Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Uzi bila picha ni majungu tu
 
KIZIMKAZI hana muda na Watanganyika. Majizi yanajipangia nauli tu. YY anasubilia majanga ndio atulie ndani y nchi. Kama majanga hakuna anasepa majuu huku anawachia wajipigie.
 
Huyu Mama tangu amekabidhiwa nchi, kila kitu kimepanda bei karibia mara dufu!
Halafu huwezi kumsikia mahali akizungumzia hii changamoto ya bidhaa kupanda bei mara dufu, huku kipato cha mwananchi kikiendele kubakia vile vile.

Yaani kwake anaona kama ni jambo tu la kawaida!! Hata sioni kama anaguswa na haya maumivu wanayopitia wananchi wengi kuhusu huu upandaji maradufu wa gharama za maisha!! So sad!! 🙁
 
Habari za asubuhi!

Baada ya tangazo kuwa nauli mpya ya magari ya usafiri wa umma kuanza leo tarehe 08 Desemba 2023 natumaini kuna wana JF ambao wamepata bahati ya kusafiri siku ya kwanza ya nauli mpya.

Umeingia kwenye chombo cha usafiri leo, ukilinganisha na jana au siku za nyuma umelipa shilingi ngapi kutoka point A to B?

Nauli kwako imepanda kiasi gani? Umepata changamoto yoyote kulipia ongezeko?

Safari njema huko.
 
Hii ni kweli, nampenda ruto huwa anazungumzia kupanda kwa bei ya bidhaa Kenya, huyu wetu sijawahi msikia
 
Ni balaa tupu mkuu, nimepanda Moshi - Arusha badala ya 3,000 sahivi ni 5,000
 
Nauli za Samia zinalenga kuwasaidia matajiri waliokopa BENKI kupata fedha za kulipa mikopo.

Kumbuka Kuna Mbunge wa Morogoro [Abuu] mwenye Mabasi zaidi ya 200 yana safari za Da-Moro-dodoma-Mbeya-Arusha.

Waziri anayejiita Msukuma ana mabasi, mawaziri wana makampuni ya usafirishaji.
Shemeji yetu[mume wa bi'tukinao ndio mkuu wa wanaopandisha nauli], ameridha na amesema walio omba ni Super Feo na sijui mpuuzi gani.
 
sasa kila chapisho mnamsifia, mnategemea nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…