Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Miss_Mariaah

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
2,176
Reaction score
4,979
Hello wakuu,

Nimeona nishare sababu niko katika hali mbaya. Mawazo mabaya ya kujidhuru yananijia kichwani. Sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye. Kila kitu kilikuwa vizuri, ghafla akakata mawasiliano. Wiki 3 sasa nikimpigia hapokei, sms hajibu.

Nimehangaika, nikaongea na dada na kaka yake lakini bado alinikalia kimya. Mara ya mwisho kuwasiliana naye tulizungumza vizuri tu. Mipango yetu ilikuwa tufunge ndoa na alipanga mwezi huu aje nyumbani kujitambulisha. Lakini ghafla kimya chake kikatokea.

Baada ya kimya kirefu, siku 5 zilizopita nikamtumia sms ya kuachana lakini hakunijibu kitu. Naumia sana. Sijawahi kumkosea chochote ila ameamua kunifanyia ukatili huu. Naumia na najiuliza maswali ambayo sipati majibu.
 
Tukusaidie nini Sasa?
 
Pole Sana ...mahusiano yana mengi..
 
Be strong.....jivute pembeni kwa muda kama ana kupima ......atarudi mwenyewe uwe stromg akirudi mpe conditions usimuonyeshe uko desparate..vumiliaa haijaisha hadi oiishe anakupima tu huyoooo.......usifanye ujinga wowote now tulizanaaa
 
Tutaaminije lakini samahani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…