Naumwa sana: Nimefika Pemba ili nitibiwe kienyeji, naombeni msaada wa Mtaalamu

Muendelezo Yesu kristu wakati anazaliwa mamajusi waliona myota wakajua Kuna mtu anazaliwa ? Huo sio unajimu? Mamajusi walipeleka dhahabu ubani na manemane Manemane ni dawa ya kienyeji ambayo ukienda maduka ya dawa za kiarabu utaikuta , ubani utaukuta nyinyi walokole mnajua vilipelekwa na kufanya kazi gani ? Mamajusi kwa lugha ya kiyunani are translated as wise men kwa wakati ule ambayo kwa tafsiri ni waganga wa kienyeji , anayebisha aje twende mpaka kiebrania au kilatin tupate tafsiri zaidi , innomino pate et filio et spitus saint amen .Kuna mtume mwingine wa dini yenu ya kiarabu kapewa utume na mganga wa kienyeji anaitwa Walaga bin Naufal who was blind and wise in telling future of somebody , a.k.a utabiri kwa lugha za walokole kumbe ni ramli ileile.
 
Wabongo mna matatizo sana yaani mnaleta masihara kwenye afya ya mtu alie serious kutafuta msaada .!!!
 
Ulifunga safari kwenda pemba ukiwa tayari Mgonjwa au ugonjwa umekukutia ukiwa huko?
 
Acha ujinga nenda kwa Mwamposa, nauli yako tu ukifika umepona na hutoi hata mia...
Kwa YESU kuna uponyaji na furaha... Kimbia sasa hujachelewa...
Hao waganga watakula pesa zako, watakupandikiza majini, watakuongezea matatzo na watakugombanisha na Mungu wako... Mwisho utakuwa mtumwa wa majini na shetani na utakufa vbaya
 
Wabongo mna matatizo sana yaani mnaleta masihara kwenye afya ya mtu alie serious kutafuta msaada .!!!
sio masikhara, yeye mada kaileta kimasihara,eti nimeshuka hapa pemba sina mwenyeji,utaendaje sehem ambayo hauna mwenyeji au conections,hata huyo mganga anaweza kukushtukia,ilitakiwa apate ushauri kabla ya safari. ila kama ni kweli pole yake sana.
 
Wabongo mna matatizo sana yaani mnaleta masihara kwenye afya ya mtu alie serious kutafuta msaada .!!!
sio masikhara, yeye mada kaileta kimasihara,eti nimeshuka hapa pemba sina mwenyeji,utaendaje sehem ambayo hauna mwenyeji au conections,hata huyo mganga anaweza kukushtukia,ilitakiwa apate ushauri kabla ya safari. ila kama ni kweli pole yake sana.
 
Amelaaniwa mtu yule amtrgemeaye mwanadamu na kumfanya kuwa Kinga yake
Mbna unatuchanganya mkuu
We mwenyewe post iliyopita umesema amtegemee yesu.

Swali
We uliumbwa kwa udongo na yy kaumbwa kwa kutumia nn nnavyojua ni binadam mwenzetu tu, tumezidiana sifa tu

NB
Anyway, mwenye thread yupo serious
Kwenye ushauri wa masuala ya tiba za kienyeji.
Ww unaleta risala za kiroho.

Umemkosea!! , Kama huna Cha kujibu kulingana na kichwa cha thread apo juu VUNGA.

Kuna watu Wana Iman Kali kuliko ww.
Wametulia.



End**
 
0773806592
 

Hali ya mleta mada nai feel sna. Sabab mi mwenyewe nlishapitia hko for 9yrs (kiroho & kienyeji & hospitals ) vyote vilidunda nlichanganyikiwa kabisa kila kitu hakiendi mwili mmbovu (unawaka Moto, ganzi, vitu vinatembea mwili mzima, unahisi Kuna Kama 100kg mgongoni)

rehma zake Mungu nlipata amani badae hukoooo Muheza Tanga,

pemba wapo hao watu lkn hasa wete au kisiwa Cha chumbe au Tumbatu


Tafta bodaboda au wazee kwenye draft au kahawa au nenda kwa shekha wa mtaa huwa hawakosagi data Hawa watu.

Namba sikushauri Sana we tumia njia apo juu mojawapo utawapata mguu kwa mguu mpka unafka au wao wenyewe ndo wakupe namba
 
UPDATE:
Nimeshapata mtaalamu na niko huku kisiwani natibiwa.
Tiba nilianza jana na nashukuru Mungu mpaka sasa najihisi nafuu...ila nilienda nikiwa katika hali fulani, hivo inabidi nikae huku ili hii hali iishe niweze kumalizia tiba.

Namkushukuru sana mwana Jf mmoja kwa moyo wake wa kunisaidia....
Wema bado wapo wengi sana Jf.
Na wabaya pia wako wengi sana Jf.

Asanteni wote mnaoendelea kunipa pole na kunitia moyo kuanzia jana mpaka leo.

ILA NAOMBA NIWAAMBIE KITU, SISI BINADAMU TUNAZALIWA TUKIWA NA DINI ZETU TIMAMU.
UKIONA MPAKA MTU ANAIKENGEUKA DINI YAKE KWA MUDA NA KUTAFUTA TIBA YA UPANDE WA PILI, USIMCHEKE WALA KUMKEJERI WALA KUMPA MANENO YA KARAHA, BALI MPE POLE NA KAMA UNA NJIA YA KUMSAIDIA, BASI MSAIDIE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE....JAMANI TIBA NA MAGONJWA YAPO.

Sina roho mbaya, binadamu tumeumbwa kusaidiana.
Nikipona nitakuwa shuhuda.

Asanteni.
 
Dah kweli hatujui yalikukuta lakini kwenda sehemu pasipo kujua unaenda kwa nani hata kama hupajui anapoishi basi angalau ujue anapofanyia shughuri zake mkuu kweli hapo haupo sawa pole sana ushauri mdogo tafuta pahala pa kulala kisha anza kujichanganya maskani utapata tu mtaalam tena kwa pemba hakuna uficho sana kama unguja.
 
Bado hujapona kule ikulu? Sini uliambiwa uende hospital au umeambiwa umerushiwa dawa? Njoo inbox
 
 
Kwani yesu anakaa Pemba..?
 
Mnataka mjue machimbo ya watu nini mkaharibu code zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…