Kujihami gani kwa kuvamia Nchi huru?
Frank Wanjiru,najua kuwa unajua Nia na malengo ya Marekani katika ukanda wa Balkan na nchi zilizojitenga na Umoja wa Kisoviet.
Najua kuwa unajua Marekani na washirika wake wana Nia ovu juu ya Urusi.
Najua kuwa unajua makubaliano ya NATO na Urusi ya kutokuongeza wanachama wa NATO kuelekea Mpakani na Urusi.
Najua kuwa unajua kuwa Marekani na Urusi na maadui wakubwa.
Najua kuwa unajua Urusi hawawezi kuivamia nchi yoyote bila sababu za maingi na mahsusi.
Kusema ukweli kubali kataa Marekani Hana Nia nzuri katika uhusiano wake na Ukraine na Urusi analijua Hilo dunia inalijua hilo wewe unajua Hilo na Mimi najua Hilo.
Sasa Urusi anajua zaidi yetu sote.
Urusi hawezi kuivamia Ukraine bila sababu nasema.
Mkuu Frank Unaamini Irani Ni Taifa huru?
Unaamini Korea Kaskazini Ni Taifa huru?
Unaamini Cuba Ni Taifa huru?
Je kwa Nini Marekani haruhusu matifa haya yajimilikie silaha za nyukilia kwa ajili ya Ulinzi wao?
Kwa Nini Marekani haruhusu Korea Kaskazini hata kujaribu makombora yake ya masafa marefu au hata kufanya mazoezi ya kijeshi ndani ya ardhi yake kwa ajili ya Ulinzi wake?
Wakati Marekani anaweza kufanya mazoezi ya kivita na nchi yoyote?
Irani ni nchi huru kwa Nini Israel hawataki nchi huru ya Irani imiliki silaha ya nyukilia?.
Ikumbukwe nchi zenye nyukilia Ni India, Pakistan,China , France,Japan,UK,UsA,Russia na Israel.
Hizi zote Ni nchi huru Zina silaha za Nuke.lakini Nchi huru za Cuba,Iran na Korea ya Kaskazini Ni marufuku.
Sasa ukipata majibu ya hayo maswali (na ninajua kuwa majibu unayo),ndio utajua kwa Nini Urusi haitaki Ukraine na wenzake wajiunge na NATO