Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Badala ya kila nyumba kuungwanishwa na umeme wa bei nafuu ,wakaletewa mwenge ili uwamulike mpaka huko vijijini na mipakani, sindio vifkra za MKT hizo

Mambo ya lamli za Mlingotini bagamoyo, na Mzee Forojo Ganze. Hili watu hawataki kabisa kulisema. Shekhe Yahya, marehemu, alikuwa anasema mwenge ni ishara ya kishetani. Sijui ana ukweli au uongo kiasi gani
 
Waulize wazee watakwambia,unafahamu hata historia ya Mwamwindi na Kreluu ilikuwaje mpaka akampiga risasi?msipende sana kusoma storie za kwenye vitabu zimepotoshwa kwa maslai ya wakupwa

Unasema kama vile kusimuliwa kuna ukweli usiyopidishwa. Na wanaosimulia ni waongo namba moja. No research no right to speak.
Waafrika bila kufanya tafiti zenye kuutafuta ukweli na kuusema ukweli ulivyo, tutaendelea kurogana na kujiona ndio maendeleo, wakati tunazidi kuwa mafukara.
Ukweli pekee ndio utatuweka huru
 
Kama umezaliwa miaka ya 70 na hujui yaliyotokea basi utakuwa ni baba/babu mpumbavu sana kuwahi kutokea. Kuhusu Mwalimu Nyerere naweza kusema ana mazuri mengi kuliko mabaya. Aliipenda Tanzania na alitaka kila mtanzania afaidi keki ya taifa ila bahati mbaya akawa haambiliki. Kosa lake kuu ni kuamini yeye anajua kila kitu.
Unajua aliyewaharibia Wazanzibar Maisha?mpaka leo hii hakuna amani hasa kipindi cha uchaguzi sababu yake ni yeye na kila mwaka wapinzani wanashinda,hata mapinduzi yenyewe hayakufanywa na wazanzibar bali wamakonde walipitia Tanga kwenda Zanzibar na kufanya huo unyama wa mauaji kwa faida ya nani,yupo anayejua

Leo hii Zanzibar bila mapinduzi ingekuwa mbali sana kiuchumi tofauti na Tanganyika,
 
Unasema kama vile kusimuliwa kuna ukweli usiyopidishwa. Na wanaosimulia ni waongo namba moja. No research no right to speak.
Waafrika bila kufanya tafiti zenye kuutafuta ukweli na kuusema ukweli ulivyo, tutaendelea kurogana na kujiona ndio maendeleo, wakati tunazidi kuwa mafukara.
Ukweli pekee ndio utatuweka huru
Iko hivi nazani hata kesho ukiamka huwezi kumkoza mzee wa miaka 70,80 na kuendelea,au tafuta sehemu ya tukio husika lililowahi kutokea halafu waulize wahusika wa pale hasa wazee,utaupata ukweli no utafaidika kuliko kusoma vitabu vilivyoandikwa kwa kupotosha ukweli
 
Unajua aliyewaharibia Wazanzibar Maisha?mpaka leo hii hakuna amani hasa kipindi cha uchaguzi sababu yake ni yeye na kila mwaka wapinzani wanashinda,hata mapinduzi yenyewe hayakufanywa na wazanzibar bali wamakonde walipitia Tanga kwenda Zanzibar na kufanya huo unyama wa mauaji kwa faida ya nani,yupo anayejua

Leo hii Zanzibar bila mapinduzi ingekuwa mbali sana kiuchumi tofauti na Tanganyika,
Hakuna aliyewaharibia maisha wazanzibar. Ni wenyewe. Nani huyo mtaje ili dunia ikucheke? Shida yetu kubwa hatutaki kukubali tunawajibika kwa madhira yetu wenyewe. Kila tatizo tunasukumia watu wengine. Baada ya mapinduzi, ilikuwa dhahiri yangetokea mapinduzi mengine tena sio muda mrefu. Na hali ya usalama wakati ule, ilikuwa inaangaliwa kwa dhana ya ubepari au ukomunisti.
Je Zanzibar, iligawanyikaje katika hayo makundi mawili? Kina babu na wenzake walishakuwa wakomunisti. Na walikuwa peke yao au wakubwa wengine? Je Mzee Karume alikuwa upande gani? Mwarabu aliyepinduliwa?
Nani aliyeomba kuunganisha nchi na kwa maslahi ya nani? Mambo ya maisha hayana nafasi kwa watu vigeugeu.
Ukigeuka nyuma ukakatataa maneno yako mwenyewe uliyoyasema kwa mdomo wako, unakuwa mnara wa chumvi
 
Iko hivi nazani hata kesho ukiamka huwezi kumkoza mzee wa miaka 70,80 na kuendelea,au tafuta sehemu ya tukio husika lililowahi kutokea halafu waulize wahusika wa pale hasa wazee,utaupata ukweli no utafaidika kuliko kusoma vitabu vilivyoandikwa kwa kupotosha ukweli

Ndio maana nakwambia mnadanganyana. Hawa wazee waanze kuandika ili hata akifa, wengine wasome na kuelimika. Tumepoteza elimu kubwa sana Africa sababu ya kusimuliana. Unayemsimulia hajui maana ya unayoyasema. Akiyapindisha kesho tunasema ndio ukweli wenyewe.
Urongo. Tuandike. sarufi zipo ili watoto na wajukuu waje kuyasoma. Mbona misaafu imeandikwa na haikuachwa kwa lugha ya masimulizi? Unajua maana yake nini?
Achana kusikiliza hadithi tena za watu wenye akili finyu wasiojua hata maana ya wanayoyasimulia. Waandike tumalize mambo
 
Mambo ya lamli za Mlingotini bagamoyo, na Mzee Forojo Ganze. Hili watu hawataki kabisa kulisema. Shekhe Yahya, marehemu, alikuwa anasema mwenge ni ishara ya kishetani. Sijui ana ukweli au uongo kiasi gani
Mwenye asili Aachi asili. Lile ni tambiko la kweli kabisa. Ila mbona hatutumii asili kitajirisha nchi😎 ,
 
Uongo mtupu.
Tukisema watu walivaa magunia mnatuona waongo,Kingine hiki kulikuwa na kodi ya kichwa tena ilikuwa pesa ndogo sana,ulikuwa ukilipa unapewa card fulani ambayo ukikutana na mgambo unaonyesha

Lakini kutokana na umasikini uliokubuhu baadhi ya wanaume walikuwa wanakimbia nyumba na famiria zao toka alfajiri na kwenda kujificha maporini na kuludi usiku ili kuwakwepa migambo,jiulize huo mda anaojificha maporini angezalisha kiasi gani akiwa nyumbani?
 
Wakati unazaliwa mwaka wa sabini nilikuwa tayari nina miaka kumi na nne. Kwa hiyo tafadhali acha kuandika uongo kwa maslahi yako. Sijahadithiwa kama wewe.
 
Wakati unazaliwa nilikuwa na miaka kumi na nne. Kwa hiyo tafadhali acha kuandika uongo kwa maslahi yako.
Usizani tanzania yote ilikuwa kama Daresalaam kwa kipindi hicho na Mikoani kulikuwa sawa na wilayani au na Vijijini,

Unajuwa mtu kipindi hicho alikuwa anakwenda hospital mfano hizi pravete na zilikuwa chache za mission yaani wamisionari halafu unapewa dawa imexpire,unaambiwa hii unaweza kutumia hata mwezi mmoja haina tatizo,na kuna selikali,sijui kama huko zilikotoka Wazungu walikuwa wanatumia,na unarizika unakunywa kabisa
 
Hebu nieleze ni mkoa gani watu walikuwa wanavaa magunia ezi hizo? Usilete stori za kutunga hapa.
 
Mfano hai tafuta historia ya Safari ya D.k Salim Armed Salim alipokwenda mtwara akawakuta watu wamevaa magunia,ikabidi akamwambie Rais wafanye mpango waruhusu mitumba maana ilikuwa imepigwa marufuku,tulikuwa tunategemea viwanda vya ndani vizarishe nguo,na vilikuwa havitoshelezi.

Watu wameshawahi kuuziwa pafu za sigara,yaani mranguzi anauza sigara iliyowashwa,ukipiga pafu moja unatoa hera,anapewa mwingine nyie vijana tumetoka mbali
 
Hebu jifunze kuandika kwanza dogo. Sina haja ya kutafuta hiyo historia kwani nilikuwepo. Sijahadithiwa kama wewe uliyehadithiwa.
 
Nyerere last time alikuwa Raisi wa Tanzania almost 40 years ago, leo bado mnafikiri shida zenu ni Nyerere, at least shukuru hakutuachia vita kama haya matekaji ya siku hizi yanapotupeleka, na Kwa msio jua Nyerere alikuwa ahead of his time, yeye ndio alipigania nchi iwe na vyama vingi huku CCM aliyoianzishia walikuwa wanatutisha vyama vingi vitaleta vita, Nyerere nakubali sera zake za uchumi zilituletea umaskini lakini alionekana kubadilika mwishoni, alikuwa mtu wa haki na hakuwahi na Tamaa, alikufa maskini kabisa, na ingekuwa anaishi Nina uhakika asingekubaliana na siasa za CCM za wizi wa kura, kubambikia kesi, utekaji au kuuza maliasiri za nchi. He was a good man
 
Back
Top Bottom