Nature inavyo-expose hoja ya ukamilifu wa QUR'AAN

Na swali linakuja kwanini asubiri Miaka zaidi elfu 5 na Tangu kumuumba mwanadamu kushusha kitabu kilichokamilika ambacho ni mwongozo wa huyo mwanadamu asiyekamilika
Unajua lakini quraan ni nini kaka?

Ni mjumuisho wa mafundisho maelekezo na masimulizi kabla ya kuumbwa kwa dunia mpaka kwa Muhammad, nikiwa na maana habari za adam, sijui nuhu, musa, yahya, issa bin mariam, suleyman, daudi na wengineo(habari zao zipo mule ndio masimulizi ninayomaanisha)

Quraan imeshushwa huku mwishoni kwa sababu hakuna tena muongoaji(muongozi) kama wenzetu waliopita, umma za zamani zilipata viongozi(manabii) watu wanakuwa wanakumbushwa na manabii. Hivyo hakukuwa na haja ya wao kupewa quraan. Sana sana kuna sheria chache au maneno machache manabii wa kipindi husika walikuwa wakipewa ili wawaelekeze watu mfano ni taurati ya mussa, injili, zaburi ya daudi, na kwa nabii ibrahim(a.s) pia. Na vitabu vyote hivyo havipingani na quraan.
Sababu quraan ndio ufunuo wa mwisho, hakutakuja nabii wala mjomba wa nabii, aseme fanya hiki, usifanye hiki, ni quraan tu ndio tunapata kujua hiki sawa hiki si sawa.

AHSANTE.
 
Nianze ku declare interest. Nimezaliwa katika familia ya kiislamu/ ukoo wa kiislamu. Tena sio waislamu wa wasiwasi.
But ndani ya nafsi nimesha jivua huo utambulisho wa uislamu. Siji identify na dini yoyote. Nimeujua ukweli kuhusu dini zote.
Huu uhuru wa kuikana imani na kuamua kuacha kuamini kabisa nimezoea kuuona kwa Wakristu tu. Ni waisilamu wachache sana wanaoweza kujitokeza na kusema wameamua kuacha kuamini katika dini au kuabudu na kubaki neutral (achana na wale wanaohama upande). Ilikuwa hata kama kwa vitendo hawatekelezi wanayopaswa katika uisilamu, lakini walikuwa wanakaa kimya. Kwa hili umejilipua
 
Mimi nimesema kilichoandikwa usilete maelezo mengine. Unajua maana ya kuelea?
 
Kweli jamaa umevurugwa,akopi vifungu vya bibulia vinavyosema mwanadamu achonge sanamu lake aliite bikira malia na aanze kuliabudu?
 
Ni kitu gani kipya kwenye quran ambacho hakukuwepo kwenye primitive mythologies?
 
Nazani Bado haujanielewa hata kidogo kwa sababu sipendi ligi za kijinga wacha yaishe
 
Quran haijafanya yoyote kati ya hayo uliyosema
 
Hata machizi wanaamini wapo sahihi ktk hoja zao.
 
Kuna kitu hakipo sawa either umemezeshwa au unaongea kile kinachokuja kwenye ubongo wako kwa muda huo kwanza nimekuomba ushahidi wa maandiko yoyote yale ya wayahudi wenuewe au popote kwenye spurces zinazoaminika kuonesha kwamba alikuwa akikariri hayo mahubiri bado nasubiri.

Kingine ni kwamba nabii Ibrahim (alayhi salaam) aliruhusiwa na mke wake bi sara ( radhialahu anha) kumuoa bi khajir (radhialahu anha) kama mke wake wa pili ili aweze kumzalia mwana na ndo hapo Allah( the exalted one) akambariki mwana wa kwanza wa pekee aliyeitwa ismail (alayhi salaam) ambaye pia alikuwa nabii na ndo hapo sasa nabii ibrahim(alayhi salaam) akaota ndoto ambayo ilikuwa ni wahyi (revelation) kwamba anamtoa mwana wake wa pekee kafara mbele za Allah (the exalted one) hii ikiwa ni kama kipimo cha imani kwake na akafuzu huo mtihani ndipo akabashiriwa kupata mtoto mwengine kutoka kwa bi sara (radhialahu anha) na mtoto wake atakuwa ni nabii pia hivyo atapata uzao wa mitume na manabii kutoka kwa watoro hao na uzao wao kama watakuwa ni waongofu.

Ushahidi huu tunaupata kwenye quran takatifu surah saffat aya ya 101-102

Quran 37:101-102
 
Kwanini Mungu aumbe binadamu asiyekamilika? Ili iweje?
Au ndo ili atende dhambi mwishowe amchome moto? Anapata faida gani sasa
Mwanadamu ameumbwa na udhaifu kwenye maumbile yake kulinganisha na viumbe vingine kwa maana yeye hana nguvu kama hao ila haimaanishi hana akili timamu ya kupambanua mambo, kwenye sekta hiyo amependelewa na ndio maana yeye ni kiongozi na msimamizi wa mambo hapa duniani na wengine wamedhalilishwa chini yake.

So mtu akifanya dhambi amefanya kwa maamuzi yake binafsi na mwisho wake ukiwa mbaya asimlaumu mtu.
 
Kaun a majini na watu ili baadae awatumbukize jahannamu? [emoji848]... that's insane

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi unafahamu asili wanadamu walikuwa wapi kabla ya kuja hapa duniani? sisi hapa sio kwetu tumekuja tu kwa muda kisha tutarejea kwenye makazi yetu ya milele, mwanadamu hajaumbwa ili afe ameumbwa ili aweze kuishi milele sasa kuna watakaokataa kurudi huko na wataamua kushika njia ambazo sio muongozo wa yule aliyewaumba nae hana njia nyingine zaidi ya kutimiza ahadi yake ya kuwatumbukiza katika jahannam kwa kule kuasi kwao.

"Tukasema: Shukeni humo{ardhini} nyote; na kama ukikufikieni uongofu utokao kwangu, basi watakaofuata uongofu wangu huo hawatakuwa na hofu juu yao wala hawatahuzunika."

"na wale waliokufuru na kuzikanusha aya zetu, hao ndio watu wa motoni, na humo watadumu milele"

Quran 2:38-39

Kwahyo ukielewa hapo hupati tabu kujua chanzo cha watu kuunguzwa motoni ni nini na mola wako hamdhulumu yeyote anampa stahiki yake.
 
Huo mfano bado haumake sense kwann mungu aumbe watu alafu awatese baadae.
.
Ngano inatengwa na makapi kwasababu makapi hayatumiki na tunajua kabisa hata kabla hatujayapanda. Sasa kama na mungu anajua kabisa kama watu flani ni 'makapi' inamaana huyo mungu ni kiumbe flani hivi mkatili sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna ushahidi wowote wa kwamba mwanadamu alikua huko unaposemea. Sisi binadamu, kama ilivo wanyama wengine, tunazaliwa, tunapumua, tunakula mwisho tunakufa. Utofauti wetu na wanyama wengine ni vile tulivo na uwezo mkubwa wa kifikiri...
.
Ushahidi pekee wa hayo mambo unayo yasema ni aya tu za quran, kitabu ambacho hakuna ushahidi kama hata kililetwa duniani na muumba wa ulimwengu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787]sasa mbona quran wanasema imetoka kwa mungu. Quran inayosema usiku jua linazama (nafkiri matopeni). Quran inayosema mtume alishika jua mkono mmoja na mwezi mkono mwingine na akaugawa mwezi katikati. Quran inayosema mtume alipaa kwa farasi mwenye mabawa... no any scientific reasoning iko hapo. Hakuna scientific precision hapo.
.
Ukiangalia habar za maafuriko ya nuhu utaona mtunzi wa hio hadith hana ujuzi wa sayansi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitabu kinakuaje cha mungu wakat mungu mwenyew hayupo[emoji2377]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Mungu hajawahi kuwa na Nabii wala Mtume yoyote yule kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu akiwa amekamilika KWA KILA.kitu. ..

Kusema sijui Mungu alimtuma Nabii nani nani sijui KWA watu ni kuidhalilisha sifa ya uungu alio nao.."[emoji118]

Kwa hiyo akina Mussa, YESU, Paulo, Petro, Elia, Yohanna etc walijituma na hawakutumwa si ndiyo? Kwa hiyo wale hawakuwa mitume bali matapeli na walaghai siyo?
 
Uliwaona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…