Pengine sasa ametambua ulikuwa siyo uamuzi wa busara na ni mzigo kutetea mradi huo wa international airport na Vitu vingine Chato, maana havina faida pana kwa wana Chato na taifa pia
Mfano nchi jirani ya Congo DR , mtawala wake alijenga uwanja wa ndege mkubwa na sasa ni mahame :
Mahame ya kijiji cha Mobutu Sese Seko Ngebu wa Zabanga Zaire Congo DRC
22 Dec 2018
Katika mji wa Gbadolite alikotoka, Rais Mobutu Sese Seko alijenga kasri kubwa la kifahari na uwanja wa ndege ambao ndege za kusafirisha bidhaa za anasa kama vile mvinyo ghali kutoka Ulaya zilitua na kupaa. Njia ya kutumiwa na ndege kupaa na kutua katika uwanja huo ilikuwa kubwa kiasi cha kuweza kutumiwa na ndege kubwa ya wakati huo Concorde - ambayo aliikodi mara kwa mara. Lakini alipotimuliwa madarakani mwaka 1997, kila kitu kilisimama. Sasa ni mahame.