Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

NNyie
Mada inafikirisha kiaina ila the fact I know ni kwamba mwalimu himself alikuwa ana uwezo sana as a person sasa kuhusu kutokuwa na uwezo wa kuiongoza nchi mh labda Nisikilize maoni ya wadau kwanza
Nyie vijana wa sasa hivi hamuwezi kujua umaskini watu waliopitia waulize wakubwa zako
 
umekula ubwabwa mwingi halafu ukenda kulala na kuota hayo maisha mazuri ya Nyerere.
Kitu kimoja kinachowapiga chenga watu wengi hasa waliozaliwa kuanzia 1980 wanadhani maisha mazuri yanaletwa na vitu vingi vya anasa anasa kama vilivyopo sasa 🤣

Kumbe ni tofauti kabisa !
Maisha mazuri kwanza yanaletwa na Afya yako ikiwa nzuri, pili uwe na peace of mind , na tatu uwe na kazi ya halali ya kukuingizia kipato 🙌🙏

Vyote hivyo vilikuwepo Enzi zile ndio maana hatujawahi kulima na kutumia makemikali mnayoyaita Mbolea kwenye Mashamba yetu !

Leo hii mnakula makapi yaliyowekewa kemikali hata harufu ya wali au Ugali huwezi kuusikia wakati Chakula kinapikwa !

Leo watu wana Stress mpaka kwenye kope 😂😅🤦🏽‍♂️
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukali, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni inchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Ungethubutu kuongea haya awamu yake uone kama ungeishu Hadi leo
 
Mwaka 1973/74 kulikuwa na upungufu mkubwa wa chakula; si kwa sababu ya siasa za wakati huo, bali hali ya mazingira ilikuwa ngumu kote duniani na haikuwa Tanzania pekee.
Baadhi ya lawama dhidi ya Nyerere huwa zinalazimishwa na baadhi ya watu kwa misukumo binafsi au sababu za kidini.
Miaka hiyo njaa ilipiga sehemu kubwa ya Eastern Africa kutokana na ukame na pia uchumi kuyumbishwa na OPEC. Ila kwa Tanzania wabaya wake wanakomalia suala ujamaa villagisation.
 
Kwani lilibka yingo kalisema?

Mimi nilikuepo, tena huyo hajaelezea waliokua wanapotea. Au walipotezwa?
. Wengine tunashukuru tulikua nabuwezo wa kuikimbia nchi.
Kuikimbia nchi, ndiyo maana ukaishia kuwa kama ulivyo, kwani wewe huoni jinsi ulivyo athirika kimaisha?
Mimi nilikuepo, tena huyo hajaelezea waliokua wanapotea. Au walipotezwa?
Sasa kama ulikimbia nchi, halafu "ukawepo" huoni ulivyo changanyikiwa na maisha yako hayo ya ulevi? Kati yako wewe, na Ali Hassan Mwinyi, ni nani aliyeweza kueleza hao unaosema "walipotezwa"?

Kwani lilibka yingo kalisema?
[/QUOTE]
Dalili za kuathirika tayari ndizo hizi. Jitahidi kutafuta msaada wa kupoza haya mambo bado ungali na uhai.
 
Baadhi ya lawama dhidi ya Nyerere huwa zinalazimishwa na baadhi ya watu kwa misukumo binafsi au sababu za kidini.
Miaka hiyo njaa ilipiga sehemu kubwa ya Eastern Africa kutokana na ukame na pia uchumi kuyumbishwa na OPEC. Ila kwa Tanzania wabaya wake wanakomalia suala ujamaa villagisation.
Miaka yote hii hawa watu wame fanya kila kitu uongozi wa Mwalimu Nyerere uonekane kuwa mbaya bila ya mafanikio yoyote.
Wengi wa hawa wanasukumwa na imani zao za kidini kama ulivyo sema; na chimbuko la hili ni tokea huko mwanzo kabisa baada ya kupata uhuru. Bila kutumia umakini mkubwa wakati huo, nchi hii ingejikuta katika matatizo ya udini mapema zaidi. Lakini naona taratibu tunaelekea huko huko kama tutaendelea na mwendo tulio nao sasa hivi.
 
Mwaka 1973/74 kulikuwa na upungufu mkubwa wa chakula; si kwa sababu ya siasa za wakati huo, bali hali ya mazingira ilikuwa ngumu kote duniani na haikuwa Tanzania pekee.
Kabisa kabisa !
Hao watoto wa miaka ya hivi karibuni wamekaririshwa vitu ambavyo vimetengenezwa na maadui wa Nyerere.
Sisi wengine hatujakaririshwa bali tulikuwepo miaka yote ya Utawala wake !!
 
Mwaka 1973/74 kulikuwa na upungufu mkubwa wa chakula; si kwa sababu ya siasa za wakati huo, bali hali ya mazingira ilikuwa ngumu kote duniani na haikuwa Tanzania pekee.
upungufu mkubwa wa chakula uliletwa na kuhamisha watu kiholela na kuwapeleka kwenye vijiji vya ujamaa kwenye maeneo mapya. Watu walihamishwa kutoka makao yao ya asili na kupelekwa maporini kwa hivyo msimu uliwapita wa kilimo kwani walichelewa kutayarisha mashamba. Hali ya ukame ndiyo ikakolezea umasikini.

Rev. C. K. Omari aliandika kitabu na kufafanua vizuri sana kuhusu janga hilo la ujamaa. Nadhani alikuwa lecturer pale UDSM kama sikosei.
 
Ni sababu iliyo changia, siyo sababu pekee; na hakuna mtu aliye kuwa amepanga itokee hivyo. Watu kuhama ilikuwa ime pangwa hivyo bila kuwa na ufahamu wa kitakacho tokea na hali ya hewa.
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukali, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni inchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Umasikini unasabishwa na akili alizo nazo mtu(binadamu), swali fikirishi je mwalimu Nyerere ndiye aliwambia wazazi wako wakuzae na kukulea kimasikini, wenzako walio zaliwa miaka hiyo ni matajiri, kwasasa una miaka 54
 
Umasikini unasanishwa na akili alizo nazo mtu(binadamu), swali fikirishi je mwalimu Nyerere ndiye aliwambia wazazi wako wakuzae na kulea kimasikini, wenzako walio zaliwa miaka hiyo ni matajiri, kwasasa una miaka 54
Ulishawahi kusikia kama wazazi wetu walikuwa wanakatwa mishahara yao kwa ajili ya kusaidia vya vya ukombozi inchini mwao,mfano Flerimo,A.N.C Swapo na vingine.
Umeshawahi kubahatika kwenda inchi mojawapo ya hizo,halafu fananisha maisha ya watu wake na sisi tuliokuwa tunawasaidi kama yanafanana,
 
South Africa nimeenda hata Zimbabwe nilienda South Africa nilienda 1990 Pretoria, 1991 JB, 1991 Zimbabwe- burawayo and Harare, niliobahatika kuona mashamba makubwa sana ya mabeberu, hata kwenye siasa tulikaririshwa kwamba Tanzania haiwezi kuwa huru kama nchi nyingine za Afrika hazija pata uhuru, kwenda shule, (sekondari), kupanda mabus tulikuwa tunatumia makaratasi yaani waranti lifti tulikuwa hatutoi nauli, what is your base of you're questions in reality though not all citizens can enjoy the national cake, kila kitu, (mtu), na zama zake siyo wananchi wote huwa wanafaidi keki ya taifa
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukali, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni inchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Chuki binafsi itakumaliza. Walaumu wazazi wako kwa umaskini na siyo mwl nyerere.
 
Back
Top Bottom