makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Unajua lakini quraan ni nini kaka?Na swali linakuja kwanini asubiri Miaka zaidi elfu 5 na Tangu kumuumba mwanadamu kushusha kitabu kilichokamilika ambacho ni mwongozo wa huyo mwanadamu asiyekamilika
Ni mjumuisho wa mafundisho maelekezo na masimulizi kabla ya kuumbwa kwa dunia mpaka kwa Muhammad, nikiwa na maana habari za adam, sijui nuhu, musa, yahya, issa bin mariam, suleyman, daudi na wengineo(habari zao zipo mule ndio masimulizi ninayomaanisha)
Quraan imeshushwa huku mwishoni kwa sababu hakuna tena muongoaji(muongozi) kama wenzetu waliopita, umma za zamani zilipata viongozi(manabii) watu wanakuwa wanakumbushwa na manabii. Hivyo hakukuwa na haja ya wao kupewa quraan. Sana sana kuna sheria chache au maneno machache manabii wa kipindi husika walikuwa wakipewa ili wawaelekeze watu mfano ni taurati ya mussa, injili, zaburi ya daudi, na kwa nabii ibrahim(a.s) pia. Na vitabu vyote hivyo havipingani na quraan.
Sababu quraan ndio ufunuo wa mwisho, hakutakuja nabii wala mjomba wa nabii, aseme fanya hiki, usifanye hiki, ni quraan tu ndio tunapata kujua hiki sawa hiki si sawa.
AHSANTE.