Mtuache
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 260
- 712
🚨Shirika la ndege la gharama nafuu kutoka Ireland, Ryanair, limeibuka na wazo jipya la kupunguza zaidi nauli za ndege: kuondoa viti kwenye baadhi ya safari zake.
Mpango huu unalenga kuanzisha safari maalum ambapo abiria watasimama kwa muda wote wa safari, kwa kutumia mikanda ya usalama maalum iliyoambatanishwa kwenye kuta za ndani ya ndege. Teknolojia hiyo imeelezwa kuwa tayari ipo kwenye hatua za majaribio.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa, mfano wa safari inayotajwa ni kutoka Tanzania hadi Ufaransa, ambayo inakadiriwa kuchukua masaa 9 angani, huku nauli yake ikisemekana kuwa ni euro 10 tu — takriban shilingi elfu 30 za Kitanzania.
Mpango huo unalenga hasa kuwafikia wasafiri wa kipato cha chini wanaotamani kusafiri nje ya nchi kwa bei nafuu, sawa na nauli ya ndani ya nchi kupitia treni au mabasi.
Swali linabaki:
Uko tayari kusimama masaa 9 angani kwa bei ya soda na maandazi?