Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Lawama lazima abebeshwe kama ambavyo kikwete, magu, na sasa samia wanavyolaumiwa,
Yaani lawama hazikwepeki kwa kuwa yeye ndio alikua kiongozi,
Inchi ilimshinda na hii ndio statement sahihi
Huko AU makao makuu Addis Ababa Ukitembelea utakutana na Statue zake !

A true son of Africa
A true Statesman of Africa
That’s Mwalimu 🙏🙏
RIP.
 
Sahihi kabisa 🙌👍
 
Pesa yote ilielekezwa kwenye kumshughulikia Nduli !
Mpaka Magari binafsi baadhi yake yalikuwepo huko Front !
Kwahiyo kwa vyovyote vile Uchumi lazima ulitetereka na ndipo Mabeberu wakawa wamempata Mwalimu pale walipotaka kumpata !
Viwanda vilikosa malighafi au?..hivi ni visingizio tu,yule mzee ni failure number one
 
Nyerere anastahili heshima popote anapopewa mpaka leo hii. changamoto za dunia ile sio sawa na hizi za miaka ya sasa. Nchi nzima chuo kikuu kilikuwa kimoja tu.

Unasafiri kutoka Dar mpaka Tanga usiku kucha wakati ni mwendo wa masaa mawili tu.
Ila alikata watu mishahara kuchangia harakati za ukombozi kusini mwa africa,unajua kipindi hicho tuliongoza kupokea misaada,lakini hakujenga shule ya sekondari hata mmoja,lami ikawa suala la peponi,mnasikia simuulizi tu
 
Ingekua hatuwezi kuvinunua maduka yasingekua mengi
 
Ngoja nikusahishe Kwanza,wewe ni kati ya wale waliosoma historia zilizopotoshwa, Ngoja nikupe historia ya Vita vya Tanzania na Uganda, Iddy Amini Dada alipompindua Miritoni Obote alikimbilia Tanzania kwa rafiki yake Nyerere,kwa kushirikiana na Yoweri Museveni na Obote walijaribu kurudi Uganda kwa mtutu wa bunduki wakitokea Tanzania ikashindika, wakafurushwa na majeshi ya Iddy Amini,
Baadaye kwa Sapoti ya jeshi la JKT bado ikashindikana,ndipo Amini akawafurusha mpaka kagera,hapo likaingilia jeshi la JWTZ, kuwafukuza ndani ya mipaka yetu
Sababu targeti ya Nyerere ilikuwa kumrudisha madarakani rafiki yake Obote ikabidi Vita viwe vya mda mrefu mpaka Arua kalibu na mpaka wa Sudan,

Sasa jiulize hivi Vita vilivyoharibu uchumi wa Tanzania vilikuwa na umuhimu wowote,Au mchokozi alikuwa Nyerere au Iddy Amini, maana yake Obote asingepinduliwa na Iddy Amini, hivi Vita visingetokea,na Iddy Amin hakuwa mjinga aanze tu kushambulia Tanzani,kwa nini hatukumshitaki kama tulivyoshambuliwa na Burundi wakatulipa fidia,msipende kusoma historia zilizopotoshwa na watu kwa maslai ya Viongozi

Na nimekushangaa kwa kusapoti Azimio la Arusha,ni kati ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere,na kumbuka inchi haikuwa na wasomi wa kutosha katika uendeshaji wa Viwanda na makampuni,
Kama shule tu walikuwa wanafundisha walimu wa UPE waliotoka kumaliza darasa la saba,unategemea hayo makampuni yaliyokuwa na management ya wasomi kutoka inche baada ya kutaifishwa yalisimamiwa na watu wenye elimu ya kutosha?
Halafu usipende kuzalau watu
 
Ila alikata watu mishahara kuchangia harakati za ukombozi kusini mwa africa,unajua kipindi hicho tuliongoza kupokea misaada,lakini hakujenga shule ya sekondari hata mmoja,lami ikawa suala la peponi,mnasikia simuulizi tu
Tulisoma bure na shule nyingi zilikuwa na viwango bora vya ufundishaji. Changamoto zilikuwa nyingi kwake ukizingatia wasomi walikuwa wachache sana.
 
Kuna ajenda ya siri nyuma ya kutukuzwa sana kwa Nyerere, lakini ukiangalia hali ilivyokua kipindi chake mfano umasikini nankushughulikiwa kwa walipishana nae mawazo kama Oscar Kambona.
Huoni jinsi usivyo kuwa na akili?
Kutakuwaje na "ajenda ya siri..." kwa kiongozi ambaye hayupo tena, lakini wajinga wa aina yako bado mnahangaika na 'legacy' ya uongozi wake?
Nani ana ajenda hapa kama siyo nyinyi? Ajenda yenu ni nini?
Namna unavyo andika tu inaonyesha wazi wewe huna uelewa wala ufahamu wa kujadili jambo kama hili kwa kutumia akili zako mwenyewe.
Umehitimu wapi/chuo gani; kile cha Kariakoo kwa mzee Mohammed na wazee wake?
 
Mbona kama umepanick, padri alisema

nyerere hakuwa malaika,amekosea mengi tu,
Siku ya pili wakamuweka ndani, hata sasa hamuheshimu mawazo ya wengine kama ambavyo wewe umejibu maoni ya mdau
 
Naona mfuasi wa Nyerere, mada imekupiga kwenye mshono, sasa kama uko Ethiopia na Kenya walitaabika ndio halali na sisi tutaabike.
Nikisema uwezo wako wa kufikiri ni mdogo usidhani nabahatisha. Nimeweka hiyo mifano ya Kenya na Ethiopia kwa maksudi kabisa kuonyesha kuwa tatizo la njaa halikuwa kwa Tanzania pekee, na halikusababishwa na uongozi mbaya kama mnavyo taka kuaminisha watu. Lakini wewe hilo nalo huna uwezo wa kulitilia maanani.
 
Tatizo hapa kuna watu wanajadili kishabiki sababu tu wanamapenzi na Nyerere,Wazee wa Zamani waelewa huwa hawamkubari
 
Jikite kwenye mada, aliharibu inchi na huo ndio ukweli, na ukweli haunin'ginii
Kama si mzee Mwinyi (MUNGU amrehemu)tungekuwa kama zimbabwe
Mpaka anang’atuka bado tulikuwa na pesa yetu ikiwa Strong !
Hakukubali kugeuka jiwe na ndio maana akaamua kung’atuka. !

Watu wengi wenye Chuki na Mwalimu wanazo hidden causes za kwanini wanamchukia na kumsema vibaya. !

Na hiyo huwezi ukawazuia watu wasimchukie au kumsema vibaya !

Lakini tuliokuwepo ENZI zile na ambao hatukuona ubaya wowote anaopakaziwa na wabaya wake tutaendelea kumkumbuka kwa Mazuri yake ambayo yalikuwa mengi na tutamsamehe kwa yale machache aliyokosea 🙏🙏🙌
 
Tatizo hapa kuna watu wanajadili kishabiki sababu tu wanamapenzi na Nyerere,Wazee wa Zamani waelewa huwa hawamkubari
Ni wazee wapi hao?
Hata leo hii, pamoja na kwamba Mwalimu alikwisha fariki siku nyingi; ukipitisha kura kumshindanisha Samia na Nyerere katika uongozi, Samia haambulii kitu.
 
NNh
HHe
Hebu nikuulize kulikuwa na Sababu gani ya Tanzania kuingia Vitani na Uganda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…