Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Hakuna aliyewaharibia maisha wazanzibar. Ni wenyewe. Nani huyo mtaje ili dunia ikucheke? Shida yetu kubwa hatutaki kukubali tunawajibika kwa madhira yetu wenyewe. Kila tatizo tunasukumia watu wengine. Baada ya mapinduzi, ilikuwa dhahiri yangetokea mapinduzi mengine tena sio muda mrefu. Na hali ya usalama wakati ule, ilikuwa inaangaliwa kwa dhana ya ubepari au ukomunisti.
Je Zanzibar, iligawanyikaje katika hayo makundi mawili? Kina babu na wenzake walishakuwa wakomunisti. Na walikuwa peke yao au wakubwa wengine? Je Mzee Karume alikuwa upande gani? Mwarabu aliyepinduliwa?
Nani aliyeomba kuunganisha nchi na kwa maslahi ya nani? Mambo ya maisha hayana nafasi kwa watu vigeugeu.
Ukigeuka nyuma ukakatataa maneno yako mwenyewe uliyoyasema kwa mdomo wako, unakuwa mnara wa chumvi
Tuongee ukweli kutoka moyoni,kinachowaunganisha watu kutoka moyoni ni Dini,Uisilamu Kwa Zanzibar ulikuwa zaidi ya asilimia tisini na tisa Wazanzinar walikuwa au wako Dini moja,walikuwa wanaswali pamoja,ni ngumu watu hawa kuchinjina,kuna mtu tena wa dini nyingine aliyeenda kuwatia uchonganishi
 
U
Nyerere last time alikuwa Raisi wa Tanzania almost 40 years ago, leo bado mnafikiri shida zenu ni Nyerere, at least shukuru hakutuachia vita kama haya matekaji ya siku hizi yanapotupeleka, na Kwa msio jua Nyerere alikuwa ahead of his time, yeye ndio alipigania nchi iwe na vyama vingi huku CCM aliyoianzishia walikuwa wanatutisha vyama vingi vitaleta vita, Nyerere nakubali sera zake za uchumi zilituletea umaskini lakini alionekana kubadilika mwishoni, alikuwa mtu wa haki na hakuwahi na Tamaa, alikufa maskini kabisa, na ingekuwa anaishi Nina uhakika asingekubaliana na siasa za CCM za wizi wa kura, kubambikia kesi, utekaji au kuuza maliasiri za nchi. He was a good man
Unawajua idadi ya watu waliotiwa kizuizini na nyerere,tena wengine wakakimbia inchi,ni kubwa kuliko marais wote waliokuja baada yake
 
1. Ukame
2. Njaa kubwa kuwai kutokea mpaka tukala ugali wa njano
3. Pressure kutoka nchi za maghalibi na taasisi za fedha za kimataifa
4. Vita ya Kagera shughuli zote za uzalishaji nikama zilisimama.
5. Kulipuka kwa gonjwa la ukimwi.
Hzo mbanga zilimpeleka mzee puta hakaona yeye hawezi kukubali masharti ya nchi za maghalibi ikabidi angatuke.
Ile vita ya Kagera ilikuwa inatumia dola nyingi sana za kimarekani kwa siku? Kumbuka Tz ilikuwa haitengenezi silaha nyingi za kivita, vyote hivyo vilinunuliwa kwa pesa za Kigeni . Naona wachumi wengi hawajadadavua kwa kina athari ya ile vita kwa uchumi wa Tz. ambao uliporomoka sana baada ya vita. Vile vile nidhamu za utendaji kazi maofisini na mashirika ya umma uliporomoka sana , na wizi wa mali ya Umma ukaota mizizi.
 
Wewe Unasema umezaliwa miaka ya sabini halafu Unasema kulikuwa hakuna nguo na kwamba watu walikuwa wanavaa magunia 😂😅

Mimi nimezaliwa miaka ya Hamsini lakini sikuwahi kuona watu wakivaa magunia 🤣

Na pia vyakula tulikuwa tunakula mpaka tunasaza 😀😅

Maisha yalikuwa ya raha sana ndio maana ukaona hata Wacongomani wengi walihamia huku Tanzania kuja kupiga muziki !

Maisha yalikuwa mazuri sana asikudanganye mtu !

Sasa hivi maisha ni magumu kuliko ilivyokuwa Enzi zile !
Kama wapo Wazazi wako waulize !
Wewe usingeweza kujua maisha yakoje maana miaka hiyo ya 70 ndio kwanza Umezaliwa !😅🙌🙏👍
Daah, umenifurahisha sana sana na kunikumbusha mbali sana.

Mimi baby yangu alikua ni mkulima wa zao fulani la biashara kule kijijini .
Wakati wa Likizo tulikua tunakwenda kukaa kwa Babu .
Tulikua tunakutana wajukuu zaidi ya 15. Lakini tulikua tunakula chakula na kusaza. Unalazimishwa kula . Kuku wananchi kwa wawili . Kila kitu kilikuwepo na Jumapili wote tunapewa sadaka na babu ya kutoa Kanisani.
mwezi mzima wa likizo ni kama sherehe. Ila kazi kazi tu. Babu akafariki akiwa na zaidi ya miaka 90. Babu alikua na watoto 10 kwa mke mmoja. Mtoto wake wa Kwanza aligraduate Makerere University, na wengine wakiwa wafanya biashara lakini wote walisoma na kupata elimu yenye manufaa kwao.

Babu alikua anaamka mapema sana na kwenda shambani na kila mtu alipangiwa kazi ya kufanya na jioni alikua anakwenda kupiga mitungi yake. Alikua na elimu ya Darasa la nne lakini aliyamudu maisha kisawasawa.

Leo vijana walioko kijiji kile kile ni ombaomba na hakuna tena zao lile la biashara. Wenye hela kidogo ni boda boda na hawawezi hata kuoa na kuishi na mke na hata watoto wawili .

Mwalimu alijenga ujamaa na watu kujitegemea ndio maana Tanzania wananchi hawategemei serikali iwaletee chakula , malazi na hata mavazi.
Wezi wanahalalisha wizi wao kwa kumtukana Nyerere.

Mpaka leo hua najiuliza mbona maisha yale ya kiafrika yalikua mazuri na ya furaha sana .

Wewe Unasema umezaliwa miaka ya sabini halafu Unasema kulikuwa hakuna nguo na kwamba watu walikuwa wanavaa magunia 😂😅

Mimi nimezaliwa miaka ya Hamsini lakini sikuwahi kuona watu wakivaa magunia 🤣

Na pia vyakula tulikuwa tunakula mpaka tunasaza 😀😅

Maisha yalikuwa ya raha sana ndio maana ukaona hata Wacongomani wengi walihamia huku Tanzania kuja kupiga muziki !

Maisha yalikuwa mazuri sana asikudanganye mtu !

Sasa hivi maisha ni magumu kuliko ilivyokuwa Enzi zile !
Kama wapo Wazazi wako waulize !
Wewe usingeweza kujua maisha yakoje maana miaka hiyo ya 70 ndio kwanza Umezaliwa !😅🙌🙏👍
 
U

Unawajua idadi ya watu waliotiwa kizuizini na nyerere,tena wengine wakakimbia inchi,ni kubwa kuliko marais wote waliokuja baada yake

Walitaka kupindua nchi live na kusababisha uasi kwa kufadhiliwa na hawa mnaowarudisha leo kuja kuchukua rasilimali alizokuwa amazitaifisha .

Hebu mkae mtafakari kuwa ingekuaje kama kila kitu kingebaki mikononi mwa Wazungu ,waarabu na wahindi?
Tungekua na uhuru gani ?
Yaani mpaka ikulu ilikua ni mali ya wazungu ,majaji wote walikua ni wazungu , Askari wote wenye vyeo walikua ni wazungu. Nyumba zote zinazomilikiwa leo na NHC zilikua za waarabu na Wahindi na wao ndio walikua wanafanya biashara kwenye nyumba zao katikati ya miji yote nchini . Maeneo yote ya Ofisi za wakuu wa Wilaya kama BOMAN ni maeneo ya Wazungu na n
 
U

Unawajua idadi ya watu waliotiwa kizuizini na nyerere,tena wengine wakakimbia inchi,ni kubwa kuliko marais wote waliokuja baada yake

Walitaka kupindua nchi live na kusababisha uasi kwa kufadhiliwa na hawa mnaowarudisha leo kuja kuchukua rasilimali alizokuwa amazitaifisha .

Hebu mkae mtafakari kuwa ingekuaje kama kila kitu kingebaki mikononi mwa Wazungu ,waarabu na wahindi?
Tungekua na uhuru gani ?
Yaani mpaka ikulu ilikua ni mali ya wazungu ,majaji wote walikua ni wazungu , Askari wote wenye vyeo walikua ni wazungu. Nyumba zote zinazomilikiwa leo na NHC zilikua za waarabu na Wahindi na wao ndio walikua wanafanya biashara kwenye nyumba zao katikati ya miji yote nchini . Maeneo yote ya Ofisi za wakuu wa Wilaya kama BOMAN ni maeneo ya Wazungu na neno la Waingereza . Mashamba yote ya Korosho,pamba, Mkonge, Korosho, Chai,Tumbaku, Zabibu, Maaple ,Minazi , Machungwa ,Misufi, Maembe , Shahiri, ngano, mahindi na maharage kule Arusha n. k yote yalikua ya wazungu . Waafrika hawakua hata na maeneo ya kujenga zaidi ya kuishi kota za wazungu na kuwa vibarua . Mapori yote yalikua ni mali ya serikali .
Tanganyika haikua na viwanda vingi wakati wa Mkoloni kwa sababu viwanda vingi vilikuwa Kenya na Zimbabwe . Tanganyika ilikua ni sehemu ya kuchota mali ghafi.

Mtume na Nabii Mtakatifu Julius Kambarage Nyerere Nabii wa Afrika na Mzalendo alitaifisha Mali zote na ardhi za Mashetani waliokuja kuwaua waafrika na kutwaa rasilimali zao walizoumbiwa na Mungu kwa ajili ya vizazi vyao wakiwemo Wamasai Waliofukuzwa na Waarabu koko toka Misri kwenye bara la Mtu mweusi . Na leo Waarabu wale wale wamewafata tena kule Loliondo kwa mgongo wa mjukuu wao mwarabu koko.

Nyerere akajenga viwanda vingi sana ili kutumia malighafi zetu wenyewe kuzalidha. Tulizalisha nguo na nyuzi kwa pamba zetu wenyewe . Tulikua na viwanda vya mafuta ya Karanga leo hata ukimwambia Abadili kuwa tulikua na mafuta ya Karanga ,tan band badala ya Blue band ya Kenya hajui ,anachojua ni kuagiza makontena ya mafuta kutoka Indonesia na China basi na kutangaza kuwa watanganyika hawawezi kuzalisha vitu vyao . Kanga za urafiki zilikua ni bora sana zikishindana na kanga za Kenya.

Kwa hali ilivyokuwa Chuki ya wale walionyanganywa mali zao ilikua ni kubwa sana kwa Nyerere. Na Ukumbukwe hakua ni Mwanajeshi bali Raia lakini Mzalendo kama Mwanajeshi ,Hali iliyopelekea kuwa na majaribio mengi ya kumpindua lakini kutokana na uzalendo wa Watanganyika waliokua wanampenda Rais wao majaribio yote yalishindikana. Hujuma za kiuchumi ziliendelea zaidi baada ya Kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti. Nyerere akasoma alama za Nyakati za Mfumo wa Vyama vingi na jinsi nguvu ya Mataifa makubwa inavyotumika kutumia pesa kuleta vita na uasi kwenye nchi za Afrika kushinikiza vyama vingi. Nyerere hakutaka kuwa rais wa Nchi ya Kibepari mana yeye na chama chake hakuamini katika unyama wa mabeberu na dhulma za nchi za Kibepari. Akaamua kung'atuka madarakani.

Kilichofuata ni Wale wale waliokua wanatamani maisha ya anasa kuanza kujipanga kupitia Demokrasia ili wakamate na kuifanya mali yao wakiwemo vijana walipoenda siasa za kujilimbikizia mali kwa kukwapua mali za umma. Walijimilikisha mpaka nyumba ambazo hata Wakoloni hawakuzifanya mali binafsi. Waliuza mapaka nyumba za Polisi ,mahakama,TISS n.k. na kuzifanya mali zao na familia zao na marafiki zao.
Wakajiwekea sheria za mafao na mishahara mikubwa na marupurupu makubwa bila kujali hali ya uchumi wa nchi. Wakabadilisha utamaduni wetu wa kuitana Ndugu na kutunga sheria ya kuitwa Mheshimiwa. Wanajiona wao sio ndugu zetu bali waheshimiwa na kuanza kujiona kama wazungu weusi mbaya zaidi wakawa wabaya zaidi ya wakoloni chini ya mifumo kinyama ya Kibepari.

Tujiulize,
Tulikua watu milion 14 maji bure , umeme ni Mita madeni kibao.
Elimu bure vitabu vimejaa librari tunapewa mpaka madaftari na penseli.
Matibabu bure .
Wafanyabiashara wachache .
Simu madeni kibao.
posta madeni kibao.
Benki kubwa mja NBC .
Wafanyakazi kama walimu walikua na maisha mazuri na shule za serikali zilikua za bweni zikiwakutanisha wanafunzi kutoka kila sehemu alimradi awe amefaulu kwa ufaulu wa Juu.
Bado vita ya Uganda ikaibuka, vita za Nchi za kusini ambazo zilikua zinatokana na waafrika wenzetu kudai uhuru hivyo Tanganyika ikawa ndiyo mfadhili na msaada mkubwa kwao kijeshi.
Kama sio uzalendo Mwalimu angewezaje kujenga viwanda na mashirika ya umma zaidi ya 360 kwa mazingira kama hayo ?

Leo hii , Tuko mil.65 tozo kila mahali. Watalii kibao,mabilionea wa ndani kibao, Wafanyabiashara kibao.
Majengo yanayolipa kodi ya majengo na ardhi ni mengi nchi nzima.
Bandari inapitisha mizigo ya ndani na nje mara mia moja zaidi ya kipindi cha Mwalimu.
Wafanyakazi wanadhulumiwa pesa zao za pension kwa sababu tu ya ubinafsi wa Mabepari kuanzisha miradi ya kifisadi na wao kuwa mabilionea huku watumishi wakibaki kuwa fukara. Badala ya kuwapiga kitanzi wezi kwenye mifuko ya jamii ya wafanyakazi kama NSSF wanaopigiwa mabomu na risasi ni wale wanaodai mafao yao ambayo yamegeuzwa kuwa dili la watu kupiga pesa kwa kujenga majengo yasiyo na tija kwa wafanyakazi zaidi ya Watu wachache kupiga dili.
Wakaja watawala walimfuata Nyerere wakaungana na wapiga dili kujilimbikizia mali huku wakiwateua marafiki zao kusimamia mashirika ya umma kwa lengo la kupeana fadhila na sio kuendeleza mashirika . Bodi za mashirika za kumwaga lakini wamewekwa Makada na marafiki ili wachote pesa za kampeni kurudishana madarakani na kuendelea kutafuna nchi.

Wengine sasa wanakuja na marafiki zao wakijifanya ni wawekezaji kumba ni wao na kujimilikisha mpaka bandari na kila sehemu yenye kukusanya pesa tu. Hawataki kujenga viwanda bali kuanzisha makampuni ya kushika tenda za serikali kuchota pesa . Hawajengi kiwanda cha Sukari na Mbolea ,hapana wanataka kutengeneza vikampuni vya kuingiza sukari bila Kodi halafu wanauza kwa bei ya juu wapige pesa .

Hawa kamwe hawatamsifia Mwalimu zaidi ya kuwasifia wale waliowaruhusu na kuwawekea mazingira mazuri ya kuigeuza nchi kuwa shamba la wageni wao.

Wengine waliambiwa huyu Mzee akiendelea kuwa Hai wewe huwezi kuwa Rais kamwe .

Mwalimu akaondoka akiwa mzima kwenda check akarudi akiwa paradiso. Nini kilitokea bado hakijawekwa wazi kabisa kiuchunguzi na hakijachunguzwa.

R.I.P.Mwalimu JKN.
Shujaa wa nchi za Kusini Mwa Afrika na wengine leo wanapata fursa ya kupiga picha kwenye vikao vikubwa duniani kwa mgongo wako .
Shukrani ya Punda ni Mateke
 
It's very obvious Nchi Ilimshinda ikamlazimu kutoka tu madarakani
Mkuu both ways,ila mwanzo alianza vizuri.Kulikuwa na law and order ilioachwa na wakoloni.
Lakini taratibu nchi ikatoka kwenye mstali.
Lakini wafadhili wakuu wa maendeleo siku hizo walikuwa nchi za magharibi na pia nchi za mashariki kila upande ukivutia upande wake.
Baada ya vita vya Kagera ndio wafadhili wa nchi za magharibi walimtolea uvivu akina Raisi Reagan wa Marekani na Waziri Mkuu Margaret Thatcher wa Uingereza.
Walikata misaada ya maendeleo, nchi ikashindwa kukopesheka na taasisi za fedha,nchi iliyumba sana lakini wananchi waliongeza mshikamano licha ya ugumu wa maisha.
Kuna incidences nyingi za kutaka kumpindua zilianza kujitokeza lakini hakubadirisha msimamo wake akisema hawezi kugeuka jiwe hadi anastaafu.
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukari, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni nchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Mwalimu alikosea sehemu mbili...1.UJAMAA NA UTAIFISHAJI ULIOPELEKEA LAANA KUBWA 2. VITA YA UGANDA ILIYOTULETEA UMASIKINI
 
Unajua aliyewaharibia Wazanzibar Maisha?mpaka leo hii hakuna amani hasa kipindi cha uchaguzi sababu yake ni yeye na kila mwaka wapinzani wanashinda,hata mapinduzi yenyewe hayakufanywa na wazanzibar bali wamakonde walipitia Tanga kwenda Zanzibar na kufanya huo unyama wa mauaji kwa faida ya nani,yupo anayejua

Leo hii Zanzibar bila mapinduzi ingekuwa mbali sana kiuchumi tofauti na Tanganyika,
Akili za kushikiwa hizi.
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukari, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni nchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Wewe ni mtu mzima lakini huna akili hata kidogo. Nyerere alikuwa binadamu kama binadamu yeyote na sio malaika lakini J.K Nyerere alifanya jitahada kubwa sana kuivusha Tanzania katika kipindi ambacho teknolojia ilikuwa duni, umasikini mkubwa na wimbi la Ujinga na maradhi.. Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi katu kubeza jitihada za Mwl Nyerere.. Hakika alikuwa mtu muungwana sana na mwenye maono yasiyo mithilika.
 
Daah, umenifurahisha sana sana na kunikumbusha mbali sana.

Mimi baby yangu alikua ni mkulima wa zao fulani la biashara kule kijijini .
Wakati wa Likizo tulikua tunakwenda kukaa kwa Babu .
Tulikua tunakutana wajukuu zaidi ya 15. Lakini tulikua tunakula chakula na kusaza. Unalazimishwa kula . Kuku wananchi kwa wawili . Kila kitu kilikuwepo na Jumapili wote tunapewa sadaka na babu ya kutoa Kanisani.
mwezi mzima wa likizo ni kama sherehe. Ila kazi kazi tu. Babu akafariki akiwa na zaidi ya miaka 90. Babu alikua na watoto 10 kwa mke mmoja. Mtoto wake wa Kwanza aligraduate Makerere University, na wengine wakiwa wafanya biashara lakini wote walisoma na kupata elimu yenye manufaa kwao.

Babu alikua anaamka mapema sana na kwenda shambani na kila mtu alipangiwa kazi ya kufanya na jioni alikua anakwenda kupiga mitungi yake. Alikua na elimu ya Darasa la nne lakini aliyamudu maisha kisawasawa.

Leo vijana walioko kijiji kile kile ni ombaomba na hakuna tena zao lile la biashara. Wenye hela kidogo ni boda boda na hawawezi hata kuoa na kuishi na mke na hata watoto wawili .

Mwalimu alijenga ujamaa na watu kujitegemea ndio maana Tanzania wananchi hawategemei serikali iwaletee chakula , malazi na hata mavazi.
Wezi wanahalalisha wizi wao kwa kumtukana Nyerere.

Mpaka leo hua najiuliza mbona maisha yale ya kiafrika yalikua mazuri na ya furaha sana .
Umemaliza kila kitu !
Ni kweli yale majizi ya mali za Nchi ndiyo yanayomtukana Mwalimu !

Mimi nina Rafiki yangu tulisoma pamoja na kuishi pamoja kijijini
Hivi sasa yupo nje ya Nchi alishahamia huko kitambo sana, lakini kila tunapopata kuongea ni lazima tutakumbushana maisha yale yalivyokuwa mazuri japo yalikuwa very simple life !

Wamuache Mwalimu apumzike kwa Amani , Mwalimu was Genius ,
Mwalimu aliipenda Nchi yake na aliwapenda Wananchi wake ,

Tulisoma bure mpaka madaftari vitabu na kalamu tulipewa bure na tulitibiwa bure na tulipewa warrant za Serikali kwa ajili ya kusafiri kutoka Nyumbani kwenda Shule tulizopangiwa!

Mpaka Chakula tulikula bure mashuleni !
Majizi ya mali za Umma hayawezi kumsema vizuri Mwalimu hata siku moja !
 
Kuna msemo unasema 'huwezi kutumia akili iliyosababisha tatizo kutatua tatizo'..haishangazi kuona kwamba hakuona tatizo kwenye ujamaa wake,ujamaa kwake ulikua dini,alichukia sana mtu kuwa tajiri
Hakuuchukia utajiri kama utajiri aliiona jamii yetu kwa wakati ile ikiwa bado ipo nyuma sana kielimu na katika masuala mengi hivyo ujamaa ulikuwa na lengo la kuepuka uwepo wa matajiri wachache sana miongoni mwa maskini wengi sana.

Mwalimu hakuwa malaika lakini alijaliwa na Mungu maono makubwa, aliziona hizi hulka zilizokuja kuichafua haswa awamu ya nne na kuendelea. Kwamba angeruhusu uwepo wa matajiri miaka ile hao wachache wenye elimu wangewaumiza wengi wasio na watetezi.

Alikwepa misuguano ya kitabaka ambayo ingeweza kuzaliwa kwa kuruhusu wachache wawe na nguvu na wengi wakose mtetezi.

Alisambaza elimu ili iwe silaha ya mtoto wa mkulima kuweza kuitumia katika vita za kimaisha.

Anaweza kulaumiwa pia kwa kuleta ujamaa kwani huwa hauruhusu ubunifu wa mtu mmoja mmoja na unatengeneza wajinga wengi.
 
Wewe ni mtu mzima lakini huna akili hata kidogo. Nyerere alikuwa binadamu kama binadamu yeyote na sio malaika lakini J.K Nyerere alifanya jitahada kubwa sana kuivusha Tanzania katika kipindi ambacho teknolojia ilikuwa duni, umasikini mkubwa na wimbi la Ujinga na maradhi.. Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi katu kubeza jitihada za Mwl Nyerere.. Hakika alikuwa mtu muungwana sana na mwenye maono yasiyo mithilika.
Nyerere aliacha viwanda kila mkoa tena vile vikubwa.. MWATEX, MUTEX, General Tyre na vingine vingi tu, nani alikuja kuviua?.

Alijenga msingi wa kila mtu kwenda shuleni na kupata elimu tena bure kabisa, tunamlaumu Nyerere kwa kumuonea, kuna mengi ya kijinga yamefanyika baada ya mwaka 1985 akiwa ameshatoka ikulu.
 
Mkuu both ways,ila mwanzo alianza vizuri.Kulikuwa na law and order ilioachwa na wakoloni.
Lakini taratibu nchi ikatoka kwenye mstali.
Lakini wafadhili wakuu wa maendeleo siku hizo walikuwa nchi za magharibi na pia nchi za mashariki kila upande ukivutia upande wake.
Baada ya vita vya Kagera ndio wafadhili wa nchi za magharibi walimtolea uvivu akina Raisi Reagan wa Marekani na Waziri Mkuu Margaret Thatcher wa Uingereza.
Walikata misaada ya maendeleo, nchi ikashindwa kukopesheka na taasisi za fedha,nchi iliyumba sana lakini wananchi waliongeza mshikamano licha ya ugumu wa maisha.
Kuna incidences nyingi za kutaka kumpindua zilianza kujitokeza lakini hakubadirisha msimamo wake akisema hawezi kugeuka jiwe hadi anastaafu.
Unajua sababu ya Nchi kutokukopesheka??
Kwanza Mwalimu alikataa madini yasichimbwe kama Serikali haitapata asilimia 50 ya mapato yatakayo patikana ! = Waliokuja wajanja baada yake wakaruhusu mikataba ikatiwa saini Serikali ikawa inapewa asilimia 3 % ya mapato yanayo patikana kwenye dhahabu 😱 !

Nchi ilishindwa kukopesheka kwa sababu Nchi ilikuwa na deni la Dollar billion 8 inasemekana !
Mabepari lengo lao ilikuwa wakubaliwe kuchimba madini kwa bei Chee waliyokuwa wanataka wao !
Na pia walilazimisha ili Nchi iweze kukopeshwa na IMF ni lazima Mwalimu akubali thamani ya pesa ya Tanzania ishushwe !

Yote hiyo ilikuwa ni kumkomoa Mwalimu kwa sababu ya kwanza kuzisaidia Nchi nyingi za kusini mwa Africa kudai na kisha kupata Uhuru wao,
Tulikuwa tukibadili dolla ya marekani kwa shs 5 za Tanganyika na baadaye za Tanzania !

Mwalimu alifanyiwa hujuma na Mabeberu kwa sababu ya misimamo yake ya kukataa kunyonywa Rasilmali za Nchi !!
Weka Hiyo Akilini Mkuu 🙏👍
 
Wanaomlaumu Nyerere bila ya kujua mengi ya wakati ule wengi ni vijana wadogo ambao wakati wa awamu yake walikuwa aidha hawajazaliwa au watoto chini ya miaka kumi, ambao bado hawajaanza kusikiliza taarifa za habari na kuelewa nini anachokisema mtangazaji..
 
Miaka yote hii umekuwa mtu mzima; na sijui kama hata shule ulikwenda, bado hata akili ya kutafuta taarifa mwenyewe huna?
Unaeleza umezaliwa miaka ya 1970. Sasa wewe kama mtoto hayo mambo uliyajuaje?
Tueleze ulipata utapia mlo ndiyo maana akili yako ikadumaa kiasi hiki?

Ni waTanzania wangapi walikufa njaa wakati huo, unajuwa? Je, Ethiopia na hapo Kenya, nako Nyerere aliwanyima chakula watu wa huko waliokuwa wakifa kwa njaa?
Naona mfuasi wa Nyerere, mada imekupiga kwenye mshono, sasa kama uko Ethiopia na Kenya walitaabika ndio halali na sisi tutaabike.

Kuna ajenda ya siri nyuma ya kutukuzwa sana kwa Nyerere, lakini ukiangalia hali ilivyokua kipindi chake mfano umasikini nankushughulikiwa kwa walipishana nae mawazo kama Oscar Kambona.

Ukiangalia current consenquencies za maamuzi yake mfano kuto-review katiba licha ya kuona imempa Rais umungu mtu utagundua teacher hakuwa na maajabu kama anavyotukuzwa.
 
Back
Top Bottom