakiungwa mkono na Marekani Uingereza,Ufaranza,Uturuki,baadhi ya nchi za Ulaya, Sehemu kubwa ya Waarabu na Israel ili kumtoa Assad.

Urusi peke yake ilipinga Assad kuondolewa na kwa jeuri kabisa katikati ya hao wote ikapeleka majeshi yake na kupigana na yoyote aliekua anataka kumtoa Assad na hatimae leo Assad yupo madarakani zaidi ya miaka nane.

Urusi Tena ikapeleka vifaa vya kijeshi nchini Venezuela kumuunga mkono Raisi Nikolas Maduro ambae Marekani Uingereza na nchi nyingi za Amerika ya KUSINI kufanya kila hila kutaka Maduro aondoke madarakani kisiasa ama kijeshi.Urusi alipeleka vifaa vya kijeshi na wataalamu wa kijeshi nchini Venezuela kumlinda Maduro na Hadi leo yupo miaka kadhaa Sasa. Hii ya Venezuela sio maslahi muhimu Sana kwa Urusi ila kuweka heshima tu.

Kwa Urusi kule Ukraine Ana maslahi makubwa ya muhimu na ya kweli kabisa. Hivyo nchi yoyote duniani huwa inaingia vitani kupigania maslahi yake.

Urusi hapa iko tayari kupigana Vita kabisa na haijali matokeo ya Vita Bali maslahi kwanza. Lakini NATO hasa wa upande wa Ulaya Hawa hata Vita ikianza wao hawoni umuhimu wa Vita. Kwa hiyo NATO wanatishia tu lakini Urusi Hatishii Bali ataingia kweli Kama akiona ujinga unaendelea. Nimeonesha mifano hapo juu ya Georgia,Crimea, na Syria. Urusi hakutishia Bali aliingiza majeshi kweli na Hali halisi tumeiona. Kama mnadhani utani subirini mtaona Kama Urusi ataogopa kuivamia Uraine.
bila shaka muandishi ni dr shika
 
Russia hata mkimchangia ni kazi bure aisee, awa jamaa kiukweli wanajiweza sana kwenye mambo ya kivita na pia ni watu majasiri na wenye mapenzi ya dhati na taifa lao.

Kwenye ww2 kulikuwa na mapigano ya kugombea jimbo la stalingrad.Mrusi akiwa peke yake huku upande wa pili yupo Mjerumani,Mtaliano, hungary na Romania.ilipigwa vita ya kufa mtu na mwisho wa siku Mrusi akaondoka na ushindi.

Kila nchi inajiweza kwa kiasi chake. Russia sio invincible kama wengi mnavyojaribu kuweka.
Ukipata muda kasome yaliyomkuta Afghanistan na Chechnya....bila kusahau kwenye WW2 kama sio ile baridi kumsimamisha Adolf historia ingeandikwa tofauti.
 
Hayo maneno ya kwenye vijiwe vya bangi.kwani WARUSI wao ni maroboti mpaka baridi isiwaumize.katika kosa kubwa Hitler alilofanya katika maisha yake ni pale alipojaribu kuivamia URUSI, naimani kama asingeivamia URUSI basi historia ingeandikwa vingine kabisa.na siyo Hitler peke yake Napoleon wa Ufaransa alipiga mataifa mengi makubwa ila alipoingia kwenye ardhi ya WARUSI ukawa ndo mwisho wake.

Kuhisu Afghanistan ni sehemu ngumu san ya kupambana na adui kutongana na mazingira yake ya milima, Marekani na Nato wana zaidi ya miaka 10 Afghanistan na bado Wataliban wana tawala maeneo mengi ya nchi.Na sasa ivi washaanza kuondoa vikosi vyao ndani ya ardhi ya Afghanistan.

Kuhusu Chechnya mbona tumeshasahau kuwa kulikuwa na waasi wa Chechnya.WARUSI walisafisha waasi wote mpaka leo ni moja kati ya jimbo linalovutia ndani ya Nchi ya URUSI.

WARUSI sio watu wa mchezo ndugu hata vifaa vyao ni moja kati ya vifaa bora kwenye uwanja wa vita.AK 47 hata ukichimbia chini miaka 100, siki ukitoa ni mwendo wa kufuta vumbi tu unaingia nayo uwanja wa vita.kafanye ivi kwenye bunduki ya KIMAREKANI uwone nini kitakutokea
 
Nadhan ameelewa mkuu.......sema Mara nying western media haziwazungumzii kiuwezo
 
Hoja yangu imejikita kwa Putin kutengeneza mifumo imara kama mpinzani USA na iwe na uwezo wa kupandikiza viongozi huko USA na kwingineko siyo yeye kua ndo kila kitu...ikitokea akifa leo ndo tena RUSIA irudi ilikotoka? nisome vizuri tena.
Tatizo watu mnaongelea Urusi utafikiri ni nchi yenye miaka 60 ya kujitawala...Hawa watu wapo na system ya utawala maelfu ya miaka nyuma huko, kabla hawajawa empire, russia empire, soviet union, russia republic, russia federation....
Hata Putin akifa leo..maisha yataendelea tu kwa hawa jamaa...either kuendelea na mfumo wa sasa au kuanzisha mwingine, wanaweza fanya chochote hawa...
 
Apigane na China, Urusi au Korea kaskazini atachukua nn? Ni bonge la hasara
Hivi unajua China na Russia wana rasilimali kiasi gani!? Kwa taarifa rare earth materials zaidi ya 80% yanapatikana China (usiniulize hayo materials yana umuhimu gani). Russia anatandika bomba la kusafirisha gesi kwenda ulaya, kutwa US anazusha visa juu ya hili (tafuta majibu kwa nini US anazusha visa hivi)
 
Anachofanya Urusi hata Hitler alianza hivyo hivyo,mwishoe akajitanua na kuota mapembe. Kama hujui kuwa Ulaya wanalichukulia hili jambo seriously subiri uone moto wake. Nchi kama Poland, Romania,Norway na Sweden wanalichukulia kwa uzito mkubwa sana.
Nchi gani ya ulaya inayotaka kugeuzwa kifusi na makombora ya Urusi ?
 
Nchi gani ya ulaya inayotaka kugeuzwa kifusi na makombora ya Urusi ?
Kwanza, Nadhani NATO wakimsumbua anaweza kuichukua Alaska kwa sababu mara kadhaa amesikika akinong'ona kuwa aliuza eneo lile kimangumashi. Hivyo ni muda mzuri anaweza "kuwarudishia hela kwa staili ya aina yake" na kuchukua eneo lake.
 
Mzee kumbe bado hz nchi hujazijua vzr, pamoja na marekan kuwa na uchumi mkubwa ila anuogopa RUSSIA vibaya coz hawa jamaa wana teknology kubwa za silaha kuna zingne had USA haoni ndani. Kuprove hili that's y NASA inategemea vituo vya RUSSIA Kwenda anga la mbali fuatilia miji ya RUSSIA inaitwa STAR CITY & CARPUSTIN YARD

RUSSIA ni hatare sema tu WESTERN MEDIA ZINA I VICTIMIZE
Jamaa wamejiandaa kitambo sana tokea baada ya vita ya 2 ,Kuna mpaka mifumo ya kibank ambayo muda wwote kikinuka wanauwezo wa kujidisconnect na mataifa wanayotaka ,Rafiki wake mkubwa ni China ambayo mji mmoja wa kawaida wa China GDP yake ni sawa na Uswizi au Italy
 
Back
Top Bottom