Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Ni wazee wapi hao?
Hata leo hii, pamoja na kwamba Mwalimu alikwisha fariki siku nyingi; ukipitisha kura kumshindanisha Samia na Nyerere katika uongozi, Samia haambulii kitu.
Mwinyi akiwa Rais alimwambia Mwalimu wewe Mwalimu ni mlima mimi Mwinyi ni Kichuguu tu
Kichuguu hakiwezi kushindana na Mlima 🙏🙏
 
Ngoja nikusahishe Kwanza,wewe ni kati ya wale waliosoma historia zilizopotoshwa, Ngoja nikupe historia ya Vita vya Tanzania na Uganda, Iddy Amini Dada alipompindua Miritoni Obote alikimbilia Tanzania kwa rafiki yake Nyerere,kwa kushirikiana na Yoweri Museveni na Obote walijaribu kurudi Uganda kwa mtutu wa bunduki wakitokea Tanzania ikashindika, wakafurushwa na majeshi ya Iddy Amini,
Baadaye kwa Sapoti ya jeshi la JKT bado ikashindikana,ndipo Amini akawafurusha mpaka kagera,ost yangu siijagusia hapo likaingilia jeshi la JWTZ, kuwafukuza ndani ya mipaka yetu
Sababu targeti ya Nyerere ilikuwa kumrudisha madarakani rafiki yake Obote ikabidi Vita viwe vya mda mrefu mpaka Arua kalibu na mpaka wa Sudan,

Sasa jiulize hivi Vita vilivyoharibu uchumi wa Tanzania vilikuwa na umuhimu wowote,Au mchokozi alikuwa Nyerere au Iddy Amini, maana yake Obote asingepinduliwa na Iddy Amini, hivi Vita visingetokea,na Iddy Amin hakuwa mjinga aanze tu kushambulia Tanzani,kwa nini hatukumshitaki kama tulivyoshambuliwa na Burundi wakatulipa fidia,msipende kusoma historia zilizopotoshwa na watu kwa maslai ya Viongozi

Na nimekushangaa kwa kusapoti Azimio la Arusha,ni kati ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere,na kumbuka inchi haikuwa na wasomi wa kutosha katika uendeshaji wa Viwanda na makampuni,
Kama shule tu walikuwa wanafundisha walimu wa UPE waliotoka kumaliza darasa la saba,unategemea hayo makampuni yaliyokuwa na management ya wasomi kutoka inche baada ya kutaifishwa yalisimamiwa na watu wenye elimu ya kutosha?
Halafu usipende kuzalau watu
Be careful usiipindishe mada yako mwenyewe.
Sisi tume live the history.
Katika post yangu sijagusia CHANZO cha vita ya Uganda, nimeelezea MATOKEO ya vita ya Uganda.
 
...ulizaliwa 1970 wewe ndy unajuw zaidi yetu kama ilimshinda au haikumshinda kulingana na mateso uliyopitia wakat huo au uchumi wa nch au maendeleo uliyoyakuta akashndw kuendeleza au jns alivyokuw akitawala na utawala wa wakoloni.nadhani ww ndy mwenye majibu wa swali lako,asant
 
Kutawaliwa na Sultani Mzanzibari wa kawaida angeendelea kuwa Manamba hadi leo.
K
Be careful usiipindishe mada yako mwenyewe.
Sisi tume live the history.
Katika post yangu sijagusia CHANZO cha vita ya Uganda, nimeelezea MATOKEO ya vita ya Uganda.
Kabla ya kueleza matokea ilibidi ueleze chanzo,unajua jamii forum ni zaidi ya shule,hatutakiwi na sisi tuwe sehemu ya kuopotosha jamii,huku tunajua ukweli
 
Tulisoma bure na shule nyingi zilikuwa na viwango bora vya ufundishaji. Changamoto zilikuwa nyingi kwake ukizingatia wasomi walikuwa wachache sana.
Hakujenga sekondari muda wote aliokaa madarakani,robo karne, kusoma bure ni misaada hiyo toka kea watu weupe, huchukua miaka kumi na nne kupata msimu wa diploma,12 certificate
 
Hakujenga sekondari muda wote aliokaa madarakani,robo karne, kusoma bure ni misaada hiyo toka kea watu weupe, huchukua miaka kumi na nne kupata msimu wa diploma,12 certificate
Shule zilimilikiwa na serikali na tukasoma sisi, hivyo ni kama alizijenga yeye. Zilitaifishwa kutoka kwa wakoloni.

Mkuu tulisoma bure na miaka ile mpaka masuala ya chakula yalikuwa ni bure, pale forodhani wanafunzi wa sekondari walikuwa wanakula muda wa mapumziko, vifaa vya masomo vilitolewa bure pia.

Nyerere aliheshimu sana elimu, awamu ya kwanza asilimia karibu 95 tulijua kusoma na kuandika.
 
Angesema vinginevyo angepotezwa, Mwinyi alikuwa mjanja, jamaa pamoja na kufeli alikuwa ni dikteta mkubwa sana kuwahi kutokea inchi hii , magu anasingiziwa
Plus,watoao rejea hiyo hawamjui mwinyi,yeye hataki kukuru na mtu,kama unapenda sifa atakumwagia mijisifa,mwinyi alijua kwamba mwamba alifeli vibaya, ndiyo maana alitoa kijembe cha foleni za unga
 
Shule zilimilikiwa na serikali na tukasoma sisi, hivyo ni kama alizijenga yeye. Zilitaifishwa kutoka kwa wakoloni.

Mkuu tulisoma bure na miaka ile mpaka masuala ya chakula yalikuwa ni bure, pale forodhani wanafunzi wa sekondari walikuwa wanakula muda wa mapumziko, vifaa vya masomo vilitolewa bure pia.

Nyerere aliheshimu sana elimu, awamu ya kwanza asilimia karibu 95 tulijua kusoma na kuandika.
Kutaifisha ni sawa na kujenga,bro!?..au ndiyo mahaba,shule za 1900 kuhudumia 1960-80s, wangapi wamezaliwa hapo,kwa nini hujengi shule?..hutaki wasomi?
 
Kutaifisha ni sawa na kujenga,bro!?..au ndiyo mahaba,shule za 1900 kuhudumia 1960-80s, wangapi wamezaliwa hapo,kwa nini hujengi shule?..hutaki wasomi?
Awamu ya pili mpaka ya sita zinafanya kazi gani?. Ni uvivu wa kufikiri kila kitu kumtupia lawama Nyerere wakati wapo waliomfuatia katika nafasi ya urais.
 
Back
Top Bottom