Walitaka kupindua nchi live na kusababisha uasi kwa kufadhiliwa na hawa mnaowarudisha leo kuja kuchukua rasilimali alizokuwa amazitaifisha .
Hebu mkae mtafakari kuwa ingekuaje kama kila kitu kingebaki mikononi mwa Wazungu ,waarabu na wahindi?
Tungekua na uhuru gani ?
Yaani mpaka ikulu ilikua ni mali ya wazungu ,majaji wote walikua ni wazungu , Askari wote wenye vyeo walikua ni wazungu. Nyumba zote zinazomilikiwa leo na NHC zilikua za waarabu na Wahindi na wao ndio walikua wanafanya biashara kwenye nyumba zao katikati ya miji yote nchini . Maeneo yote ya Ofisi za wakuu wa Wilaya kama BOMAN ni maeneo ya Wazungu na neno la Waingereza . Mashamba yote ya Korosho,pamba, Mkonge, Korosho, Chai,Tumbaku, Zabibu, Maaple ,Minazi , Machungwa ,Misufi, Maembe , Shahiri, ngano, mahindi na maharage kule Arusha n. k yote yalikua ya wazungu . Waafrika hawakua hata na maeneo ya kujenga zaidi ya kuishi kota za wazungu na kuwa vibarua . Mapori yote yalikua ni mali ya serikali .
Tanganyika haikua na viwanda vingi wakati wa Mkoloni kwa sababu viwanda vingi vilikuwa Kenya na Zimbabwe . Tanganyika ilikua ni sehemu ya kuchota mali ghafi.
Mtume na Nabii Mtakatifu Julius Kambarage Nyerere Nabii wa Afrika na Mzalendo alitaifisha Mali zote na ardhi za Mashetani waliokuja kuwaua waafrika na kutwaa rasilimali zao walizoumbiwa na Mungu kwa ajili ya vizazi vyao wakiwemo Wamasai Waliofukuzwa na Waarabu koko toka Misri kwenye bara la Mtu mweusi . Na leo Waarabu wale wale wamewafata tena kule Loliondo kwa mgongo wa mjukuu wao mwarabu koko.
Nyerere akajenga viwanda vingi sana ili kutumia malighafi zetu wenyewe kuzalidha. Tulizalisha nguo na nyuzi kwa pamba zetu wenyewe . Tulikua na viwanda vya mafuta ya Karanga leo hata ukimwambia Abadili kuwa tulikua na mafuta ya Karanga ,tan band badala ya Blue band ya Kenya hajui ,anachojua ni kuagiza makontena ya mafuta kutoka Indonesia na China basi na kutangaza kuwa watanganyika hawawezi kuzalisha vitu vyao . Kanga za urafiki zilikua ni bora sana zikishindana na kanga za Kenya.
Kwa hali ilivyokuwa Chuki ya wale walionyanganywa mali zao ilikua ni kubwa sana kwa Nyerere. Na Ukumbukwe hakua ni Mwanajeshi bali Raia lakini Mzalendo kama Mwanajeshi ,Hali iliyopelekea kuwa na majaribio mengi ya kumpindua lakini kutokana na uzalendo wa Watanganyika waliokua wanampenda Rais wao majaribio yote yalishindikana. Hujuma za kiuchumi ziliendelea zaidi baada ya Kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti. Nyerere akasoma alama za Nyakati za Mfumo wa Vyama vingi na jinsi nguvu ya Mataifa makubwa inavyotumika kutumia pesa kuleta vita na uasi kwenye nchi za Afrika kushinikiza vyama vingi. Nyerere hakutaka kuwa rais wa Nchi ya Kibepari mana yeye na chama chake hakuamini katika unyama wa mabeberu na dhulma za nchi za Kibepari. Akaamua kung'atuka madarakani.
Kilichofuata ni Wale wale waliokua wanatamani maisha ya anasa kuanza kujipanga kupitia Demokrasia ili wakamate na kuifanya mali yao wakiwemo vijana walipoenda siasa za kujilimbikizia mali kwa kukwapua mali za umma. Walijimilikisha mpaka nyumba ambazo hata Wakoloni hawakuzifanya mali binafsi. Waliuza mapaka nyumba za Polisi ,mahakama,TISS n.k. na kuzifanya mali zao na familia zao na marafiki zao.
Wakajiwekea sheria za mafao na mishahara mikubwa na marupurupu makubwa bila kujali hali ya uchumi wa nchi. Wakabadilisha utamaduni wetu wa kuitana Ndugu na kutunga sheria ya kuitwa Mheshimiwa. Wanajiona wao sio ndugu zetu bali waheshimiwa na kuanza kujiona kama wazungu weusi mbaya zaidi wakawa wabaya zaidi ya wakoloni chini ya mifumo kinyama ya Kibepari.
Tujiulize,
Tulikua watu milion 14 maji bure , umeme ni Mita madeni kibao.
Elimu bure vitabu vimejaa librari tunapewa mpaka madaftari na penseli.
Matibabu bure .
Wafanyabiashara wachache .
Simu madeni kibao.
posta madeni kibao.
Benki kubwa mja NBC .
Wafanyakazi kama walimu walikua na maisha mazuri na shule za serikali zilikua za bweni zikiwakutanisha wanafunzi kutoka kila sehemu alimradi awe amefaulu kwa ufaulu wa Juu.
Bado vita ya Uganda ikaibuka, vita za Nchi za kusini ambazo zilikua zinatokana na waafrika wenzetu kudai uhuru hivyo Tanganyika ikawa ndiyo mfadhili na msaada mkubwa kwao kijeshi.
Kama sio uzalendo Mwalimu angewezaje kujenga viwanda na mashirika ya umma zaidi ya 360 kwa mazingira kama hayo ?
Leo hii , Tuko mil.65 tozo kila mahali. Watalii kibao,mabilionea wa ndani kibao, Wafanyabiashara kibao.
Majengo yanayolipa kodi ya majengo na ardhi ni mengi nchi nzima.
Bandari inapitisha mizigo ya ndani na nje mara mia moja zaidi ya kipindi cha Mwalimu.
Wafanyakazi wanadhulumiwa pesa zao za pension kwa sababu tu ya ubinafsi wa Mabepari kuanzisha miradi ya kifisadi na wao kuwa mabilionea huku watumishi wakibaki kuwa fukara. Badala ya kuwapiga kitanzi wezi kwenye mifuko ya jamii ya wafanyakazi kama NSSF wanaopigiwa mabomu na risasi ni wale wanaodai mafao yao ambayo yamegeuzwa kuwa dili la watu kupiga pesa kwa kujenga majengo yasiyo na tija kwa wafanyakazi zaidi ya Watu wachache kupiga dili.
Wakaja watawala walimfuata Nyerere wakaungana na wapiga dili kujilimbikizia mali huku wakiwateua marafiki zao kusimamia mashirika ya umma kwa lengo la kupeana fadhila na sio kuendeleza mashirika . Bodi za mashirika za kumwaga lakini wamewekwa Makada na marafiki ili wachote pesa za kampeni kurudishana madarakani na kuendelea kutafuna nchi.
Wengine sasa wanakuja na marafiki zao wakijifanya ni wawekezaji kumba ni wao na kujimilikisha mpaka bandari na kila sehemu yenye kukusanya pesa tu. Hawataki kujenga viwanda bali kuanzisha makampuni ya kushika tenda za serikali kuchota pesa . Hawajengi kiwanda cha Sukari na Mbolea ,hapana wanataka kutengeneza vikampuni vya kuingiza sukari bila Kodi halafu wanauza kwa bei ya juu wapige pesa .
Hawa kamwe hawatamsifia Mwalimu zaidi ya kuwasifia wale waliowaruhusu na kuwawekea mazingira mazuri ya kuigeuza nchi kuwa shamba la wageni wao.
Wengine waliambiwa huyu Mzee akiendelea kuwa Hai wewe huwezi kuwa Rais kamwe .
Mwalimu akaondoka akiwa mzima kwenda check akarudi akiwa paradiso. Nini kilitokea bado hakijawekwa wazi kabisa kiuchunguzi na hakijachunguzwa.
R.I.P.Mwalimu JKN.
Shujaa wa nchi za Kusini Mwa Afrika na wengine leo wanapata fursa ya kupiga picha kwenye vikao vikubwa duniani kwa mgongo wako .
Shukrani ya Punda ni Mateke