Kama ilivyo ada kwa UVCCM kupongeza mazuri ya serikali, basi ni wakati muafaka UVCCM waandae maandamano ya kumpongeza Raisi kwa kupandisha bei ya nauli, ili wabunge wenye mabasi akina Abood, Msukuma na wengine akina Super Feo watajirike.
UVCCM itapendeza kama maandamano ya kupongeza nauli mpya yatafanyika jumatatu 11-12-2023.
USAFIRISHAJI: Leo Desemba 8, 2023 Watumiaji wa huduma za Usafiri za Mabasi ya Masafa Marefu (Mabasi ya Mikoni) na Mafupi (Daladala) wanakutana na gharama mpya za Nauli.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), nauli za Mabasi yote zimepanda baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Watoa Huduma na Wadau wa Usafiri (Wananchi).
Mama toka aingie madarakani, si mafuta, si tozo, si nauli zinapanda tu na hata mafuta soko la dunia yapo chini sana sema hizi kodi ni zaidi ya nusu ya bei.