Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

Au pengine nimuongezee swali la nyongeza...ndugu Zingzingzing

Kuna ndugu yake, rafiki, jirani au anaemfahamu aliyeponywa?

Kwa ufupi, kanuni ya uponyaji ni imani ya mtu kwa nguvu ya uponyaji (Mungu) sio Mwamposa. Huyu anachofanya ni kuamsha imani.
Naona umekubali kuwa Mwamposa anatumiwa na Mungu kwa watu wake
 
Ivi aliyeumba "ulemavu" ni nani? Na ni nani anayeombwa/ anayetakiwa na waombaji kuwaondolea ulemavu? Alikosea kuwaumba hivyo? Hakujua kama watateseka hapa duniani? Kwanini tunamkosoa muumbaji kwa kuwaaminisha walemavu kwamba wao "hawapo normal" na kuna namna ya kuwafanya wakawa "normal". Kwa matakwa ya Mungu alitaka wawe walemavu, haya yanayoletwa sasa ni matakwa ya nani? Mwamposa au Mungu huyo huyo?

Nachoka sana.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
[emoji3][emoji3]mbona kama magongo ni mapya na yanafanana.

Kama kongamano linaendelea peleka kilema au kipofu unayemjua akipona mwamini
Faith healing..hakuna kuponywa kwa kujipangia kama unavyosema..haya Kristo baada ya kuwaponya aliwaambia imani yako imekuponya usitende.

Sio kukokota watu ili uamini miujiza na uponyaji..kuwa na akili hata kidogo basi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tofautisha mafunuo na mafundisho. YESU alimponya kipofu kwa mafunuo, yani hakurudia Hilo Jambo Tena. Ila huyu Mwamposa kila siku anatumia mafuta.
Kwahiyo wewe kosa la mwamposa ni kurudia kuponya watu kutumia mafuta..pole sana acha uhafidhina naona ndio unao kusumbua.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama kichwa cha habar hapo juu, ujio wa Mwamposa, Songea ni neema.

Umeleta uponyaji mkubwa sana, vilema wanatembea, vipofu wanaona, hiyo haina kupinga.

Mimi nilikuwa simuamini lakini kwasasa naanza kumuamini.

View attachment 2387081
Unaweza leta uthibitisho wa ulichokiandika hapa? Usiseme ni Imani.. imani ni sawa na imagination na illusion hata uchawi pia ni imani.Huyo Mwamposa kwa nini asiende Hospitali kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU) na kuponya vilema na viwete?...Huyo Mwamposa ni mfanya biashara wa ki imani tu.
 
Mkwe hebu acha ufukunyuku🤣🤣🤣

Mkwe hakuna namna usikute nabii ana kipaji cha useremala pia anaweza kusaidia kwenye utengenezaji wa madawati ya dharura shule zetu za kata
 
Hii nchi walio na matatizo ya akili ni walokole sijui kwanin huwa wanachengesha kuwataja
 
Muambie apite pale mloganzila, muhimbili amalizie na pale lugalo wakati anaelekea Tanganyika packers ndio kuna wagonjwa verified sio hao wa mchongo. Wapuuzi hawataisha ktk jamii

Wangekuwa wakweli hao wagonjwa hospitalin wote wangepona
 
Kwahiyo wewe kosa la mwamposa ni kurudia kuponya watu kutumia mafuta..pole sana acha uhafidhina naona ndio unao kusumbua.

#MaendeleoHayanaChama
Unaweza leta ushahidi wa mtu unayemfahamu kuwa alikuwa kiwete miaka yote lakini kwa sasa kaponywa?
 
Back
Top Bottom