Nataka niulize hili swali kabla sijaenda kulala.
It is just a rhetorical question.
Itakuwa vipi kama wananchi wakisema,"Nyie Polisi,msimkamate Tundu Lissu?"
Kisasi ni tiba nzuri na dawa ya kuwaadhibu wanaodhulumu haki za wengine .
Sijajua kama Lisu alikuamatwa kwa kosa gani ?
Ila ni lazima sasa pawe na sehemu maalumu ya kulipa kisasi ili CCM wale Chadema wakilia .
Kilio kisipolingana Chadema watakimbiana.
Ni vizuri hata yule anayetoa amri ya kupiga na kuua na kukamata wapinzani naye ajue kua nguvu hiyo hiyo itaingia kwenye chama chake .
Ilitakiwa mpaka sasa nchi nzima pawe na maandamano na ndio uwe mwanzo wa mabadliko . Vinginevyo CCM iwe katika mazingira magumu.
Ni lazima nguvu ya umma ionekane kwa macho .
Ofisi za CCM bado zipo salama kila mahali .
Wanafikiri ni rahisi ndani ya nchi moja kundi moja lenye nguvu sawa na lingine kutumia polisi kama fimbo ya kufanya wanachotaka .
Ni bora wanachama wote wakaingia mitaani ili kama ni kukamatwa wakamatwe na kujaa magerezani na vituo vya polisi .
Hali ikae sawa mapema .
Eti Uchaguzi utakua huru na haki kwa hawa ambao hata mikutano tu sio huru.? Kama MKUTANO tu watu wanapigwa itakuwaje kwenye kura zinazomnyima Samia Ulaji na Marafiki zake na ndugu zake kutoka Oman walijazana ndani ya Tanganyika kupora kila kitu ?
Hapo Rushwa itatolewa mpaka kwenye vyombo vya dola ili kuwadhibiti wapinzani ?