Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Kukabiliana na wabongo wezi imeshindikana kwa hiyo suluhisho ni kuwapa waarabu ambao sio wezi, kweliii!!!! Kwa nini wabongo wanakuwa wezi? Kuna mwenye hili jibu? Kama haliko kwa nini lisijulikane na kupatiwa ufumbuzi.

Hii ishu mimi naiona ni kama mzazi nyumbani kwake kuna chakula kingi. Ila anao watoto ambao watukutu na si waaminifu wanadokoa hicho chakula.

Kudhibiti huo udokozi anaona karaha. Hivyo anaamua jambo la kufanya ni bora mimi niwe na uhakika wa kupata chakula njaa niisikie tu huko. Baada ya kupata huo uhakika anasema sasa hiki chakula kilichopo kwa vile watoto hawa sio waaminifu basi ngoja nifungulie na mbwa nao waje kugombania na kugawana hicho chakula na watoto. Uzuri wenyewe hawa mbwa ni wale waliopata mafunzo hawawezi kuwadhuru watoto zaidi ya kula hicho chakula na watoto.
Ishu kubwa bandari iendeshwe kisasa cargo ziingie na zitoke kwa wakati maswala ya usenge wa wabongo wanao fanya hapo kushirikiana na tra yaishe.
Bandari + tra imekuwa kichaka cha upigaji na kufirisi watu ,mjomba angu amefanya kazi hapo miaka ya 60 hadi Leo mifumo ni Ile Ile hakuna kilicho badilika. Contena zinajazana hapo muda unapotea kodi inapotea bado rushwa na ukiritimba umetawala .Bora serikali ikae bambeni ijipigie percent yake tu, huku mifumo ikiboreshwa.

Imebaki taNesco .

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
Ifike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.

Kwa taarifa zaidi soma hapa >> Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam

Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.

Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?

Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.

Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.
It
Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
Serikali ilinunua ndege za biashara mnashangilia, ikikodisha bandari ili isifanye biashara mnasifia! Tanzania nchi yangu Tanzania
 
Bila ya mpangilio maalumu....

Kyuku lilu, Kulikuwa hakuna ubisnafsishwaji , kulikuwa na Uwezeshwaji wakati wa WW'2....Huo ndio Ukweli.

.....Ubinafsishwaji unaodaiwa humu Jamvini JF ni....

.....ule wakusema Tuwaachie wazungu waje watunyooshee- that is Pathetic

Soma Historia tena,tena vizuri tu.
Huwa inajirusdia na haijalishi imetokea kwa nani-alimradi imetokea Duniani.

Nitatumia Mfano wa Ufalme Dhalimu wa Muingereza. Ambao ndio ulikuwa chanzo kikuu cha mitufuano Ulaya katika karne chache zilizopita, takribani miaka 900 iliyopita. Na kupeleka Private/public partneship yaani waliokuwa naza na wale wanaosimamiwa na Serikali kushamiri.

Nchi nyingi , mfano Marekani, Australia NewZealand n.k zilitokana na Migongano kati ya Wafanyabiashara wakubwa waliohodhi madaraka makubwa ya kifedha, na ya Kisiasa.....yaani Serikali za Kifalme na Familia zao waliokuwa na fedha na madaraka ya uamuzi wa kisiasa na ya kidini.....
Na....

Wa Machinga(watu wa chini na wa kawaida) na wengine wengi tu, Uingereza na kwingineko(France, Uturuki,Portugal) to name a few. Waliokuwa katika vuguvugu za kujikomboa, Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.

.... kumbuka ilikuwa ni Wafanyabiashara (marafiki wa Famikia za Kifalme)waliopewa kibali na Serikali za Kifalme kwenda kuvamia maeneo au Nchi , Visiwa na mpaka kufikia mabara kama Australia, New Guinea, India, New Zealand n.k n.k

Sasa , baada ya biashara kukua, wamachinga nao wakakua,yaani,nao waliweza kuwa na hela kama baadhi ya Wafanyabiashara wakuu(waliopewa vibali na madaraka na Falme zao/serikali zao) na hivyo kuwapeleka kuwa na usemi mezani. In short wengi hawakukubali kupeleka tozo na ushuru kwa Familia za Wafalme wao....

.....ndilo jambo liliowaungansiha wafanyabisahara wakuu na wafanyabisahara wadogo(Machinga) yani ordinary citizen na wakubwa-Kupinga tozo, ushuru na rushwa!

Ndimo kukazaliwa U.S.A ndimo kukaja The French Revolution ....Na marevolusheni mengine lukuki Ulaya.
In short, Serikali za Kifalme zilidondoshwa na Wafanyabiashara waliochoshwa na Serikali zao na Wananchi wa kawaida waliochoshwa na wote... yaani Wafanyabiashara waliokumbatiwa na Serikali pamoja na Serikali(Familia za Kifalme) zenyewe.

Kuna mifano hai Tanzania leo hii!

Anyways wote hawa, yaani Nchi nilizozitaja hapo juu zimezaliwa ili kuondokana na Udhalimu wa Muingereza au Serikali za Ufalme......wa walipotoka baada ya mageuzi ya Kisiasa na ya Kidini..-..ila bado kukawa na Ukwasi. Kulikuwa hakuna hela, magonjwa yalitamalaki, umasikini ukaongezeka yaani Chumi za wanamageuzi hazikuwa kana zile za Ufalme walizozikataa...Ilibidi wayarudie yale yale waliyoyakataa dhidi ya Nchi zao/Falme zao. (Ndipo laana ya wazungu ilipoozaliwa)

Safari hii baraka zote zilitoka Serikalini kwenda kutafuta rasilimali kwa udi na uvumba! -Yaani warudi kulekule walikokuwa wakifanya biashara, ila safari hii Kwa mtutu wa Bunduki....Wakatwangana tena, -kumbuka safari ya kwanza ilikuwa ni kugombania maeneo ya biashara;barabara,bandari na mashamba makubwa.

ila, safari hii, ni Maeneo mahususi yenye kutoa rasilimali walizokuwa wameshaanza kuzitegemea kuendesha chumi za Serikali zao Mpya baada ya revolusheni/mageuzi

Ndio uamuzi wa kuteka(colonization) maeneo na kujenga Miundombinu yao wenywe kwenda directly kwenye Rasilimali walizozihitaji kuasisiwa

.... kugombania Visiwa, Nchi, na hata mabara- ikawa mbinde kweli kweli manake Walichinjana kweli kweli wenyewe kwa wenyewe, laana ilianza kuwarudia. ....Na ndioo

Usemi kuwa Afrika kuna laana ikazaliwa; haikuwa ina maana ya kusema Waafrika wamelaaniwa. Hapana, bali ulikuwa na maana kuwa Vita zao, baina yao sasa wanazirudia tena Afrika, yaani laana yao inawatafuna(Anathema will devour us) kwa kuendlea kuuana Afrika.

Leo hii bado ni, Mtazamo wa kizungu wa kile kilichowatokea wakigombania Rasilimali za Bara letu.(Ushahidi upo kwenye hansard za bunge Uingereza)westmisnter. na Kwingineko, nao ni kuuwana kinyama huku wakiamini na kumkufuru mungu kwa waliyowafanyia Wenyeji wa maeneo walikokuwa wakifanya Mauaji, mateso, na hata kupeleka magonjwa ya zinaa n.k kana ilivyokuwa ikiwatokea Ulaya karne zilizopita!

UN ikaja na vyombo vingine kana IMF WB WHO n.k vyombo vyote hivi vikiwa ni muendelezo wa Taasisi zlizoasisiwa na Wafanyabisahara na kupewa baraka na baadae mamalaka na Serikali zao kwa lengo moja tu, nalo ni kuhodhi madaraka na mamlaka juu ya Sehemu wanazotaka Rasilimali.

Mpaka leo hii, pamoja na kuwa kuna Serikali katika Nchi za Ulaya na Marekani- Bado nguvu ya Wafanyabishara ni kubwa hata kuliko Serikali. Amini Usiamini, the Big Corporations run these Countries when it comes to shove, yaani kwenye mambo yanayohusu Uchumi Wafanyabishara na mashirika ndio wanaokuwa na usemi. Sisi huku ndio usiseme. Tuna minywa minya tu.

Pamoja na mafanikio mengi waliyapata kutokana na private/public partnership Nchi nyingi zimekuwa zinashindwa kufanya mageuzi ya kisiasa kama wananchi wanavyodai.

Hivi sasa kuna wengine wanajuta na wanataka kurudisha maeneo nyeti ya Uchumi kama vile Miundombinu chini ya Serikali angalau kwa asilimia kubwa. Kuondokana na Monopoly.

Nchi yetu bado ni changa sana, kumuachia mtu au watu wenyekuwa na kipato chao maradufu au mara kumi ya kipato au bajeti nzima ya Serikali ya Tanzania, yaani kuendesha na nyingine za kimaendeleo, ni kujiuza mazima.

Naunga mkono uwezeshwaji wa Watanzania wenyewe. Yaani wazalendo Halisi, Waafrika. Bora, Kuliko kuja kuteswa na Makaburu

Why not, Why not, why not?

Tutakunjana karibuni sana.

Kuna watu hawafikiri strategically.

UBINAFSISHAJI ULIOFANYIKA ULAYA BAADA YA VITA KUU YA PILI (WW-2)
Ndg.wana JF, kwa ufupi tu, ule ubinafshaji uliofanyika kwa wazungu baada ya WW-2 ni tofauti sana na huu unaofanyika hapa kwetu TZ.
Wazungu wao waliwachukuwa WANANCHI wao/watu wao/makampuni Yao, aidha yakiwa ndani ya nchi ama nje, i e Europe ama USA, n.k. Wakapa na ruzuku kupitia mabanki yao. Hii iliwafanya waendelee kwa haraka kwani wote ni wamoja! Lakini sisi tunamchukuwa Mwaarabu aliyetufanya watumwa, ama Mzungu aliyetutwala)Mkoloni, eti atuendeshee biashara, viwanda, mashamba, bandari, viwanja vya NDEGE, machimbo ya madini mbali mbali, je ni kweli atatuendeleza?
Mie sielewi hii akili Watanganyika tumeipata wapi? Aidha, itoshe kusema tu kuwa sisi Watanganyika/Watanzania sote tumelaaniwa, tuna laana ama tumerogwa. Nani katuroga? Huenda hata aliyeturoga kafa labda! Shame on us! Hivi hata Waafrika wenzetu, majirani zetu hatuzomei na kutuonea huruma sisi? Mbona ktk mataifa ya Wazungu mmoja/nchi ikifanya vibaya wengine wanaingilia kati? Yaani kama EU/US, je kwetu mboa AU ipo kimya?
Hebu wana JF hapa tusaidiane kwa mjadala wa kina ili vizazi vijavyo vifahamu kuwa karne fulani sii wote walikuwa vilaza kama kina Chief MANGUNGA wa MSOWERO KILOSA MOROGORO. Huyo hakusoma, naye ni "CHIEF" Je hawa wetu ""CCM""si wamesoma? Tena na historia ya akina MANGUNGA, imrkuwaje?
Jadili, paza sauti na tuwashauri.
Wakibinafsishiwa wabongo ndio utaona shoo lake. Wabongo unawajua unawasikia??
 
Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.
Nitakuelewa sana Tena sana kama Ndugu yangu Chige na wadau wengine wa masuala ya maendeleo watakubali kujumuika kuchangia uzinwako huu. Tumsubiri.
 
Ndugu zetu wabongo hata ukiwatengenezea au kuwanunulia mfumo..watauchezea..akili zetu tunazijua wenyewe. Wacha tubinafsishe tu.
 
Nilipoona Zembwela na Kitenge wanaenda Singapore kujionea jinsi walivyo binafsisha bandari. Pale pale nilijua kuna kitu kinafuatia...

Wanasiasa wamesoma mindset za watanzania, nikiri tu wametuweza mpaka siku tutashtuka itakua ni too late.

Nb: nchi changa kama yetu kubinafsisha bandari ni mapema mno. Watu wachache wanasaliti nchi kwa manufaa ya mda mfupi.
 
Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100
Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-

19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.
Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.
Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.

b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.

d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.

e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.
Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.
f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ifike wakati Serikali iachane na kufanya biashara make huu ni ujamaa na ushakuwa proved haiwezekani zaidi ya upigaji.

Kwa taarifa zaidi soma hapa >> Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam

Mashirika ya umma kama Bandari, Tanesco, Maji, sijui Posta, TTCL, ATCL, na zinitakiwa kuingia sokoni kuuzwa.

Hiyo Bandari ya Dar kama ingejengwa ya Baganoyo na ya Bagamoyo ikawa ni private na ya Dar ikawa ni ya Serikali bila shaka meli zingehamia Bagamoyo na ya Dar ingekuwa kama TTCL now.

Tanesco angali utendaji wao, lazima wafuatwe offisini uwe unajuama na mfanya kazi mmoja wapo, na sio tu kufuatana na kuwapa rushwa juu, sasa ingekuwa inasimamiwa na watu weupe unazani kungekuwa na kufuatana offisini?

Angalia TTCL haijulikani kazi zao kwa sasa, hivi TTCL ilikuwa ni ya kushindwa hadi na wakina Haloteli? TTCL ilipaswa kuwa sawa na Vodacom, ila Kwa sababu ni Mali ya Umma hakuna anaye jali pale na imejaa wafanya kazi wengi kuliko ufanisi na hakuna anajali.

Mamlaka za maji zimejaa upigaji tupu, unafuatilia kuunganishiwa maji hadi unachoka na lazima uhonge la sivyo hutakaa uunganishiwe maji.

Kwani Bandari ikikodishwa hao wanao kodisha watakuja kuondoka nayo? Wataihamisha? Tuachane na ujamaaa
Wachache sana ndio watakaokuelewa,mfano mdogo mwendokasi tu wameshindwa kuuendesha kiufanisi na kila siku wanalalamika hasara ndio itakua bandari waliyoishindwa miaka yote,uendeshwaji wa ile bandari yetu ni kituko cha dunia kwa wakati tuliokua nao
 
Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100
Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-

19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.
Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.
Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.

b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.

d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.

e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.
Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.
f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unaweza kuweka ushahidi kama ni uwekezaji wa miaka 100?
 
Mashirika au bandari kupewa wawekezaji hakuna guarantee kwamba ufanisi utaongezeka.

Wahindi wa TRL walifanya nini au ulikuwa bado kiunoni mwa Mzee wako?

Viongozi wanafanya mambo ya kijinga na chawa mnakata viuno halafu mambo yakibuma wanakuja kuandika vitabu kukiri makosa baada ya kustaafu na hamna la kuwafanya.

Miaka 60 ya kujitawala bado tupo hoi,kwa nini uongozi wa juu wa taifa hili tusiutafutie wawekezaji?
 
Hivi amekosekana Mzungu hadi aje Mwarabu?

Lakini bado naamini Watanzania wapo waneoweza .

Tatizo ni kutaka kuteua Kwa kujuana badala ya kutangaza hizo nafasi watu waombe Na kufanyiwa usaili.
 
Hivi amekosekana Mzungu hadi aje Mwarabu?

Lakini bado naamini Watanzania wapo waneoweza .

Tatizo ni kutaka kuteua Kwa kujuana badala ya kutangaza hizo nafasi watu waombe Na kufanyiwa usaili.
Umemsahau Binamu wa Mjombashangazi ?
 
Naungana na wewe serikali kufanya biashara ni kunufaisha watu wachache tu maana wizi ni asili ya watanzania ziwekwe terms nzuri kimkataba ambazo zitaipa pesa za uhakika serikali wawaachie wawekezaji.hata ufanisi utakuwepo sana na malalamiko yatapungua sana
Hata iyo kodi tutayolipwa italiwa na wachache labda tubinafsishe na Serikali ya Ccm
 
Ishu kubwa bandari iendeshwe kisasa cargo ziingie na zitoke kwa wakati maswala ya usenge wa wabongo wanao fanya hapo kushirikiana na tra yaishe.
Bandari + tra imekuwa kichaka cha upigaji na kufirisi watu ,mjomba angu amefanya kazi hapo miaka ya 60 hadi Leo mifumo ni Ile Ile hakuna kilicho badilika. Contena zinajazana hapo muda unapotea kodi inapotea bado rushwa na ukiritimba umetawala .Bora serikali ikae bambeni ijipigie percent yake tu, huku mifumo ikiboreshwa.

Imebaki taNesco .

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Kwa hoja hii basi hakuna kitu serikali itatakiwa kubaki nacho
 
Back
Top Bottom