Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Sasa hapa Tatizo ni bandari au ni Serekali?

Kwanini unapendekeza bandari ibinafsishwe bada ya Serekali inayoshindwa kusima bandari ndio ibinafsishwe.
Watu wake, kwami wale Ma director wana share pale?
 
Hakuna nchi ambayo imebinafsisha kila kitu mzee bandari ni sehemu nyeti sana huwezi kumpa mtu binafsi aendeshe kuna mambo mengi ya kiusalama kwetu na nchi jirani ni sawa na kuzi privatelize airports haiwezekani zitakuwa ni highways za kupitishia magendo na silaha haramu .
YAANI TUMPE MCHINA NDIO ASIMAMIE BANDARI YETU LOL!!
Saa100 kichwa anakitumia kufungia ushungi amna mtu pale
 
Akili za hovyo kabisa hizi, kwa hiyo furaha yako uwape wageni wakuendeshee mambo yako wewe uendelee na story za pwagu na pwaguzi kwenye kijiwe cha kahawa.

Kama mnataka kubinafsisha kwa nini msiwambie watanzania wenyewe waunde makampuni waiendesha, au ndo ule jenerali Ulimwengu aliuita ugenishaji.​
Nyie mmeweza nini? Taka kimoja wapo mlicho weza kufanya biashara
 
Ukweli kubinafsishwa sioni kama ni busara. tuone mfumo wa uendeshaji mashirika ya umma ndio tatizzo kubwa, ubadilike, isaidie kuwabana wateule au uongozi wake. Hivi hakuna kiongozi anayeumia kwa kuchagua fisadi eti kwa sababu unamfahamu au anafahamia na wapambe wako.

Turudi kwa Rais kwa Rais Mkapa, ili kiongozi aombe, na kweka vigezo vya utekelezaji; kwamba kila mwaka anapimwa kwa utekelezaji wake na kamati maalum ya usimamizi wa mashirika ya umma. Kila shirika lijulikane madhaifu yake ya kuboresha.
Upi? Hakuna commitment pale make muda wowote mkurugenzi anapigwa chini
 
Tatizo 10% na ujinga wa viongozi kiwango cha SGR, na hata tunachopata sasa hatutapata, zitaundwa kampuni za mikobani kama Richmond then tutaambiwa ni DP Dubai, dawa ni kutafuta CEO mwenye uzoefu na uendeshaji wa bandari kubwa, apewe malengo, budget na bila kuingiliwa na wanasiasa na ikiwezekana aripoti moja kwa moja kwa Raisi (bandarini kuna pesa nyingi sana pale), hakuna haja ya kugawana na mtu yeyote wakati tunaweza kukusanya zote na zaidi, bandari sio kampuni za simu ,too much money there
 
Ccm mnauza bandari yetu miaka 100? Mkataba gani wa miaka 100? Kwa malengo Yapi? Miaka 100 mabadiliko yatakua makubwa sana hapa Duniani, Kwanini tunahukumu vizazi vyetu vitatu au vinne kwa tamaa za sasa?

Baada ya hapo atakuja mwingine ajifanye Mzalendo wakati alishiriki uchafu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii story ya Namibia inaonekana ni kama 100% kilichotokea Namibia.

Soma hapo chini

"In 2019, DP World, a Dubai-owned port operator, under the aegis of Sultan Bin Sulayem, with support from the former Transport Executive Director, Willem Goeimann orchestrated a plan to gain control of the newly constructed N$4.2 billion Walvis Bay container terminal through a direct agreement for a period of 50 years.

DP World’s strategy included extending unwarranted generosity to several Namibian decision makers, some of whom were completely oblivious of their true intent; to avoid a competitive process that would most probably undercut their chances of controlling this strategic asset. To bypass Namibia’s procurement laws and justify a direct agreement, DP World’s agents pushed for a largely farcical Government-to-Government agreement between UAE and Namibia, which was a mere smokescreen, hiding DP World’s real motive. This deception was clearly manifested when they signed an MOU with Nara Namib to develop a Free Economic Zone in Walvis Bay.

It was considered dangerous and inimical to the interest of Namibian People but it seems no one made the effort to analyse it in detail.

For unscrupulous foreign opportunists all you need is the opportunity, an architect to draft the master plan, a local agent that knows how to manipulate the system, a few key officials and the unscrupulous foreign investor to exploit Namibia and deprive it of real economic development".


Aisee ndio maana nilimsikia Mbunge mmoja akiwasifia sana baada ya kwenda ziara huko Dubai. Kumbe ndio zao hawa Mabwana. Haya kila la kheri waungwana.
 
👀Muda Wa Kubembelezwa Umefika Sasa
 
Ccm mnauza bandari yetu miaka 100? Mkataba gani wa miaka 100? Kwa malengo Yapi? Miaka 100 mabadiliko yatakua makubwa sana hapa Duniani, Kwanini tunahukumu vizazi vyetu vitatu au vinne kwa tamaa za sasa?

Baada ya hapo atakuja mwingine ajifanye Mzalendo wakati alishiriki uchafu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Alhaji Mwinyi Alivyifanya Loliondo Kuitoa Miaka 100 Kwa Mwarabu
Yanakwenda Kukamilishwa Tena Na Mama Anawapa Tena Waarabu Bandari Miaka 100
 
Huu ni ukoloni wa kidigitali/ Digital era colonialism ndio hizi hadithi wanakuja na mifumo yao ya kisasa. Huu ni ukoloni ule ule kwa mbinu za kisasa. Mifumo gani ambayo mswahili wa leo hawezi kuweka? Kuna wakati tuliaminishwa miamala ni Maximalipo tu mbona kuliwekwa mifumo mengine ya kiserikali na mambo yanaenda. Kinachotakiwa ni utashi na mitazamo ya waliopewa jukumu la kuongoza wenzao.

Binafsisheni na majeshi nayo kama mmeaamua kujitoa ufahamu kiasi hiki.
 
Wewe ukiunga mkono haimaanishi jambo hilo ni halali.
 
Serikali imejaa wezi na wapigaji? Unakubali kuwa sisi Kama sisi hatuwezi kuendesha hata hii serikali?

Kama tatizo ni wapigaji, si Kuna mamlaka ? Kuna raisi? Kwa nini hao wapigaji wasiadhibiwe? Au unataka kusema raisi na vyombo vya dola hawawezi kusimamia serikali?

Kesho wapaji wakiwa ikulu, inabidi ikulu nayo apewe mtu wa nje kuiendesha?

Tunatetea Jambo ambalo ni gumu
Kubali tu hata ubishe vipi huo ndiyo ukweli. Kwani TTCL imekodishwa? Angalia performance yake ilivyo
 
Sipendi ubinafsishaji wa Bandari ya Dar sababu itaondoa uwezo wa Clearing Agents ku clear mizigo kwa kodi ya chini kwa faida ya mteja haswa magari yaliyoyochakaa ambayo ni over taxed. Kwa mfumo uliopo, Clearing Agents wana nafasi kubwa ku clear mizigo kwa kodi ya chini kuliko ile ambayo TRA wangedai. Hii ni win-lose situation. Hakuna mtu mwenye akili nzuri anayetaka kulipa kodi ya TRA ambayo inaenda kununua Land Cruiser LC300 na kujenga mahekalu ya MaCCM.
 
Back
Top Bottom