Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

usitetee mipango mibovu. Hata Nyerere mwenyewe alikiri kukosea
Hebu Kwanza!

Ni wapi "nimetetea mipango mibovu"?
Kuhamia vijijini ilikuwa "mipango mibovu"? Nani kasema kuwa ilikuwa "mipango mibovu"?
Kwa vile tu umekariri ulicho soma bila kutumia akili, ndiyo uje hapa kunieleza nikubaliane na wewe kuwa ilikuwa mipango mibovu?

Halafu kuonyesha jinsi gani usivyo tumia akili yako sawasawa, nionyeshe mahali ambapo "Hata Nyerere mwenyewe alikiri 'kukosea'" - kwa kuanzisha vijiji, au kukosea katika mambo yote? Ni binaadam yupi asiyekosea maishani mwake?

Ulitegemea Nyerere awe malaika? Kila mara watu wa aina yako mnakimbilia hiyo hoja ya Nyerere "kutokosea", jambo ambalo mna lizua wenyewe kwa kukosa hoja za kupinga aliyo yasimamia kama kiongozi.
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukari, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni nchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Haukumshinda, kuongoza ni changamoto na alikuwa na nia njema ndio maana alianzisha viwanda zaidi ya 100 nchi nzima.

Waliorithi ofisi yake walikuwa watu wa hovyo wenye kuendekeza siasa za kibinafsi zenye kuabudu makundi na majungu.

Uwezo wetu sisi watanzania wa kujiongoza wenyewe ni mdogo sana. Dodoma miaka michache iliyopita ulikuwa mji uliopangiliwa vizuri sasa nenda leo uone namna maafisa ardhi kwa tamaa zao walivyouharibu ule mji.
 
Watu wenye roho mbaya ndivyo walivyo uwa wanajijali wenyewe tu na wanapenda sifa na kuabudiwa na ndivyo hali ilivyo hivi sasa nchini mwetu,
Nyerere anaabudiwa kuliko Mwenyezi Mungu aliyetuumba,kila kitu utasikia Mwalimu alisema!
Angalia hata Muungano tulionao ulistahili kabisa muundo wake kupitiwa upya lakini ni kama vile kila kiongozi anaogopa kuchokonoa jambo hilo kwani anaona atauudhi mzimu wa Nyerere sasa labda tusubiri hadi vile vizee vyote vinavyomuabudu huyo bwana mkubwa vife vyote.
By the time wanakwisha na wewe utakuwa umego. Ni generations nyingine tatu au nne mambo yatakaa tofauti. mark my words.

Halafu Nyerere hakutufundisha kuiba na kula rushwa. Na hili nalo uliongeze kwenye matatizo yanayokusibu.
 
Binafsi namkubali mwamba Kuibadili nchi kutoka umasikini wa 0 ni kazi ngumu sana , Laiti angekata tamaa Tusingekua hapa..

Watu hawakua na elimu ya kutosha, Serikali haina akiba yeyote, Watu walikua na Mindset ya kusaidiwa na serikali...

Alipata tabu sana mwalimu
 
Tunapokuwa tukiongozwa na uvivu wa kufikiri kila udhaifu tunamtupia Mwalimu Nyerere.

Leo hii pale wizara ya ardhi ili mtu apate hati yake katika eneo analolimiliki ni lazima atoke jasho, haki ni ya kwako lakini unahangaishwa kupanda zile ngazi kila kukicha.

Eneo la mbezi beach square meter moja ina thamani ya tshs 350,000 zidisha mara ukubwa wa eneo analomiliki mtu, unapata kiasi cha pesa kuanzia milioni 500 kwenda juu.

Huo ni mtego kwa maana ya wao watu wa ardhi kutaka uwasilishe makaratasi yenye kuonyesha umiliki wako wa asili vinginevyo wanakupa invoice yenye kitu kinachoitwa ACQUISITION COST ambayo ni bei ghali sana, lengo lao ushindwe kulipia hiyo pesa halafu wao mawaziri na wakurugenzi wanachukua eneo lako kiurahisi sana!.

Ni wizi unaofanyika kwa njia za kisiri sana, ni uporaji unaohalalishwa na sheria za nchi.

Haya ni masuala ambayo Mwalimu Nyerere hakuyaacha wakati wa awamu ya kwanza ni dhuluma zilizokuja miaka ya kuanzia awamu ya pili mwishoni na ya tatu.
 
By the time wanakwisha na wewe utakuwa umego. Ni generations nyingine tatu au nne mambo yatakaa tofauti. mark my words.

Halafu Nyerere hakutufundisha kuiba na kula rushwa. Na hili nalo uliongeze kwenye matatizo yanayokusibu.
Japo sijakuelewa ulichokusudia lakini naheshimu maoni yako.
 
Japo sijakuelewa ulichokusudia lakini naheshimu maoni yako.

Ni hivi kusema wafe watu ndio legacy yake ipotee sio kitu cha siku mbili tatu. Pengine generation kadhaa nyingine. Wewe na mimi tutalikosa hilo boti.
The roots are so deep. It requires same level of thinking to uproot them
 
Hebu Kwanza!

Ni wapi "nimetetea mipango mibovu"?
Kuhamia vijijini ilikuwa "mipango mibovu"? Nani kasema kuwa ilikuwa "mipango mibovu"?
Kwa vile tu umekariri ulicho soma bila kutumia akili, ndiyo uje hapa kunieleza nikubaliane na wewe kuwa ilikuwa mipango mibovu?

Halafu kuonyesha jinsi gani usivyo tumia akili yako sawasawa, nionyeshe mahali ambapo "Hata Nyerere mwenyewe alikiri 'kukosea'" - kwa kuanzisha vijiji, au kukosea katika mambo yote? Ni binaadam yupi asiyekosea maishani mwake?

Ulitegemea Nyerere awe malaika? Kila mara watu wa aina yako mnakimbilia hiyo hoja ya Nyerere "kutokosea", jambo ambalo mna lizua wenyewe kwa kukosa hoja za kupinga aliyo yasimamia kama kiongozi.
Tafadhali kijana - wewe unaona kuhamia vijiji vya ujamaa ilikuwa mipango mizuri? Kutaifisha mashamba ilikuwa mipango mizuri? Wewe unaujua umri wangu hata ukasema nimekariri? Na wala hakuna sehemu nimesema Nyerere amekosea katika mambo yote. Mimi degree yangu ya kwanza nilipata mwaka 1980, kwa hivyo hiyo enzi ya Nyerere uliyoisoma kwenye vitabu mimi nimeipitia katika maisha yangu.

Akili yako unayotumia ambayo iko na muelekeo mmoja inakufanya uwe kipofu.
 
Hayati Mwalimu ni Siasa za Ujamaa na Kujitegemea ndio zilimshinda na alishindwa kukiri kuwa zimemshinda na KAMA KAWAIDA YA WATANZANIA WANAKUSHAURI MAMBO UNAYOPENDA KUYASIKIA HUKU WANAKUOGOPA KINAFIKI.
Kambona alimwambia ujamaa haufai,tukaishia kumtusi kwenye nyimbo za mchakamchaka shuleni,hashauriki yule,aliitwa haambiliki enzi zake
 
Ni hivi kusema wafe watu ndio legacy yake ipotee sio kitu cha siku mbili tatu. Pengine generation kadhaa nyingine. Wewe na mimi tutalikosa hilo boti.
The roots are so deep. It requires same level of thinking to uproot them
Kizazi 1980s hakimtukuzi huyo mzee
 
Hali ni mbaya vijana wetu wameingia kwenye hatua ya kupinga kila kitu ! Sikuhizi vijana wetu wana pinga hata uwepo wa Mungu wanatafuta wabaya kila siku.
Nyerere kwa kipindi chake alifanya yote aliyoamini yanaweza kuivusha nchi nia yake traditional ilikutana na ukinzani wa kila aina ndani na nje nadhani hiyo ni fundisho kwamba wenye nia njema na nchi huwa hawawi wengi na wanazungukwa na watu wanaojifanya wana nia ya pamoja kumbe wanawazia matumbo yao na familia
 
Kweli hata ccm haisababishi umasikini wa watanzania ila INAONGOZA vizuri sana na magaidi yanashugulikiwa
Umeandika nini?

Tanzania watu hawataki kulipa kodi hakuna uzalendo kabisa na hao wachache wanaotoa kodi zinapotelea kwenye matumbo ya wachache...

Watu ni lazima walipe kodi hakuna namna na CCM inatakiwa ilisimamie hili swala kikamilifu..
Majizi,majambazi mafisadi lazima yachukuliwe hatua..
Hii kinga ya Raisi hatuitaki,inatakiwa iondoshwe mapema..kama mtu alivurunda amekwiba ashitakiwe achukuliwe hatua kali ili wengine wajifunze...
Ccm inatakiwa ijue hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Yule mzee alikua anakiri kukwama dhahiri kabisa.Ni kwamba tulishindwa kumuelewa na kuchukua hatua muhimu.
-alitoa kitabu cha kuhusu Ujamaa na kusema kila akikisoma(maandishi na si uhalisia)hakuona kilipokosewa hadi akaja kusikia azimio la Zanzibar.
-alikiri kukosea mambo mengi na mengine yalikua mema tu.Akaendelea kuasa kwamba shida ni sisi hatujui kuacha mabaya na kuchukua mazuri yaendelezwe kwa mazuri mengine ili kuleta ustawi.
-aliikataa CCM hadharani na kwa hisia alisema kwa sababu inaenenda hovyo,angeiacha.Si mama wala baba yake hiyo CCM.
-alienda mbali akatuletea uhalisia(siyo utunzi)wa nchi kimaandishi jinsi nchi ilivyokua imeharibika kimifumo/kuoza.Kitabu kikazua taharuki.
-jumlisha na hotuba mbalimbali za kuasa na kujuta.
Kazi ikabaki kwetu kusuka twende kilioni au butus!
Kuna msemo unasema 'huwezi kutumia akili iliyosababisha tatizo kutatua tatizo'..haishangazi kuona kwamba hakuona tatizo kwenye ujamaa wake,ujamaa kwake ulikua dini,alichukia sana mtu kuwa tajiri
 
Ni hivi kusema wafe watu ndio legacy yake ipotee sio kitu cha siku mbili tatu. Pengine generation kadhaa nyingine. Wewe na mimi tutalikosa hilo boti.
The roots are so deep. It requires same level of thinking to uproot them
Moja ya vitu alivyofanikiwa Nyerere ni kutufanya Watanzania kuwa mandondocha wa kufikiri yeye ni kiumbe wa kipekee ambaye alikuwa sahihi kwa kila jambo alilofanya! Kuna watu wanamuona yeye ni zaidi ya Mungu!
 
Binafsi namkubali mwamba Kuibadili nchi kutoka umasikini wa 0 ni kazi ngumu sana , Laiti angekata tamaa Tusingekua hapa..

Watu hawakua na elimu ya kutosha, Serikali haina akiba yeyote, Watu walikua na Mindset ya kusaidiwa na serikali...

Alipata tabu sana mwalimu
Sasa kwann alilazimisha tupate uhuru wakt bado tulikuwa hatuna uwezo kujiongoza
 
Back
Top Bottom