Ubalikiwe sana mtumish wa BWANA.
MUNGU ni MWAMINIFU SANA
Nakuombea uushinde hii changamoto iliyoko mbele yako, ningepata namba yako ya cm ingekuwa vizuri lakin nitajaribu kukuelezea hata kwa kuandika tu
Ukisoma kitabu cha kwanza cha nabii samweli sura ya tatu utaona kwamba MWENYEZI MUNGU aliinuka akamwita nabii samweli kuanzia mara moja hadi mara tatu, lakin nyakati zote hizo tatu ambazo MWENYEZI MUNGU alimwita samweli badala ya samweli amwitikie MUNGU na amwendee MUNGU yeye nyakati zote hizo alimwendea kuhani El
Mpaka kuhani El akajiongoze akamwambia samweli sikuiiti mimi bali huenda unaitwa na MWENYEZI MUNGU kalale tena ukiitwa mwitikie MUNGU na mwendee MUNGU
Sasa hapa nataka nizungumze kitu mtumish Kuna kitu kinaitwa macho ya KIROHO au macho ya ROHO au macho ya ROHONI, HAKUNA KITU KIBAYA KAMA KUKOSA MACHO YA ROHO UTATESEKA SANA
tunamuona samweli akiseka hajui amwendee nani kati ya MUNGU na kuhani El, badala ya amwendee MUNGU yeye anamwendea kuhani El mpaka MWENYEZI MUNGU mwenyewe anayahamisha macho ya ROHO kutoka kwa samweli anayapeleka kwa kuhani El, kuhani anagundua kwamba kwa macho ya ROHO huyo kijana samweli anaitwa na MUNGU
Narudia tena MWENYEZI MUNGU anayahamisha macho ya ROHO kutoka kwa samweli anayapeleka kwa kuhani El, kuhani El anagundua kwamba kwa macho ya ROHO kwamba huyo kijana anaitwa na MUNGU
Sasa ndo wewe sasa MWENYEZI MUNGU amekuita katika wito wa ndoa sasa wewe ulichokosea umekosa macho ya ROHO au macho ya ROHONI badala utafute MUME wewe umeenda kutafuta mtu tu ili mradi mwanaume kwa sababu ni mwanaume, kwahiyo MWENYEZI MUNGU alichoamua kukifanya kwako ni kuyahamisha macho ya ROHO au macho ya ROHONI na kuyapeleka kwa huyo mnyakusa
Ndipo huyo mnyakusa akatambua kwamba kumbe wewe maria unahitaji ndoa na yeye hahitaji ndoa kama kuhani El alivyotambua kuwa samweli anaitwa na MUNGU na yeye kuhani El hamuiti samweli ndipo kuhani akamwambia nenda unaitwa na MUNGU wala Mimi sikuiiti
Sasa basi huyo kijana wako mnyakusa baada ya kupata hayo macho ya ROHO kaamua akae kimiya kwa maana yeye huenda siyo muoaji ndo maana kakaa pemben
Sasa wewe badala ushukuru kwa MUNGU unataka kujiua tena why unataka kuzihuzunisha mbingu,
MAISHA YA NDOA NI KITU ENDELEVU SANA USIFE MOYO WALA USIILAUMU MIPANGO YA MUNGU
JIKUBALI MTUMISH USIJE KUHALIBIKIWA
Asante
Kama ungenipm nikapata namba yako tungeongea vizuri binti wa MUNGU
BWANA na amani yake awe pamoja na wewe