Naumwa sana: Nimefika Pemba ili nitibiwe kienyeji, naombeni msaada wa Mtaalamu

Naumwa sana: Nimefika Pemba ili nitibiwe kienyeji, naombeni msaada wa Mtaalamu

Washa mishumaa ya nta kwa muda wa saa moja au mawili kabla ya kulala hii itakufanya ulale kwa utulivu na kukumbuka ndoto zako
1737230252932.jpg
 
Kwani mnaojuaa hizo chimbo za Waganga wa jadi mkimjibu hapa au kumfata inbox mnapungukiwa nini??
Kama hauna cha kumsaidia ukinyamaza pia ni busara tosha.

Dunia ina mengi sana yasipokukuta unaweza kuwa unatukana kila mtu na kujiona wewe unaishi kwa akili zako.
Siku zote chizi anachekesha akiwa atoki nyumbani kwako..Omba na Sali sana yasikukute Duniani kuna mitihani mizito mno.
Polee sana muhitajii jukwaa ni kubwa sana na kila mtu anaupeo wake wa kufikiriaa naamini kabisa msaada unaweza kuupata hapa hapa jukwaani Waungwana wapo

Umenena vyema
Hao wote waliomjibu nyakunyaku wana stress zao nyingi wanatolea kwa huyu.

Wanajiaibisha bila kujua, huku wakifikiri ni sifa kujibu utumbwo wao kwa kutosema na kupita huku mtu yupo serious
 
Awali ya yote nakupa pole lakini kingine hebu tuambie Kuna mtu yoyote yule mshagombana au umedhulumu chake? Lakini hujaeleza ni Tatizo Gani linalokusibu.Na ni kwa mda Gani ila Mimi ningekushauri ungeanza kushughulika kiroho zaidi kuliko huko kwa waganga Cha msingi imani kwanza uamini Yesu anaweza kukuponya sijajua Imani yako.Lakini kingine kama ulikosana na mtu patana nae
 
Kwani mnaojuaa hizo chimbo za Waganga wa jadi mkimjibu hapa au kumfata inbox mnapungukiwa nini??
Kama hauna cha kumsaidia ukinyamaza pia ni busara tosha.

Dunia ina mengi sana yasipokukuta unaweza kuwa unatukana kila mtu na kujiona wewe unaishi kwa akili zako.
Siku zote chizi anachekesha akiwa atoki nyumbani kwako..Omba na Sali sana yasikukute Duniani kuna mitihani mizito mno.
Polee sana muhitajii jukwaa ni kubwa sana na kila mtu anaupeo wake wa kufikiriaa naamini kabisa msaada unaweza kuupata hapa hapa jukwaani Waungwana wapo
acha ushamba mkuu,humu jukwaani hauhitaji kuyachukulia serious masuala yote,wengine wanachangamsha jukwaa tu,na kama ulivyosema kama mtu hana cha kumshauri bora akakaa kimya,kipi wewe umemshauri! Kheri ungempa pole tu ukasepa zako. Kwako mleta mada, waganga wa wa kienyeji wapo huku bara tena kwa bei chee kabisa,hasa tabora,kigoma,kanda ya ziwa yote. Huko pemba utaishia kupigwa pesa na kutupiwa majini.
 
Aiseeee pole sana , wasamehe bure wanaokukejeli, dunia Ina mambo mengi sana, sio kila tatizo linanatibiwa hospitali au au kwa wachungaji, manabii na mitume feki wa Tanzania .Kumwambia njoo kwa yesu ndio mmemsaidia ? Yaani mnawaponda waganga halafu mnaenda kwa sirisiri .Hao wachungaji manabii na mitume mbona wanafanya kazi zilezile zinazofanywa na waganga ? Wanapiga ramli na kuibadilisha jina eti utabiri , wanawapa watu dawa za kienyeji wanabadili jina wanaziita , mafuta ya upako, maji, udongo kumbe mambo ni yaleyale , Yaani watanzania wa ajabu sana , unashabikia dini za wakoloni bila hata kujua zimeletwa kwa sababu gani? Yaani mkimtaja Yesu kristu mnajiona mmestaarabika ? , Mkiwaponda waganga mnajiona mna akili sana , kumbe bure kabisa, Soma the role of the missionaries in Africa , to prepare Africans for the complete colonisation and supress the courage and brave heart of the Africans . Kwa kifupi mitume wenu wote wa dini za mapokeo walikuwa waganga wa kienyeji na ushahidi upo.
 
Back
Top Bottom