Kwa umri wako mimi binafsi nilitegemea ungejua kilichotokea kwanza kwa experience to na pili kwa kusoma vitabu.
1970, mi niko la saba, namaliza primari.
Maisha ya kula mkate kwa Kenya Butter ilikuwa kwa sana.
Gramaphone za Grundig, magari za peugeot, vitanda vya Vono na sofa za wahindi ndio yalikuwa maisha.
1967, Mwalimu alitaifisha njia kuu za uchumi, mabenki viwanda, makampuni kama Bima, etc.
Wazalendo wakapata ajira kiuongozi na kukaa na mameneja wazalendo.
Kuanzia 70s Mwalimu alijenga viwanda vingi sana, vya tumbaku, chai, nguo n.k., makampuni ya mabasi KAMATA. UDA,RETCO Regional Transpot Corporations kila mkoa makapuni ya kusaga mazao NMC,Makampuni ya biashara mkoa, RTC, mameneja wazalendo.
Management ya viwanda na makampuni miaka ya kati ya 70s ilikuwa si nzuri, wizi kwa wingi kwenye mashirika ya umma.
Mashirika yalikuwa hayana mwenyewe na yakaanza kuzalisha losses.
Lossess zilifidiwa na ruzuku (kodi za wananchi)
1978, Idi Amin ndo akaja malizia kabisa katika downward decline ya uchumi.
Magari, malori, chakula, vijana wenye nguvu, ununuzi wa silaha nzito nzito ndio vikaumaliza uchumi kabisa.
1979, tuliposhida vita Mwalimu alitamka wazi kuwa itachukua miezi 18 kurudisha uchumi katika hali yake ya kawaida. Wachumi walmdanganya Malimi, hata baada ya miaka 18 hali ya uchumi na kushuka kwa thamani ya fedha za Tanzania ikawa hali ndio mbaya sana.
Wakati huo huo watu wakazaliana kwa wingi kugawana kile kidogo kilichopo. Wakti wa uhuru tulikuwa milioni 9, sasa miaka ya 70 tuko mara mbili au zaidi kufika miaka ya 80, mara tatu na zaidi.
Kiukweli hatuwezi kumlaumu Mwalimu kwa downward slide ya uchumi kutokana na ukweli kuwa wazalishaji waliendelea kuwa wachache na midomo ya kula kama mtoa mada iliendelea kuwa mingi sana.
Waalendo walikuwepo tena walishiriki kuyaua mashirika ya umma, sasa umlaumu Mwalimu kwa lipi?