Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Nimeshakuambia huyo ni baba Y Yako wewe sio wa taifa maana umesema mama Yako anamtambua
Founding Fathers huko US wamechongewa hadi kwenye Miamba ya Granite.
Dayle-Founding-Fathers.jpg

Usichanganye Biological Father na Founding Father rudi Shule Kasome😂😁
 
Jibuni maswali kama mnajua, acheni kumshambulia aliyeleta swali, wabongo wengi mna akili za mavi sana ndio maana hamna maendeleo
 
Shukrani Gani wewe Nyerere ni mjinga mmoja tu hajafanya lolote kwenye hii nchi

Ulitaka ajilimbikizie mali kama hawa waliopo leo unafikiri Angeiacha nchi moja?
Ni nani angekubali kodi za watanganyika zichukuliwe na Mzanaki na familia yake .
Unafikiri vijana wa enzi zile walikua waoga kama hawa sasa hivi machawa wanaoshangilia nchi yao kuuzwa kwa wazungu na waarabu bila kujua miaka 50 ijayo watakua waosha makalio ya waarabu ndipo wapate pesa ya kula?

Nyerere ndiye aliyechaguliwa na Mungu ili kuweka dira ya Nchi ya Tanganyika ipende usipenda na haitabadilika wengine wote wamejawa na ubinafsi na ufisadi.

Hata mitume wa Mwanzo hawakujenga nchi zao bila kwanza kuweka misingi ya watu wao kuwa na haki ,usawa na kuondoa dhulma.

Nyerere alikua kiongozi sio mtawala na mlafi kama wengine,miaka miwili malori zaidi ya 1000 majengo yasiyohesabika je wakikaa miaka 24 kama Nyerere?

Mabeoari yameua watu wengi sana ili kuhalalisha uovu wao.

Shukrani Gani wewe Nyerere ni mjinga mmoja tu hajafanya lolote kwenye hii nchi
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukali, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni inchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Nyerere Nchi haikumshinda kivile alijitahidi sana isipokuwa nchi iliyumba sana alivyoamua kuingiza nchi vitani kumpiga na kumfurusha madarakani Iddi Amin ile vita iligharimu sana nchi hadi ikafilisika .
Pia sera za ubepari zilimbana sana kwa kuwa alikuwa na mtzamo wa sera kinzani za ujamaa .
 
Mimi sijamfagilia mtu yeyote duniani wewe unamfagilia bwana wako Nyerere ambaye anachomwa Kuni huko Kwa ujinga aliyofanya tanzania
Kwenye Moto wa miungu ya wazungu na waarabu.?
Aisee!!!
Yaani miungu ya waarabu na wazungu inayothamini pesa ,mali kuliko watu walioumbwa na Mungu wetu Halisi na kutupa bara zuri lenye kila kitu ili tufurahiye uumbaji wake halafu unaona kuwa hao miungu ya waarabu na wazungu wana haki ya kumchoma moto Nyerere aliyepinga watu kuuzwa kama machungwa na tembo kuuawa kwa mamiloni na waarabu ili tu wafanye starehe na anasa.
Basi hizo kuni zitakua zimetoka jangwani huko Oman mana hata miti hawana hao wazao wa majini na mashetwani wanafiki !
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukali, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni inchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Ilimshinda kweli. Sera ya ujamaa ilifeli pakibwa sana nchi ikawa hoi. Ilibidi ampishe mzee ruksa ili wabadili gia angani. Aliona akibadili yeye atakua anaikana imani yake
 
Nyerere Nchi haikumshinda kivile alijitahidi sana isipokuwa nchi iliyumba sana alivyoamua kuingiza nchi vitani kumpiga na kumfurusha madarakani Iddi Amin ile vita iligharimu sana nchi hadi ikafilisika .
Pia sera za ubepari zilimbana sana kwa kuwa alikuwa na mtzamo wa sera kinzani za ujamaa .
Kwa hiyo tusema maduka ya Kaya yalianzishwa baada ya vita vya kagera?
 
Kwa hiyo tusema maduka ya Kaya yalianzishwa baada ya vita vya kagera?
Hayo maduka kusema kweli nilivyosikia kwani sikuwepo yalisaidia sana wananchi kupata bidhaa kwa bei nafuu isiyokuwa ya kibiashara (kijamaa) kabla ya vita maduka hayo yalikuwa na bidhaa nyingi muhimu kwa mahitaji ya kibinadamu ila baada ya vita na maduka hayo yalifilisika kama ambavyo serikali ilifilisika
 
Ila nakazia hapa kwa umri wako huu ukisoma Bure shule ya msingi kwa kulipa ada ya kawaida kabisa huku ukipatiwa madaktari bure na sekondari ulilipa ada bila michango yoyote huku Ukipata huduma stahiki tofauti na sasa elimu ni Bure lakini michango ni mara 10 zaidi ya ada ya iliyofutwa

Pia ulipata huduma za afya bure na dawa zilikuwa zinapatikana huku sasa hivi pamoja na kichangia na uwepo wa NHIF lakini bado watu wanabaguliwa kwa baadhi ya magonjwa.

Huyo mwamba pamoja na kwamba inaonekana alifeli ila najiuliza kama kungekuwa na cost sharing ya huduma za kijamii kama sasa maana yake tungekuwa tumesogea zaidi maana kipindi kile mwamko wa wananchi kuchangia Maendeleo ulikuwa mkubwa. Makusanyo yote yalipelekwa kwenye kutoa huduma za kijamii pasipo kuboresha miundombinu

Ila mwisho wa siku pambana acha kulia lia, Nyerere ametoka madarakani miaka 40 iliyopita hivyo hakuna excuse maana miaka 40 ni mingi kuleta mabadiliko hata kama alichemsha
 
Hayo maduka kusema kweli nilivyosikia kwani sikuwepo yalisaidia sana wananchi kupata bidhaa kwa bei nafuu isiyokuwa ya kibiashara (kijamaa) kabla ya vita maduka hayo yalikuwa na bidhaa nyingi muhimu kwa mahitaji ya kibinadamu ila baada ya vita na maduka hayo yalifilisika kama ambavyo serikali ilifilisika
Nahitaji tujadiliane kwa hoja kama hivi siyo kutukanana kama wengine haileti heshima

Na kwa ndugu zetu Zanzibar maisha yalikuwaje kipindi hicho?
 
Nahitaji tujadiliane kwa hoja kama hivi siyo kutukanana kama wengine haileti heshima

Na kwa ndugu zetu Zanzibar maisha yalikuwaje kipindi hicho?
Wazanzibar maisha yao hayakuwa magumu sana kwao kwani kwanza walikuwa wachache na pia walikuwa wanasaidiwa sana na ndugu zao waarabu.
Wazanzibar mapinduzi waliyoyafanya na Muungano waliofanya na Tanganyika viliwaingiza kwenye maisha magumu zaidi.
Wazanzibar wasingefanya yale mapinduzi zanzubar ingekuwa mbali sana kwa sasa
 
Ulitaka ajilimbikizie mali kama hawa waliopo leo unafikiri Angeiacha nchi moja?
Ni nani angekubali kodi za watanganyika zichukuliwe na Mzanaki na familia yake .
Unafikiri vijana wa enzi zile walikua waoga kama hawa sasa hivi machawa wanaoshangilia nchi yao kuuzwa kwa wazungu na waarabu bila kujua miaka 50 ijayo watakua waosha makalio ya waarabu ndipo wapate pesa ya kula?

Nyerere ndiye aliyechaguliwa na Mungu ili kuweka dira ya Nchi ya Tanganyika ipende usipenda na haitabadilika wengine wote wamejawa na ubinafsi na ufisadi.

Hata mitume wa Mwanzo hawakujenga nchi zao bila kwanza kuweka misingi ya watu wao kuwa na haki ,usawa na kuondoa dhulma.

Nyerere alikua kiongozi sio mtawala na mlafi kama wengine,miaka miwili malori zaidi ya 1000 majengo yasiyohesabika je wakikaa miaka 24 kama Nyerere?

Mabeoari yameua watu wengi sana ili kuhalalisha uovu wao.
Wacha kuleta sifa za kimungu mungu hapa Nyerere alikuwa binadamu kama wengine, alifanya mazuri na mabaya. Hakupenda kukosolewa na unazungumzia machawa gani wa sasa kuliko wale wa zamani wa 'Zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti? Vijana walikuwa desperate mpaka wakajaribu kuteka ndege ili waondoke nchini wakatafute maisha.

Wewe ulikuwa hujazaliwa ndiyo mana unakariri hayo uliyosomeshwa huko mashuleni
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukali, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni inchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Kwa kitendo cha kuung'ang'ania ujamaa wake wa mchongo ndiyo kumeifanya hii nchi mpaka kesho, kuliwa na wajanja wachache.
 
Nyerere anastaafu Ameacha viwanda vya redio ,matrekta (kubota ),magari( Nyumbu),sabuni ,kiwanda cha kuassemble scania Kibaha, Nyembe,dawa,baskeli, viberiti,mafuta,matairi, magunia ,nguo ,Mikate,maziwa,nyama,ngozi,viatu,mabegi, bia, sukari, sementi, chuma, mabati, vioo,cable za umeme na transfoma ,balbu,tochi , maturubai ,ndala za bata, sido ,vyuo vya ufundi Veta, vyuo vya Ufundi kama Dar Tech. Chuo Kikuu cha Dsm ,Mzumbe na vyuo vya kati kama Uhasibu ,IFM, CBE , Mipango, Chuo cha madini, chuo cha Kivukoni NIT, Ustawi wa Jamii , Shirika la ELIMU kibaha, Hospitali kila mkoa na Wilaya nchi nzima wakati huo hakuna tozo za majengo mengi mpaka vijijini,hakuna pikipiki nyingi zinazotumia mafuta na kulipa kodi ya kuagiza spea ,hakuna idadi kubwa ya waganyabiashara wakubwa ,hakuna tozo za umeme,hakuna idadi kubwa ya magari na pikipiki zinazotoa ushuru kwenye stendi na kwenye mafuta kwa wingi kama ilivyoo.

Kama sio Nduli Iddi amini aliyetumiwa na Waarabu na wazungu kuanzisha mapinduzi Uganda na kuvamia nchi ya Tanganyika tungekua mbali sana leo.

Lakini pia tulipata bahati mbaya kupata Mtu aliyekua sawa na Waarabu na Wazungu na kuja kugawa Rasilimali zetu kwa wageni na kuua viwanda vyetu vyote baada ya kushindwa kuwakamata na kuwafunga au kuwanyonga wezi wa mali za umma naye alawa mwasisi wa kujilimbikizia mali akishirikiana na waarabu na wazungu. Nchi ikawa shamba la wageni mpaka leo wageni wanqivamia Tanganyika na kuweka lachawa na machoko na kila aina ya walevi ,mashoga,wasagaji na wafiraji kumtukana Nyerere kwa kutumia pesa walizojikusanyia baada ya kuihujumu nchi.
Genge la wezi lilianza siku nyingi kwa kuwaua viongizi waadilifu wenye fikra njema na maono na kuwahujumu akiwemo Sokoine na kutuachia Mafisadi na wahuni.

Kama wizi wa mali za umma ndio maendeleo ya nchi basi Tanzania tumeendelea sana.
Nchi yenye madini ya kila aina ardhini tunadanganywa na misaada ya tende na halua kwa kujengewa nyumba za Ibada badala ya hospitali na vyuo vya teknolojia wajifunze watoto wakiwa wadogo badala yake wanajazwa chuki za kidini na kupigania maslahi ya dini zilizoasisiwa na Shetani mana Mungu hana dini kwa sababu haabudu na haombi Msamaha na hawekewi sheria na hahitaji kumwabudu yeyote kwa hiyo ni wazi kuwa Mungu hana dini bali ana maarifa yote na ujuzi wote na ni mtawala wa vyote.

Wakati Irani ,China ,Uturuki, India ,Japan,Korea, Urusi , Ujerumani wako bize kukuza taknolojia na ugunduzi huku Tanganyika tuko bize kujenga nyumba za ibada na wanaonufaika ni watawala na viongozi wa dini kwani dini hizo haziwasaidii watu kuwa waadilifu badala yake wanakua na chuki wao kwa wao na kuona dini zao ni bora kuliko kujenga nchi yao . Cha ajabu wale wale wanaowafandhili wao wanatafuta mianya ya kujilimbilizia mali na watoto wao hawana muda wa kukesha lisikitini na kwenye masinagogi yao waliyoyajenga kwa misaada waliyopewa kwa kubadilishana na ardhi yenye madini au kuwapa viwanda kwa bei chee.
 
Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukali, Mafuta na hata nguo.

Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni inchi ikiwa vizuri.

Je, Uongozi ulimshinda?
Wewe Unasema umezaliwa miaka ya sabini halafu Unasema kulikuwa hakuna nguo na kwamba watu walikuwa wanavaa magunia 😂😅

Mimi nimezaliwa miaka ya Hamsini lakini sikuwahi kuona watu wakivaa magunia 🤣

Na pia vyakula tulikuwa tunakula mpaka tunasaza 😀😅

Maisha yalikuwa ya raha sana ndio maana ukaona hata Wacongomani wengi walihamia huku Tanzania kuja kupiga muziki !

Maisha yalikuwa mazuri sana asikudanganye mtu !

Sasa hivi maisha ni magumu kuliko ilivyokuwa Enzi zile !
Kama wapo Wazazi wako waulize !
Wewe usingeweza kujua maisha yakoje maana miaka hiyo ya 70 ndio kwanza Umezaliwa !😅🙌🙏👍
 
Kenya walifaidika na soko la magendo upande wa kaskazini. Mafuta ya taa, bia(tusker na plisner), vitambaa vya nguo, mafuta ya kula nk nk.
 
Wewe Unasema umezaliwa miaka ya sabini halafu Unasema kulikuwa hakuna nguo na kwamba watu walikuwa wanavaa magunia 😂😅

Mimi nimezaliwa miaka ya Hamsini lakini sikuwahi kuona watu wakivaa magunia 🤣

Na pia vyakula tulikuwa tunakula mpaka tunasaza 😀😅

Maisha yalikuwa ya raha sana ndio maana ukaona hata Wacongomani wengi walihamia huku Tanzania kuja kupiga muziki !

Maisha yalikuwa mazuri sana asikudanganye mtu !

Sasa hivi maisha ni magumu kuliko ilivyokuwa Enzi zile !
Kama wapo Wazazi wako waulize !
Wewe usingeweza kujua maisha yakoje maana miaka hiyo ya 70 ndio kwanza Umezaliwa !😅🙌🙏👍
umekula ubwabwa mwingi halafu ukenda kulala na kuota hayo maisha mazuri ya Nyerere.
 
Back
Top Bottom