Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Izo hujuma hata mabeberu wenyewe kwa wenyewe wanafanyiana, na jukumu la kiongozi ni kuzi-outsmart izo hujuma.
 
Maajabu yake ni kutembea nchi nzima miaka ile barabara zote ni vumbi tupu akitafuta uhuru wa Tanganyika, maajabu ni kuwa rais wa kwanza sawa na kina Sekou Toure, Jomo Kenyatta na waasisi wengi wa afrika.

Maajabu ni kujenga viwanda katika mikoa yote kwa lengo la kuinua uchumi, changamoto alizokutana nazo akiwa rais ni kubwa kwani miaka yake ilikuwa ni ya kujenga msingi wa kitaifa tofauti na marais waliyokuja baadae na kukuta misingi ipo tayari.
 
Ali- fail parefu, aliendesha nchi kwa kufuata misingi ya usawa wakati ata vitabu vya dini vinatambua matajiri na masikini na mpaka watumwa

Basically, aliendesha nchi kiimani zaidi na siyo kiualisia. Alizuia wapambanaji akawaita mabepari na mabeberu na akawa karibu na mediocre

NCHI ILIMSHINDA, HE WAS NAIVE
 
Uhuru wa nchi teacher alitangulizwa mbele na kanisa katoriki hakuupambania yeye mwenyewe kama jeshi la mtu mmoja.

Hizo changamoto alizokutana nazo ndizo kiongozi anatakiwa kuzitatua, hakuna excuses.

Mazuri alikua nayo mabaya alikua nayo, lakini kiujumla nchi ilimshinda ndio maana akaamua kung'atuka.
 
Alizijua hulka zetu za kuchukiana sisi kwa sisi, vitabu vya dini vinaandika maelezo ya jumla zaidi kuliko uhalisia wa afrika yetu.

Kuna umafia mwingi umefanyika na unaendelea kufanyika mfano pale wizara ya ardhi kuna makundi ya vijana wasomi wenye kutafuta pesa kwa njia za dhuluma za ardhi za watu. Ukiwa huna pesa utahangaishwa milele na hupati hati yako ukitoa milioni 10 mpaka 20 unapewa hati yako.

Ni mitandao ya wizi imeletwa na hulka zetu sisi wenyewe, Mwalimu kuja na sera za ujamaa ni kwa sababu alizijua hizi hulka kabla sisi hatujazaliwa, alifahamu kwamba bila ya elimu hakuna ukombozi kwa mtanzania wa kawaida.

Hivyo ujamaa ulikuwa na lengo la kuleta a level playing field, kuwa uwanja wa haki sawa kwa wote, na alifanikiwa mapema sana kwani bila ya kuwepo ujamaa kwa misingi yetu wenyewe sioni ni kwa namna gani haya yanayotokea Kenya leo hii yasingeweza kutokea hapa Tanzania.

Alihakikisha unyonyaji haustawi kwani unapokuwepo kunakuwa na taifa lenye uonevu unaokuja siku moja kulipuka na vifo vingi vinaweza kutokea.

Tunamlaumu kwa sababu hatukuwa ndani ya akili yake kwa wakati huo wa miaka ya kutafuta uhuru na mwanzo wa nchi iliyo uhuru.
 
Hoja mfu, alichukia watu kuwa matajiri, alitaka wote wafanane vipato, alisema mtu alipelekwa jangwani akae peke yake hawezi kuwa tajiri,ila atakua tajiri kwa kunyonya wengine, yaani mimi na familia yangu tufanye kazi kwa bidii,tukuze kipato,tupate mtaji,tuajiri watu na kuongeza uzalishaji hivyo kipato kiongezeke,uite huo unyonyaji!?.. hakuwa na maono yoyote
 
Changamoto za Tanzania ya 1964 sio za hii ya 2024, tunamhukumu Mwalimu kwa akili za 2024 bila ya kujua kwa kina zipi haswa ni changamoto za wakati ule.
 
Asingekuwa na maono leo hii tungekuwa sawa na Kenya katika lindi la vita na misuguano ya kijamii isiyokwisha.
 
Na wengine wamelishwa matango pori na wale waliokuwa wamebanwa na Mwalimu wakashindwa kufanya Ufisadi waliokuwa wakiutaka !
A.k.a wanyonyaji ! πŸ˜†πŸ˜€
 
Changamoto za Tanzania ya 1964 sio za hii ya 2024, tunamhukumu Mwalimu kwa akili za 2024 bila ya kujua kwa kina zipi haswa ni changamoto za wakati ule.
Changamoto ni ujinga, umasikini na maradhi,lakini hakujenga shule hata moja,na chuo kikuu kimoja,Ili kudhibiti watu wasisome, wakati huohuo kukata watu mishahara kuchangia harakati za ukombozi kusini mwa africa
 
Izo hujuma hata mabeberu wenyewe kwa wenyewe wanafanyiana, na jukumu la kiongozi ni kuzi-outsmart izo hujuma.
Alifanya mengi sana mazuri na aliacha mengi sana mazuri ila walipokuja wasomi wazuri wakabomoa kila kitu na kuuza kwa bei chee kila kitu kilichokuwepo!
Kuanzia Viwanda mpaka mashirika ya Umma !
Kama huvijui Viwanda na Mashirika ya Umma yaliyokuwepo basi wewe utakuwa ni kijana uliyedanganywa na Wanyonyaji wa Mali za Umma !
 
Kabisa kabisa ! πŸ™
 
Izo hujuma hata mabeberu wenyewe kwa wenyewe wanafanyiana, na jukumu la kiongozi ni kuzi-outsmart izo hujuma.
You are Right πŸ™Œ
Wajanja na wasomi wazuri waliofuata baada ya Mwalimu walifaulu sana juzi-outsmart hujuma za Wazungu kwa kuwaita hao hao Wazungu waje wachimbe Dhahabu kwa kutugawia asilimia 3 ya mapato ya dhahabu itakayouzwa. πŸ™„

Tukaviuza Viwanda vyote vilivyokuwepo kwa Ushauri na masharti ya IMF kwamba Serikali isifanye Biashara !
Kukaviuza Viwanda vyote kwa Bei ya Bure kabisa. πŸ™„

Kisha wakaja wajanja na wasomi Zaidi wakawa-outsmart tena Wakubwa kwa kuingia mikataba ya Uchimbaji wa Gesi ambayo Kiongozi mmoja akaja kutuambia kwamba pale tulishapigwa hatuna chetu πŸ˜³πŸ™„πŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈ

Kweli tumefanikiwa sana Kuwa-outsmart Wakubwa wa Dunia πŸ™ŒπŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈ
 
Uko sahihi kabisa. Binafsi nawaheshimu mno wazee kwa sababu hiyo. Kuna mzee fulani mitaa ya Ilala alikuwepo siku ya sherehe za uhuru huwa ananisimulia mno mikasa iliyotokea. Tatizo wazee wengi huwa kuna mambo wanaishia kuguna na kuelezea juu juu.
 
Hayo mambo yalikuja baada ya vita ya Kagera (tulifunga mikanda). Kabla ya hapo us dollar ilikuwa shilingi tano. Na ndiyo ilikuwa nauli ya uda (da

Wewe umeandika stori za kusoma vitabuni ambazo ziliandikwa kwa ajili ya kuwapamba Viongozi,Tofautisha viwanda alivyofitaifisha Nyerere na viwanda alivyovijenga. Ninachojua mimi baada ya Azimio la Arusha selikali ilitaifisha vitu vingi Sana, kumbuka hivi viwanda,makampuni zilikuwa na management zake,baada ya kutaifisha ilibidi waweke manegement za selikali ambazo watu wake hawana uzoefu taratibu zikaanza kupungua ufanisi mpaka kufa kabisa mfano kiwanda cha kusindika Nyama Tanganyika Pekers,kilikuwa kinaajiri zaidi ya wafanyaka 2000 kabla ya kupata uhuru na kilikuwa kinauza nyama iliyosindikwa inje ya inchi na kuiingizia Tanganyika pesa za kigeni,leo hii ni uwanjwa wa maombi,hapo wa kulaumiwa siyo Nyerere

Chukulia mfano mdogo South Afrika ya makaburu ilikuwa bora zaidi kuliko ya sasa,Nelson mandera hakuwa mjinga hakuna alichotaifisha kutoka kwa wazungu,lakini Mugambe alijikuta inaharibu uchumi wa Zimbabwe baada ya kutaifisha mashamba ya walowezi, kiuharisi aliyoyafanya Nyerere hayana tofauti na aliyoyafanya Mugabe
 
Mkuu kila jambo lina wakati wake,Hadi leo tuna chuma tena kwa wingi lakini hatuna fedha na tekinologia ya kuchimba na kuchakata,vivyo hivyo,Helium gas,Gesi asilia,mkaa wa mawe,nickel,Tin,Dhahabu,almasi,Tanzanite hadi hata phosphate tupo tupo.Hatujielewi kama leo tunajengewa hata vyumba vya madarasa na maliwato jiulize kama ilikuwa sahihi kuomba uhuru 1961.
 
Nitajie viwanda vilivyojengwa na Nyerere
 
Una ujinga mwingi bwana mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…